Huyu ndo kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini

Huyu ndo kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachoua polisi na kuiba silaha kwenye vituo nchini

jaman hii kitu iko siriaz o jaman yasije yakawa ya kama wenzetu
 
Duh, hivi Tanzania tunaelekea wapi? pili Tanzania ni ya nani? tatu jeshi la polisi musikalie kuzuia maandamano ya upinzani wakati amani ya Nchi hii iko Rehani, pili hebu tutafute source ya kuibuka kwa haya makundi walianza Panya road hapa juzi mpaka wakaleta madhara ya kutosha ndipo jeshi letu lilipochukua hatua, hivi jeshi la polisi Tanzania hamna intelijensia au intelijensia yenu inafnaya kazi kuzuia maandamano ya amani?

Jambo lingine la msingi TZ ni mali yetu sote amani ya nchi hii ikitoweka haijalishi wewe ni nani, una nafasi gani, au una amini imani gani? boko haramu walianza kama hivyo leo hii hawabagui kuwa wewe ni muislamu au mkristo ukiingia site yao huna roho, Al-shabab walianza taratibu kama abdullah lakini leo hii mauaji yao hayajali uislamu wala ukristo MTANZANIA AMKA CHUKUA HATUA YA KUJILINDA NA KUILINDA NCHI YAKO, maana ya AMANI YAKO NI AMANI YA NCHI YAKO.

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU WABALIKI WATANZANIA.
 
danganya Toto Hii, sijui wamemlipa vipande vingapi vya pesa kuwatia hofu watanzania? but lazima kieleweke mwaka huu serikali mboovuu
 
nngu007

Nakataa kabisa,sijaona autheticity ya hii clip.hii ni propaganda tu,hii ni kutishana tu.sioni mantik ya huu ujumbe,tunaelekea uchaguzi tutaona mengi sana mwaka huu.


i'm just a Messenger loving my country 2 death; That's is all what i have got...

Please don't deny what's happening in our beautiful peaceful land... is no 'GOOD'
 
mtwara ni eneo la kumulikwa sana na vyombo vya usalama, ni eneo la kumulikwa sana!!!!
Kwa nini? Kuanze kumulikwa kwenu kwanza ndio wamalizie Mtwara. Machafuko ya gesi hatujayasahau bado halafu unataka watuletee mengine. Pimbi wewe jamii ya wafugaji...
 






HATIMAYE kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti hili kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!


Ijumaa liliunasa mkanda huo kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa kujitambulisha kwa jina wala kusema anakotokea hapa nchini huku akisema: "Una maneno ya hatari sana, naogopa kujianika, nitauawa."

Hatimaye kuvamiwa kwa vituo vya polisi na kuporwa silaha huku askari wake wakiuawa kikatili kumejulikana kunafanywa na nani kufuatia gazeti la Ijumaa kunasa mkanda wa video wa mtu mmoja anayejiita Kaisi Bin Abdullah akijitapa kufanya hivyo kwa lengo la kukusanya silaha ili kulipa kisasi siku si nyingi!

Gazeti hilo linadai kuunasa mkanda huo kutoka kwa mtu mmoja aliyekataa kujitambulisha kwa jina wala kusema anakotokea hapa nchini.

Bin Abdullah ametumia dakika 11: 03 kuzungumzia mambo mbalimbali lakini kubwa kuliko yote ni kuliponda Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuwakamata wenzao katika imani na harakati (zinazohifadhiwa kwa sasa) na kuwashikilia kwenye mahabusu mbalimbali nchini.

Alianza kwa Kusema:
Bin Abullah ambaye kwenye mkanda huo amevaa nguo nyeusi kama ninja na miwani ya giza, alizungumza kwa kirefu, akitoa wito lakini mbele akasema:

"Tumeshaungana ili kupambana. Mkoa wa Mtwara zaidi ya wenzetu kumi na saba walikamatwa kwa makosa ya dhuluma, makosa ya kupanga, makosa ya ugaidi.

Ishirini na moja wamekamatwa Zanzibar wako katika Gereza la Segerea (Dar). Wenzetu wengine kumi na nane wamekamatwa Mwanza wako katika Gereza la Kisongo, Arusha. Ndugu zangu, wenzetu wengine kumi na saba wameuawa Mtwara kwa amri ya ...(anamtaja waziri)." "Subira yetu imefika mwisho na tulichokuwa tunasubiri Mungu ameshatupa. Tunatoa ahadi kilichopo hivi sasa tunatoboa jahazi wote tuzame.

"Tunatoa rai, wenzetu waliopo Gereza la Kisongo waachiwe huru. Hapa hatumtishi mtu yeyote yule.""Pili, agizo la Ernest Mangu IGP, umetangaza uliwenguni kwamba umewakamata wote waliovamia vituo vya polisi na umezikamata silaha zote. Ukweli ni kwamba unatetea tumbo lako. Hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na wala silaha hazijakamatwa.

"Mungu ametukubali. Katika Kituo cha Polisi Ushirombo (Kilimanjaro) tumeweza kuvamia kituo, tukaweza kutoa roho za polisi na tukaweza kuchukua silaha, tunazo.

"Tumevamia Kituo cha Polisi Ikwiriri (Pwani), tumeweza kuchukua silaha za kutosha, tumeweza kuchukua mabomu ya kutosha. Tunazo silaha tunasubiri muda zianze kufanya kazi."Ernest Mangu nakupa changamogto, hivi sasa tuna uwezo...(maneno yanahifadhiwa kwa usalama) wakati wowote ambao tunataka.

