Hawa jamaa kila wakati wakifanya ujinga wao huwa wanaumbuka, na kwa jinsi wanavyohangaika hivyo inaonesha wazi pressure imeanza kuwapanda wananchi wameshajua ukweli hayo masoko huunguzwa kwa makusudi usiku.
Naona hata soko la Kariakoo lilichomwa na wajanja kwa makusudi ili wafanye mambo yao, ndio maana majibu ya tume iliyoundwa hawayatoi kwa wananchi, hili la Karume ndio Mungu kawaumbua.
Hii inaonesha hili taifa letu kwa sasa kuna wahuni wana nguvu sana, wanaweza kujiamulia kufanya lolote baya kwa wananchi na wasifanywe chochote na vyombo vya dola, wameviweka mfukoni.