Huyu ndo kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini

Huyu ndo kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini

Kwa nini? Kuanze kumulikwa kwenu kwanza ndio wamalizie Mtwara. Machafuko ya gesi hatujayasahau bado halafu unataka watuletee mengine. Pimbi wewe jamii ya wafugaji...
Kulikua kuna ulazima wa kunitusi mkuu??? kuna kitu unatafuta si bure.
 
Huyu jamaa kwa sauti yake tu nilivyoisikia ni mmojawapo wa viongoz wa chama cha siasa
 
Kwa polisi hapo kachokoza moto,watamkamata tu siku si nyingi,vitu anavyotaka kufanya kwa Tanzania haviwezekaniki,sehemu nyingine wanakuwa na sapoti ya baadhi ya wananchi wa kawaida,kwa Tanzania sapoti hiyo kamwe hawawezi kuipata na polisi jamii itafanya kazi yake.
 
the journey has just begun,spinin zitakuwa za kutosha mwaka huu,sa cjui hii record inaitwaje!!!
 






HATIMAYE kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti hili kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!


Ijumaa liliunasa mkanda huo kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa kujitambulisha kwa jina wala kusema anakotokea hapa nchini huku akisema: “Una maneno ya hatari sana, naogopa kujianika, nitauawa.”

Hatimaye kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti la Ijumaa kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!

Gazeti hilo linadai kuunasa mkanda huo kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa kujitambulisha kwa jina wala kusema anakotokea hapa nchini.

Bin Abdullah ametumia dakika 11: 03 kuzungumzia mambo mbalimbali lakini kubwa kuliko yote ni kuliponda Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuwakamata wenzao katika imani na harakati (zinazohifadhiwa kwa sasa) na kuwashikilia kwenye mahabusu mbalimbali nchini.

Alianza kwa Kusema:
Bin Abullah ambaye kwenye mkanda huo amevaa nguo nyeusi kama ninja na miwani ya giza, alizungumza kwa kirefu, akitoa wito lakini mbele akasema:

“Tumeshaungana ili kupambana. Mkoa wa Mtwara zaidi ya wenzetu kumi na saba walikamatwa kwa makosa ya dhuluma, makosa ya kupanga, makosa ya ugaidi.

Ishirini na moja wamekamatwa Zanzibar wako katika Gereza la Segerea (Dar). Wenzetu wengine kumi na nane wamekamatwa Mwanza wako katika Gereza la Kisongo, Arusha. Ndugu zangu, wenzetu wengine kumi na saba wameuawa Mtwara kwa amri ya ...(anamtaja waziri).” “Subira yetu imefika mwisho na tulichokuwa tunasubiri Mungu ameshatupa. Tunatoa ahadi kilichopo hivi sasa tunatoboa jahazi wote tuzame.

“Tunatoa rai, wenzetu waliopo Gereza la Kisongo waachiwe huru. Hapa hatumtishi mtu yeyote yule.”“Pili, agizo la Ernest Mangu IGP, umetangaza uliwenguni kwamba umewakamata wote waliovamia vituo vya polisi na umezikamata silaha zote. Ukweli ni kwamba unatetea tumbo lako. Hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na wala silaha hazijakamatwa.

“Mungu ametukubali. Katika Kituo cha Polisi Ushirombo (Kilimanjaro) tumeweza kuvamia kituo, tukaweza kutoa roho za polisi na tukaweza kuchukua silaha, tunazo.

“Tumevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri (Pwani), tumeweza kuchukua silaha za kutosha, tumeweza kuchukua mabomu ya kutosha. Tunazo silaha tunasubiri muda zianze kufanya kazi.“Ernest Mangu nakupa changamogto, hivi sasa tuna uwezo...(maneno yanahifadhiwa kwa usalama) wakati wowote ambao tunataka.

“Tumeweza kuchukua silaha bila kuwa na silaha yoyote. Ndugu zetu wa Tanga wameweza kuchukua silaha wakiwa hawana silaha yoyote. Ikwiriri tumechukua silaha tukiwa hatuna silaha yoyote, mpaka sasa tumeshachukua roho tano za polisi.“Ndugu zangu, ...mlikuwa mkinisubiri nitoe tamko, natoa kauli rasmi...” alihitimisha Abdullah, huku vitisho vya jumla kwenye tamko lake vikiwahusu polisi, viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na mikusanyiko ya ibada.

