LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
Katika ulimwengu wa roho kinachotofautisha kati ya wanyama na mimea ni kitu kimoja tu nacho ni "Ini". Ndiyo, ini ndiyo kitu pekee kinachotofautisha kati ya wanyama na mimea (katika ulimwengu wa roho).
Maana yake ni kwamba, kama kuna kiumbe ambacho kwa muonekano wa nje kina sifa zote za kuwekwa katika kundi la wanyama lakini kiumbe hicho hakina ini basi katika ulimwengu wa roho kiumbe hicho huwekwa katika kundi la mimea na katika uganga na uchawi hutumika kama mmea.
Mfano, asilimia kubwa ya wadudu (kama siyo wote kabisa) hawana ini. Katika ulimwengu wa rohoni wadudu walio wengi huhesabiwa kama mimea na hutumiwa katika uganga na uchawi kama mimea (asilimia kubwa ya majina ya mimea inayotajwa na waganga na wachawi ambayo hayajulikani huwa ni majina ya hawa wadudu).
Je, ulikuwa unalijua hilo? Jibu ni hapana ulikuwa hujui.
Duniani kuna watu ambao wana figo tatu. Wewe unayesoma andiko hili unaweza kuwa miongoni mwa hao binadamu. Je, ulikuwa unalijua hilo? Bila kusoma uzi huu ungeweza kulijua hilo? Kama ulikuwa unalijua basi amani ya bwana iwe nawe, lakini kama ulikuwa hujui basi leo ndiyo umejua.
Kwanini nasema hivyo? Nasema hivyo ili kukujulisha kwamba yapo mambo ambayo huyajui lakini yanatokea.
Miongoni mwa mambo usiyoyajua ni kwamba katika timu zetu za mpira wa miguu huwa kuna wachezaji wanao beba nyota za mafanikio ya timu hizo (kama ilivyo kwenye makampuni, taasisi, biashara, familia na kadhalika).
Timu zinazo tambua ukweli huu huwa zinawalinda wachezaji hao kwa hali na mali. Kampuni/biashara zinazotambua jambo hili huwa zinawalinda sana wafanyakazi wenye nyota za mafanikio ya kampuni kwa hali na mali.
Familia zinazo tambua kuhusu ukweli huu huwa zinawalinda sana watoto wenye nyota hizo n.k.
Niende moja kwa moja kwenye mada yangu.
Kwa sasa mchezaji anayebeba nyota ya mafanikio ya timu ya Yanga si mwingine ila ni Jesus Ducapel Moloko. Sikutaka kuliongea hili hadharani lakini imenibidi nifanye hivyo hata hivyo.
Wakati wa dirisha la usajili nilisikia tetesi eti Yanga wanataka kumtoa Moloko kwa mkopo Singida Big Stars, nikalewa bila kunywa. Nilikuwa kama, hawa viongozi wa Yanga hivi wanajielewa kweli? Lakini alhamdulilahi haikuwa hivyo, Moloko bado yupo Yanga.
Kwahiyo katika ulimwengu wa nyota, Moloko ndiyo anayebeba mafanikio ya Yanga kwa sasa.
Viongozi wa Yanga lazima mjifunze kusogea kama vijana wa Isachar. Viongozi wa Yanga lazima mumlinde huyu mchezaji Moloko. Moloko lazima afanywe kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Yanga na siyo dada hivi anavyotumiwa kama ziada.
Provided all the factors remain constant, Moloko anatakiwa acheze kila mechi. Ama aanze au aingie kipindi cha pili lakini kwa yote Moloko anatakiwa awe anacheza dakika zote tisini.
Sitaki kuongea mengi sana ndugu zangu lakini kwa ufupi ndio hivyo. Kwa habari za upande wa kinyota kama Yanga kweli wanataka kufanikiwa basi wanatakiwa wamuangalie Moloko kwa hicho ambalo Simba wanamuangalia Tshabalala.
Mchezaji anayeichafua nyota ya Yanga ambae kwa hesabu za kinyota katika ulimwengu wa rohoni hakutakiwa kabisa kuwepo Yanga hivi sasa.
Kumradhi kwa kusema hili kwa umma lakini mchezaji huyo si mwingine ila ni Tuisila Kisinda. Kwa hesabu za ulimwengu wa kiroho, Kisinda haitakiwi kabisa kuchezea Yanga. Uwepo wa Kisinda kwenye kikosi cha Yanga unaichafua nyota ya Yanga katika ulimwengu wa kinyota.
Yanga hauwezi kupata mafanikio yoyote kama Tuisila atasalia kwenye kikosi.
Kuna sababu za kiroho kwanini "Mungu" alimtoa Yanga na kumpeleka Berkane. Msimu uliyoisha kama Tuisila angekuwa kwenye kikosi cha Yanga, Yanga wasingechukua ubingwa.
Sitaenda kwenye maelezo lakini itoshe tu kusema kwamba kwasababu za kinyota Tuisila haitakiwi hata kuwepo kwenye benchi la Yanga. Viongozi wa Yanga walifanya kosa kubwa sana kumrejesha Tuisila bila kuwajulisha wazee wenye hekima ndani ya Klabu ya Yanga.
Kichekesho cha kinyota.
Moloko anawekwa benchi, Tuisila anapewa nafasi ya kucheza.
Katika ulimwengu wa roho kosa linalofanywa na Yanga kuweka mbadala wa Moloko na Kisinda ni sawa na kosa walilofanya Wayahudi kumkataa Yesu na kumpa nafasi Baraba.
Nini kifanyike?
1. Moloko arejeshewe namba yake, alindwe, na afanywe kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi. Kamwe asitumiwe kama ziada.
2. Kisinda aondolewe ndani ya kikosi cha Yanga haraka iwezekanavyo, vinginevyo, hakuna matumaini kwa kesho ya Young Africans.
Kama Kisinda atabaki ndani ya kikosi cha Yanga nini kitatokea?
Young Africans watatikiswa kutoka katika kiti chao stahiki cha mamlaka. Yanga mwaka huu haitobeba ubingwa wa ligi na mafanikio ya Yanga kama timu yataporomoka haraka. Inaweza kuwachukua miaka mitatu kurudi tena kwenye sehemu yao asilia.
Mechi ya Jumamosi kama Yanga watashinda, basi nitaidharau sana kamati ya ufundi ya Makolo.
#kilichowaangusha Yanga dhidi ya Al Hilal si kingine, ni bahati tu ambayo ndiyo hiyo nyota. Nyota zilikuwa chini sana.
Kumbuka maneno yangu.