Huyu trafiki kumkaribia hivi Rais sio hatari?

Huyu trafiki kumkaribia hivi Rais sio hatari?

Ni kama alikua na jambo lake, kwa nini aeleke kule kule kwa rais...
Msafara wa Rais huwa unatisha, walinzi, askari wenye mitutu huwezi kusema umejisahau au kupotea. Sasa yeye sijui alitaka apite chini kabisa ya Mama
 
Mkuu tuwe wakweli hapo walinzi wote walikuwa alert ndio maana amefukuzwa kusogea karibu.
Ndio walikuwa alert lakini umeona walikuwa 'concerned' naye? Wamemtizama kwa sekunde kadhaa, hizo sekunde zimekuwa destruction kwao
 
Msafara wa Rais huwa unatisha, walinzi, askari wenye mitutu huwezi kusema umejisahau au kupotea. Sasa yeye sijui alitaka apite chini kabisa ya Mama
Alikua na jambo lake, na attention waliyompa pale ni ya hatari sana...

Maana ile mistake ya concentrate nae ni mbaya sana...

Mpambe wa Rais nimependa hakua distrusted kabisa...
 
Niambieni ni kuanzia dakika ya ngapi ili na mm niangalie maana video ni ndefu
 
Alikua na jambo lake, na attention waliyompa pale ni ya hatari sana...

Maana ile mistake ya concentrate nae ni mbaya sana...

Mpambe wa Rais nimependa hakua distrusted kabisa...
Mpambe naye alishusha mikono kama kuwa tayari kwa lolote na yeye kamuangalia kwa muda mrefu wakati jamaa anaondoka
 
Sasa kam
Kuuliza si ujinga, wengine utaalamu wetu ni kwenye kuhesabu pesa counter, Je kitendo cha huyo Traffic kumkaribia Rais namna hiyo sio Security Breach?

Ukiangalia kwa umakini alikaribia mno tena kupita nyuma ya hao Walinzi wenye silaha nje nje, kwa akili zangu za kawaida naona hatari maana kama mtu mbaya na mwenye mafunzo anapita karibu hivyo anaweza kuwapokonya hao akafanya fujo

Lakini pia baada ya kuambiwa huku usipite pita huko akamgusa huyu afisa mmoja kiunoni kwa nyuma kiasi anaweza kugusa silaha iliyofichwa mfukoni.

Na kuonesha kuwa halikuwa jambo la kawaida, amevuta attention ya karibu wana usalama wanne mpaka watano mpaka waliokuwa karibu kabisa na Rais, kiasi wamegeuka na kumtizama kwa sekunde kadhaa wakati anaondoka, hata huyo Kamanda aliyepigiwa saluti hajamuelewa kabisa huyo askari kamuangalia kwa mashaka.

Hiyo haiwezi kuitwa Security Breach au ni kawaida tu



View attachment 1846143



Sasa Kamanda kapigiwa Saluti halafu hajajibu. Hii ni sawa?
 
Huyo trafiki ni kama amefanya kusudi kumsukuma mwanausalama baada ya kuelekezwa kwa kupita. Kimsingi, hapo kulikuwa na makosa na huyo trafiki hakufanya vyema kumsukuma mwanausalama na kumtwangia saluti mkuu wake tu.

Lipo jambo la kuchunguzwa na kurekebishwa hapo. Binafsi, sikupenda namna huyo trafiki alivyomsukuma kwa makusudi( tazama mkono wake wa kushoto) mwanausalama.
Nimeona mkuu, Hii ni Ignorance sababu mwisho wa siku wote ni wanausalama. Hakuna atakachofanywa. Jiulize angekuwa ni Raia wa kawaida kama Bwana Petro ingekuwaje.

Hii concept ya kuamini zaid wanausalama ndo inatumika sana kwenye assasinations attempts za viongozi wengi. Mfano Laurent Kabila, Abeid Karume, n.k .

Timu ya Ulinzi wa Kiongozi tu ndo inapaswa kuwa na jukumu hilo.Tena body contact inawahusu wachache zaid kutokana na perimeter wanazopewa. Wengine wanakuwa treated kama civilians tu
 
System iliyokamilika ina CHECKS AND BALANCES.

