I want to die a judge

I want to die a judge

STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI

TULIPO ISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TISA........
Hofu ya kifo aliigopa vyema tangu siku ile alikuwa akiwasikitikia sana watu ambao walikuwa wakikichukulia poa kifo ni jambo la hatari sana, kifo huwa kinatajwa kiwepesi mno ila pale kinapo mtia mtu mbavuni huwa anakuja kuelewa umuhimu wa kila pumzi ambayo anaivuta hapa duniani ila kwa bahati mbaya sana watu huwa wanakuja kujua ikiwa muda ushaenda na hawawezi kubadilisha chochote tena kwenye maisha yako hivyo kufa inakuwa ni chaguo la pekee kwa sababu kunakuwa hakuna namna tena ya kuweza kufanya kitu chochote kile, usiku ulikuwa umeanza kuingia alikuja kushtuka kwenye hayo mawazo wakati huo askari wake wote walikuwa wameshaondoka alibeba kila kilicho chake humo ndani na kuondoka kwa spidi.

ENDELEA................................
Tamaa ni miongoni mwa janga linalo itishia sana dunia hata vitabu vitakatifu vimelielezea sana hilo jambo kwenye kuzichambua zile amri kuu kumi za MUNGU, watu ambao ni wagumu sana hasa wale magaidi wa kutisha duniani huwa wanakamatwa kwa kupitia tamaa zao kwa vishawishi vya kuwaridhisha kwenye macho yao, ukikumbwa na pepo la tamaa kupitiliza basi utajikuta wewe unakuwa ni binadamu wa hovyo sana au mtu hatari zaidi kuishi kwenye ulimwengu kwa sababu kila kitu utatamani sana kiwe upande wako hiyo inaweza kusababisha hatari kubwa sana kwa watu wengine. Tanzania ni moja ya nchi ambayo tamaa imechukua nafasi kubwa sana hususani kwa vijana ambao wanaishia kwenye mambo mabaya sana hususani kwenye jiji kubwa kama Dar es salaam lakini hiyo hiyo tamaa kama ukiitumia vizuri itakufanya ufike sehemu nzuri sana ya maisha kama wewe una ndoto kubwa kwa baadaye.

Macho huwa hayafundishwi nini cha kukitazama wala ni kitu gani sahihi cha kukiona mbele, kitu chochote ambacho kinawezekana kuonwa na macho ya binadamu wa kawaida basi lazima tu kionekane, ndani ya uwanja wa ndege mkubwa zaidi nchini JNIA kila ambaye siku hiyo alikuwa ametembelea hilo eneo alibaki ameduwaa sana, kwa wenye waume walishikwa na hasira sana kwa sababu hakuna mtu ambaye aliwazingatia kwa muda huo hawakuwa na thamani kwa muda mfupi tu hata wafanya kazi wengi walikuwa wamejishika viuno na baadhi ya abiria waliduwaa na hawakuamini kile ambacho walikuwa wanakiona mbele yao.

Kwenye ndege kubwa ambayo ilikuwa inatua majira ya usiku wa manane sana alikuwa anashuka mwanamke mmoja mrembo sana ambaye hata ukitumia kalamu kumuelezea wino utakuishia ukiwa bado unatamani kalamu yako iendelee kuusifia uumbaji uliofanyika kwenye mwili wake. Rangi yake, umbo lake, mwendo wake, mikogo yake kwa tamaa za vijana wa Tanzania basi wengine hata siku ile ile walikuwa tayari kumuoa hata bila kumjua kiundani zaidi mwanamke huyo ni nani hasa.

Airport nzima watu wote walibaki wameduwaa kubahatika kwenye kuishi kwao kukutana na mrembo kama huyo watu walikuwa wakimpiga picha wengine wakitamani kama wangejua basi walitakiwa kuitisha hata waandishi wa habari mapema waonekane wakipiga picha na mrembo kama huyo, abiria waliokuwa wamepanda kwenye ndege na walianza naye safari hawakumuona kwa sababu alijifunika koti kubwa na kofia kichwani mwake kwahiyo wakati anatoka hivyo vitu aliviacha humo humo kwenye ndege akatoka kama alivyo usoni, uso ulipambwa ukapambika, miwani yake ya bei kali iliwaacha midomo wazi.

“Oya Athumani kuna watu wanafaidi sana brother hivi inamaanisha kuna mjinga ambaye anammiliki huyu mwanamke?” kijana mmoja aliuliza akiwa anamuegemia rafiki yake kwenye bega lake, alikuwa amekuja hapo kumpokea rafiki yake ambaye alitoka kwenye likizo huko Malaysia, ni watoto ambao walizaliwa kwenye maisha safi sana hivyo kwao starehe na wanawake ndiyo ilikuwa sehemu kubwa ya maisha yao.