Tamko la IGP

Baada ya video hiyo,Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu na kuzungumza naye kuhusu mtu huyo na kumkabidhi video ambapo alisema: “Nawashukuru sana kwa kuleta video hii, huu ndiyo ushirikiano unaotakiwa, nawaomba wananchi video za aina hii wazikatae kwa sababu ni kosa kuwa nazo na watu kadhaa wameshakamatwa kwa kuwa nazo.

“Sisi kama jeshi la polisi tunajua kuwa kuna watu wanadhani kufanya uhalifu kama huo kutawasaidia kutimiza matakwa yao, lakini ukweli ni kwamba polisi wapo imara na nina uhakika watuhumiwa watakamatwa kwa kushirikiana na raia wema.”

Shehe Mkuu Amkana

Baada ya kuzungumza na IGP, Gazeti lilimtafuta Shehe Mkuu Tanzania, Mufti Shaban Simba na kumsimulia kuhusu kuibuka kwa Bin Abullah na kutaka kujua pengine anamfahamu. “Kwanza hizo taarifa hizo ndiyo nazisikia kutoka kwako. Hilo jina ulilonitajia (Bin Abdullah) sijawahi kulisikia labda muangalie kwa wenzetu upande wa pili.”


Chanzo:
GPL


Mmmmhhhh this is drama kwa kwel.
Maigizo maigizo tuuuu, tena haya ya bongo movie kabisa. Ni mwny akili ndogo tu atayaamin haya maigizo. Ila serikali hii inatuona ss watanzania hatuna akili kabisa.

Hiyo source ynyw eti GPL.
 
Last edited by a moderator:
Huyu jamaa kama anafanya utani...basi analo maana utani wake umepitiliza. Lakini kama anasema na anafanya kweli...eeh Mungu tuepushe na hili balaa!
Bado napata shida kuamini hii kitu ila si vizuri kupuuzia vitu kama hivi. Pia najiuliza why now , unakumbuka mwaka flani wa uchaguzi mkuu kuliiibuka mambo kama haya sasa je haya yote ni uchaguzi au what is behind the scene.
 
CCM NOMA SANA, YAANI KWA PROPAGANDA HAWAFAI.. hadithi hii ni ya kitoto,,, na hakuna ugaidi wa kitoto kama huu duniani,eti uanzishe ugaidi kwa kuiba bunduki kwenye vituo vya polisi si utoto huu,, CCM acheni kumwaga damu za watu eti kuwatia woga wananchi!!!
Unajua nami nimefikiria hivi hivi halafu why now , kwanini hawakujitangaza kipindi cha mabomu yaliyokua yanarushwa sehemu kadhaa hadi kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha. Halafu ukiangalia vizuri video hii iko wazi kabisa sasa kwa watu wenye utaalamu wa mambo haya ni rahisi kwao kumjua.
 
Hapa ndipo uzalendo wahitajika lolote baya kuwahi kutaarifu mie mwislam tena mwenye zoote sifa kamwe siwezi toa nafsiya mwandam nisie na chukinae tujumuike kuilinda nchi yetu tutakae adhirika nisie raia
Mwenzetu wewe tayari unao uwezo wa kujilinda manake wakiona hiyo bodi yako tu lazima watoke nduki lol
 
Chanzo cha habari chenyewe gazeti la udaku lingekuwa mwananchi au nipashe ningeamini lakini udaku hauna ukweli ndani yake
 
Maendeleo ya Sultan Mangungu haya..sasa ivi hadi Tz kuna akina Abubakari Shekau 2.0 ndani ya this crazy semi-anarchy bongoland...!
 
Kama hii taarifa haina ukweli wowote, ninadhani GlobalPublishers inabidi wapewe onyo kusambaza habari kama hizi za kigaidi kwa umma na kutengeneza panic. Kwanini huyo aliyewapatia copy hawajampeleka polisi kwa maswali zaidi?
 
Sasa mbona wamechagua sehemu mbaya ya kupigia picha?? Yaani wamejiweka wazi kabisaa
 
Habari zilizonifikia mda huu Ni kuwa,kuna mapambano makali sana yanafanyika huko handeni tanga kwenye mapango ikisadikika kuwa alshababu wamejificha huko,imetanganzwa ATV mchana huu
 
Nina wasiwasi hii ni janja ya ccm kutuogopesha ili tusijitokeze kwenywe uchaguzi. Lazima tuhakikishe tunasimama imara kuwang'oa pamoja na vitisho vyao. Mungu ibariki Tanzania.

Tukupime kama we ni mtanzania ila we kama sio mbongo basi nenda hatukupimi akili
 
Kazi imeanza sasa,tushazalisha akina boko mara hii?mbona tumewah sana
 
Back
Top Bottom