What if ulinzi wa Raisi ulikuwa unatestiwa hapo jinsi utakavyo-react?

Cha muhimu ulinzi wa Raisi uwe makini zaidi na zaidi.

Kuna uwezekano wakapigwa chini wote hao.
 
Mhmhmhmh!

Tuanze mdogo mdogo kwanza!

Kwanza tuelewe mizunguko (guarding circles) inayomlinda Mh Rais. Tukiachana na mzunguko huo ambao umo ndani ambao hatuuoni, kuna mizunguko mitatu iliyo dhahiri katika video.

Mzunguko wa tatu upo huo wa polisi pamoja na wanausalama waliovalia kaunda suti. Unaona kabisa Trafki anaupita na kujitokeza kuukabili mzunguko unaofuata. Hao walijisahau kabisa.

Mzunguko wa pili ni huo wa Wanajeshi walioshikilia mitutu mikubwa mikubwa.
Ukiangalia kwa umakini, kuna mwanajeshi mmoja anamnong'oneza afisa (katika mzunguko wa tatu) kitu. Kumnong'oneza huko kukamfanya kupoteza focus ya kuangalia kwa umakini

Isingelikuwa huyo mwenzake kumuwahi huyo Trafiki na kumuamuru asipite huko bila shaka angelipita karibu kabisa na circle ya kwanza.

Mzunguko wa tatu, unahusisha wanausalama wengine pamoja na huyo mnayemwita Mpambe. Baada ya kuamuriwa kwa kusukumwa trafiki analazimika kupita katikati ya mzunguko wa pili na wa tatu.

Trafiki alifikaje?
Kwanza ametumia advantage ya yeye kuwa sehemu ya usalama. Amevalia kitrafiki.
Akapata upenyo kusogea ndani zaidi.

Lakini tukubali kuwa kuna uzembe ulifanyika wa kumpuuzia.

Hata baada ya kusukumwa anaondoka kwenda kumuagamia mwanausalama kiunoni. Sijui ni makusidi ama kukosa balance.

Huenda ni makusudi kwa kuwa hakusukumwa kwa nguvu sana. Ni kidogo tu. Lakini pia, askari anatakiwa awe mkakamavu, force kidogo kama ile si ya kukuyumbisha kutaka kuanguka.


Huenda si makusidi kwa sababu:
Uoga ulichangia kukosa balance. Nafasi baina ya aliyesukuma na aliyetaka kumuangukia haikuwa ya kutosha.

Je, ni threat?
Hapana, kwa sababu hakusababisha usumbufu wa aina yeyote. Alishindwa kuelewa mipaka yake, mahali anapotakiwa kuishia.

Ila uzembe umefanyika kwa kikosi kushindwa kumzuia kutofika huko.
Hata huyo kama mwanajeshi aliyekuwa anamnong`oneza Afisa wa suti nyeusi naye alimzuia. In such siyo mwanajeshi bali ni kikosi cha Tiss wenye majukumu kama hayo wanayofanya. Lakini hoja inabaki palepale kuwa kwa wao huyo Traffic ni mgeni na angeweza kuwa mtu yeyote au adui aliyejipenyeza na kusababisha harm (Let say Bomu la kudetonate manually/suicide bombing) . Walikosea kumuignore, alitakiwa azuiwe na kuhojiwa kwana.

WanaJF pia nahisi kama Tunamsagia Kunguni, maana Muslim ana sifa sana akiona hii anaweza kumuita
 
Nimeona mkuu, Hii ni Ignorance sababu mwisho wa siku wote ni wanausalama. Hakuna atakachofanywa. Jiulize angekuwa ni Raia wa kawaida kama Bwana Petro ingekuwaje.

Hii concept ya kuamini zaid wanausalama ndo inatumika sana kwenye assasinations attempts za viongozi wengi. Mfano Laurent Kabila, Abeid Karume, n.k .

Timu ya Ulinzi wa Kiongozi tu ndo inapaswa kuwa na jukumu hilo.Tena body contact inawahusu wachache zaid kutokana na perimeter wanazopewa. Wengine wanakuwa treated kama civilians tu
Umeongea vizuri sana, kunywa bia kiongozi.
 
Back
Top Bottom