“Huyu mwanamke lazima nilale naye ikiwezekana awe wakwangu siwezi kumuacha bora nife” kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Athumani alimjibu rafiki yake wakati huo alikuwa anajiandaa kupanda kwenye gari lakini aligairi hata miwani yake aliivua na kuilamba

“Sio rahisi hivyo mtu wangu mwanamke mwenyewe anaonekana wazi sio mnyonge yule huwezi kwenda na sera zako ambazo huwa unawapata watoto wa tabata kwa sababu ya pesa zako sio kila mwanamke ana tamaa za hovyo za hivyo” rafiki yake ni kama alikuwa anamkejeli

“Sasa subiri nikuonyeshe ili ujue kama huu mji upo kwenye mkono wangu” alijigamba sana basi rafiki yake akashikilia gari ili amshuhudie mwenzie huyo aweze kumchukua mrembo huyo ambaye alileta gumzo hapo airport. Mwanamke huyo alikuwa anaelekea kutoka nje ya lakini kwa bahati mbaya kuna mhudumu mmoja ambaye alikuwa ameduwaa sana akimtazama mwanamke huyo alijigonga chini na kummwagia glasi ya maji, alishtuka na kuanza kumuomba msamaha kwa sababu lilikuwa ni kosa kubwa sana kufanya hicho kitu kwa mteja cha ajabu mwanamke huyo alimkabidhi mkoba wake na kumpa ishara ya kusubiri hapo kisha akawa anaelekea eneo la bafuni ili akajisafishe, tamaa huwa zinamponza fisi muda mwingine kutaka kula kila anacho kiona mbele yake Athumani hakuvunga mtoto wa Tabata alienda huko huko eneo la bafuni ili akaonyeshe umwamba wake huko huko bila kuwa na wasi wasi wowote ule.

Hesabu zake zilikuwa zikimuelekeza kwenye ule mlango ambao aliona mwanamke huyo ameweza kuingia, kwake alihisi pesa ni kila kitu kwenye maisha kwa kuwa nazo alihisi amemaliza kila kitu hapa duniani, alitaka kugonga mlango huo lakini alihisi kama vile upo wazi basi akausukuma haukugoma ukaitikia vizuri kwa kufunguka, alijiramba midomo yake baada ya kuona mwanamke huyo ameinama na sehemu yake ya nyuma imetuma vilivyo tamaa zilikuwa zinampelekesha kijana wa watu kwa watu ambao hakuwa akiwajua kabisa kwenye maisha yake. Alisogea mbele na kumparamia mwanamke huyo kisha akamsogeza ukutani kwa nguvu sana akitaka kumyonya mdomo wake.

“Una miaka mingapi kijana” ilikuwa ni sauti ya kirembo sana kutoka kwa mrembo huyo akimuuliza Athumani huku akiwa anaibinua midomo yake kwa mbwembwe sana( lugha ya kiingereza ilitawala).

“Hilo sio mhimu mrembo mimi nitakupatia kila kitu kwenye maisha yako unaweza kuishi kama malikia kama tu utakubaliana namimi”

“Unaweza kunipa kila kitu kweli?”

“Ndiyo chochote kile”
“Unaweza kunipa roho yako?”

“Huo utani sa….” sentensi yake iliishia na kilio kuna ngumi nzito ilipita kwenye shingo yake alihisi kuna mtu kampiga nyuma hakuwa na wazo kabisa kwamba anaweza kuwa ni huyo mwanamke kwa uzuri aliokuwa nao machoni pake, alinyoosha mkono wake kuna sindano ndogo alizizamisha kwenye shingo ya Athumani kwa nguvu kijana huyo alibaki tu anamwangalia mrembo huyo uchu wake ulikuwa unayagharimu kabisa maisha yake.

“Ningekuua sema itanipa wakati mgumu sana kutoka hapa ndani, jiangalie sana wewe bado ni mdogo sana kuparamia watu usio wajua utakufa ukiwa bado hujafikia hata nusu ya maisha ya ndoto zako. Utakuwa sawa baada ya siku tatu ndipo koo lako litakuwa na uwezo wa kutoa sauti” maelezo hayo yalimfanya Athumani atoe machozi alijuta sana kuja hapo alikuwa amechomwa sindano ambayo ilimkausha kabisa koo lake hakuwa na uwezo wa kuongea alibaki anajinyonga kwa maumivu makali sana ya tumbo hapo chini ambapo alikuwa amekaa. Mwanamke huyo alitoka nje akachukua mkoba wake kwa yule mfanyakazi na kumpiga busu shavuni ambalo lilifanya mpaka mwanaume yule akadondoka chini hakuamini kuweza kupewa zawadi ya busu na mwanamke mrembo kama huyo.