"Tumeweza kuchukua silaha bila kuwa na silaha yoyote. Ndugu zetu wa Tanga wameweza kuchukua silaha wakiwa hawana silaha yoyote. Ikwiriri tumechukua silaha tukiwa hatuna silaha yoyote, mpaka sasa tumeshachukua roho tano za polisi."Ndugu zangu, ...mlikuwa mkinisubiri nitoe tamko, natoa kauli rasmi..." alihitimisha Abdullah, huku vitisho vya jumla kwenye tamko lake vikiwahusu polisi, viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na mikusanyiko ya ibada.

Tamko la IGP

Baada ya video hiyo,Gazeti la Ijumaa lilimtafuta Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu na kuzungumza naye kuhusu mtu huyo na kumkabidhi video ambapo alisema: "Nawashukuru sana kwa kuleta video hii, huu ndiyo ushirikiano unaotakiwa, nawaomba wananchi video za aina hii wazikatae kwa sababu ni kosa kuwa nazo na watu kadhaa wameshakamatwa kwa kuwa nazo.

"Sisi kama jeshi la polisi tunajua kuwa kuna watu wanadhani kufanya uhalifu kama huo kutawasaidia kutimiza matakwa yao, lakini ukweli ni kwamba polisi wapo imara na nina uhakika watuhumiwa watakamatwa kwa kushirikiana na raia wema."

Shehe Mkuu Amkana

Baada ya kuzungumza na IGP, Gazeti lilimtafuta Shehe Mkuu Tanzania, Mufti Shaban Simba na kumsimulia kuhusu kuibuka kwa Bin Abullah na kutaka kujua pengine anamfahamu. "Kwanza hizo taarifa hizo ndiyo nazisikia kutoka kwako. Hilo jina ulilonitajia (Bin Abdullah) sijawahi kulisikia labda muangalie kwa wenzetu upande wa pili."


Chanzo:
GPL

Fake. Sisi nguli wa hisabati hatuwezi kuikubali hii taarifa hasa hio video. pumbaf..GPL. Hii video imekaa kingese ngese sana kuliko mnavyoifikiria GTs...
 
Last edited by a moderator:
Mmmmhhhhh!!!

Haiingii akilini! Aliyewapa mkanda amekataa kujitambulisha, wala kusema anatokea wapi hapa nchini, lakini GPL wakachukua mkanda tu kutoka kwake, na yeye wakamwacha aende zake kwa amani. Kwa nini wasimfiche mahali? Kwa nini mkanda huu unaletwa wakati wa kusikiliza kesi ya Ponda, na vuguvugu zito la Zanzibar linalohoji kwa nini Mashehe wa Uamsho washitakiwe Bara? I'm smelling a rat! Ni yaleyale ya "Mkenya" wa Kova "aliyekwenda kutubu kwa Gwajima"
 
Kituko cha Karne: Eti gaidi linasema "Mheshimiwa Rais"! Hii ni sawa na Kiongozi wa Boko Haram kusema "Mheshimiwa Rais wa Nigeria" au Osama bin Laden wa enzi hizo, kusema "Mheshimiwa Rais Obama" Hata kuigiza basi, muwe mnatumia akili! This is too low!
 
Hanajidai kuvamia vituo vyetu vya polisi bila silaha na kuondoka na silaha za kutosha!!
suluhisho jeshi la polisi linyimwe silaha na zipelekwe JWTZ, wao wapewe virungu nondo mishale na sime.

Halafu iangaliwe upya huenda wanatuzuga pengine watakuwa wameshapata kontena la silaha toka nje sasa wanatupoteza. iweje uvamizi ulioelezwa utoe tambo kubwa kama ilivyoelezwa, polisi pia jamani wanatoza pesa kwa raia na kula kuku vitambi duh!
 
CCM NOMA SANA, YAANI KWA PROPAGANDA HAWAFAI.. hadithi hii ni ya kitoto,,, na hakuna ugaidi wa kitoto kama huu duniani,eti uanzishe ugaidi kwa kuiba bunduki kwenye vituo vya polisi si utoto huu,, CCM acheni kumwaga damu za watu eti kuwatia woga wananchi!!!
 
Watanzania msidanganyike. Hii video imeandaliwa na CCM kwa makusudi maalum. Kumbukeni huu ni mwaka wa uchaguzi na CCM maji yako shingoni. Lazima Waanze kutafuta mbinu chafu na hata ikiwezekana kuwaua viongozi wakuu wa upinzani kwa kisingizio cha ugaidi.
 
Nyumba za ibada mara nyingi ushambuliwa kwa msukumo wa chuki tu ,ndugu zangu mnaelewa nyumba gani zinazolengwa,mtetezi wa hizo nyumba yu hai atazifunika kwa mbawa zake.Ole wenu mnaoshiriki kuukaribisha ugaidi hapa tanganyika kumbukeni hata family zenu hazitabak salama,labda kama mtazipeleka kuishi falme za kiarabu na kwenye mataifa yanaongozwa kwa imani zenu
 
Mimi mkuu nimecheka sana aliposema Ushirombo (Kilimanjaro) mwandishi mburura huyu hata hajui Ushirombo iko wapi? Hata kama kwenye mkanda jamaa amejichanganya akasema hivyo, wewe kama mwandishi huwezi kumrekebisha? SHIGONGOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!
Alivyo sikia Ushirombo akaona inafanana na Rombo akajua lazima itakuwa Kilimanjaro. Kazi ipo kwa waandishi wetu!
 
Vyombo husika vichukue taarifa hizi kama changamoto na kuzifanyia kazi, mbuyu ulianza kama mchicha na akumulikae mchana usiku atakuunguza
 
Back
Top Bottom