Ab-Titchaz,
..kufukuza wakimbizi ni kuvunja sheria za kimataifa zinazowalinda wakimbizi.
..hata Tanzania tuliwahi kuingia ktk "mgogoro baridi" na UN/UNHCR baada ya Raisi Mkapa kuwa-repatriate wakimbizi kutoka Rwanda.
..pia kama utakumbuka, wakati Tanzania ilipofukuza illegal immigrants hivi karibuni, SG wa EAC ambaye anatoka Rwanda, akishirikiana na maofisa habari wa EAC wanaotoka Kenya, walianza kuishambulia Tanzania kutokana na uamuzi huo. hata vyombo vya habari vya Kenya navyo vilijiunga in their assault against Tanzania.
..hoja ya SG wa EAC na genge lake ndani ya EAC, and within Kenyan and Rwandan media, ilikuwa ni kwamba Tanzania inafanya kinyume na spirit ya integration ktk eneo letu la East Africa.
..hoja zilezile ambazo walikuwa wanajenga dhidi ya Tanzania, na sisi tunazitumia ku-question uamuzi wa Kenya kuwarudisha wakimbizi wa Kisomali.
..kuna UHUNI mwingi sana unafanywa na majirani zetu. kwa mfano suala la work permits hata Kenya wameondoa fees mwezi uliopita, lakini Dr.Sezibera[EAC SG] amekuwa akitumia vyombo vya habari vya Kenya na Rwanda kuishutumu Tanzania kuhusu suala hilo, huku akiwa bubu kuilaumu Kenya.