Huyu Polisi wa zamani Marehemu Mkama Sharp alikuwa na Kipaji gani ambacho Polisi wengi wa sasa hawana?

Sie tulieishi Gerezani tunamkumbuka sana Mkama sharp alikuwa anatembea na pistor mbili huku na huku pia Rungu na mikwara kibao. Siku kuna ngumi railways Gerezani kati ya Stanley na Sep wanana au Charles Libondo (Mawe Zambia)au Simba na Yanga Taifa ndo utamjua vizuri mkama sharp kwa mbwembwe. Pale jiran na msimbazi police mtaa wa kibambawe alikuwa mbabe mmoja hatari ambaye mkama sharp alikuwa haongei. Jamaa mbavu nene anaitwa Baba Jua,Huyu jamaa aliwai kuwa Bouncer wa Dar inter ya Marijani Rajabu. Alikuwa mtu hatari sijapata kuona RIP Baba Jua
 
Huyo polisi alikuwa Oyster bay pale nakumbuka miaka Ile alisumbua Sana mitaa ya Kinondoni manyanya,aibu,Togo,ufipa na mitaa ya Brazil, Moscow na mkwajuni
 
Mmoja kati ya mapolisi walioipenda sana kazi yake na kuwa proud.
Akiingia uwanja wa Taifa kutekeleza majukumu yake , kiatu safi, kiunoni kirungu na pingu zinazo ng'aa, filimbi na kash kash nyingi tu.
Kiujumla Mkama Sharp alikuwa proud na kazi yake na watu walimpenda.
 
Siku hizi kajichokea tu ni ocd huku manyara kituo nimesahau jina,ujanja wote kashindwa kumdhibiti mwanae kawa mdangaji sugu utafikiria sio mtoto wa sabasita
 
Nitafute nikuonyeshe
 
Alikuwa bondia huyu
 
Siku hizi kila sehemu ilikuwa kimbilio la ajira ma fursa
 
Unamkumbuka kitonsa, alikuwa bonge la mtu ndio walikuwa wa mwanzo kuendesha gari la polisi la kupeleka wahabusu mahakamani (karandinga)
 
Wa hivyo wapo wengi...sema unamjua huyu tu
 
Kwa nini wewe kila unapomtaja jina unaandika Nkama Sharp ila wengine wanaandika Mkama Sharp? Usahihi ni upi?
 
Hata mimi namkumbuka. Ila kwangu naona ni kama chongo kwenye kundi la vipofu. Nadhani ushamba wetu hasa enzi zile za zamani ndizo zilimkuza zaidi. Naomba nieleweke kuwa sisemi kuwa alikuwa ''mzuri'' wa kazi yake lakini nasema tu ''uzuri'' wake ulipaishwa na ushamba na woga wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…