Huzuni Nyingine Yaikumba Arusha: Ajali Yachukua Roho Za Watu 15 Jioni Hii

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Watu 15 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari kubwa aina ya Scania kufeli breki na kwenda kuparamia magari mengine katika eneo la Kibaoni Ngaramtoni Wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Ombeni Kirusha ambaye ni Shuhuda wa tukio hilo amesema “Kilichotokea ni ajali, nilikuwa na gari ndogo nikapisha gari iliyobeba cartepilar likaparamia magari hayo kulikuwa na magari matatu moja limebeba Wazungu, nakusababisha vifo vya Watu wengi, tumeokoa waliokuwa wanahema Watu nane, nilioshuhudia wamefariki walikuwa zaidi ya kumi”

Jeshi la polisi Mkoani Arusha kupitia kwa RPC Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema Watu 15 wamefariki.

Chanzo: Millard Ayo
 
Nani aliruhusu Malori Kupitia katikati ya Mji wakati Kuna Bypass?

Poleni sana wafiwa na mpumzike Kwa amani marehemu wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…