Catherine Yudel ndiye mwanamke ambaye alikuwa ameingia kwenye nchi ya Tanzania, usijisahaulishe ni komando mkubwa sana ndani ya nchi ya Cuba, penzi lilimtoa kilomita nyingi sana mpaka kumleta kwenye ardhi ya wapenda amani je kuna kitu chenye nguvu kuyazidi mapenzi duniani? Utasema ni pesa? Hapana mapenzi hayalinganishwi na kitu chochote kile wala hayawezi kununulika kwa pesa ila ngono ndiyo inayo nunulika kwa pesa. Ukiifuatilia kwa undani historia ya mapenzi utayaelewa kwamba huwa hayaelezeki kwa kutumia uzoefu au uelewa wa kawaida bali ni chembechembe zilizopo ndani ya moyo wa mwanadamu ndizo zinaweza kuelezea hisia za mapenzi, mapenzi ni siri ya mtu mmoja pekee na moyo wake ndiyo sababu wengi huwa wanawaona watu wanao penda sana kama hawana akili za kutosha pale wanapofanya maamuzi ya hovyo bila kujua ni kitu gani watu hao wanapitia, mapenzi yanaweza kukufanya ukayaacha maisha yako halisia ukaenda kuyaishi maisha mengine kabisa kwenye maisha yako, mapenzi ndicho kitu chenye nguvu zaidi duniani kushinda hata pesa ndio maana mapenzi ya kweli huwezi kuyapata kwa kutumia kipato ulicho nacho kwenye mfuko wako.

Wataalamu wa masuala ya mapenzi wameyaelezea kwa upana sana lakini hakuna hata mmoja ambaye aliweza kutoa hitimisho la mwisho kwamba mapenzi ni nini kwa sababu moyo wa mtu ndio huwa anaweza kuelezea namna penzi lake lilivyo, mapenzi ni upofu, mapenzi ni hadithi ya kufikirika, mapenzi ni mchezo wa kupata na kukosa ila mapenzi ni ugonjwa ambao huwezi kuutibu kwa kauli yako mdomoni au kwa kuyashuhudia kwa mtu, mapenzi huponywa na upendo pekee wa sehemu ambayo moyo umependa. Jamal ndilo lilikuwa tulizo la mrembo huyu asingeweza kabisa kupata usingizi ingali mwanaume wa ndoto zake alikuwa akiteseka mahali ambapo ilihitajika kuishi maisha yake yote mpaka anakuja kufa bila kuweza kumuona mwanaume huyo ambaye kwake alikuwa ni mtu wa mhimu zaidi kwenye dunia na ulimwengu wake wa mapenzi na ukizingatia ndiye aliyekuwa mwanaume wake wa kwanza kumpenda, hakuja Tanzania kuuza sura alikuja kwenye nchi hii ili kuweza kumsaidia mpenzi wake hiyo ndiyo nguvu ya mapenzi kama ulikuwa huijui.


*****************
Asubuhi sana wakati ndo kunaanza kupambazuka tu Mapande Dickson alikuwa anaamka akiwa mchovu sana tabia yake ya ulevi na kupenda sana wanawake ilikuwa imemkaa sana akilini hivyo baada ya kutoka kazini alikuwa amepitia kwenye club ambayo ndiyo ilikuwa sehemu yake pendwa kabisa ya kufanyia starehe, njaa ilikuwa inamuuma sana baada ya kushtuka asubuhi hiyo akiwa bado mchovu sana safari yake ilikuwa ni kuelekea kwenye friji ambalo lilikuwa lipo sebuleni ili akapate chakula chochote kile walau kuweza kutibu ugonjwa ambao ndio huwa unawafanya wanadamu wengi sana wanabadilisha mifumo ya maisha yako, njaa isikie kwa jirani au kwenye simulizi za watu, njaa itakukumbusha namna chakula kinavyo patikana, njaa itakupa somo la kuyaishi maisha yoyote yale hata kama yatakuwa ni ya hatari sana ila mwanaharamu tumbo hajawahi kuridhika ndiyo sababu kila siku watu huwa wanafanya kazi kwa bidi sana ili wapate chochote cha kukiweka walau wapate ahueni ambayo huwa inafanya watu kuwa na kiburi na maringo makubwa sana kwenye maisha yao kwa sababu njaa huwa inalegezwa baada ya shibe kuwalevya.

Baada ya kuusukuma mlango huo ambao ulikuwa umenyoosha njia ya kwenda chumbani alikuwa kwenye ndoto nzuri sana ambayo hakutakiwa kumaliza kuiota mapema huenda angekijutia sana kiherehere chake cha kuwahi kuamka mapema, ni ndoto ambayo ilihitaji maneno mazuri sana kuweza kuielezea kwa usahihi na ufasaha wa kuzitumia vyema tamasali za semi kuweza kuyachakata, malaika wa haja alikuwa amekaa mbele yake, ni vitu vilivyo ikonga sana nafsi yake kwenye maisha yake na ndiyo sababu alikuwa akimshukuru sana MUNGU kwa kumpendelea nafasi ya kuendelea kuishi kwenye uso wa dunia hii ya leo. Aligeuka akatikisa kichwa chake kwa nguvu na ndipo alipogundua kwamba hakuwa kwenye ndoto kabisa kitu alichokuwa akikiona hapo kilikuwa ni cha kweli kabisa, mwanamke mmoja mrembo sana alikuwa amekaa kwenye sofa yake ya kifahari sana akiwa amevaa suruali na koti dogo lililomkaa vyema ukijumlisha na kiatu chake mfano wa buti lakini kilikuwa cha kisasa sana vilimfanya ayasifie sana macho yake kuweza kuona vitu vizuri vinavyokuwa mbele yake. Mwanamke huyo alikuwa amewasha televisheni kama vile yupo kwake hakuwa na wasiwasi wowote kama amevamia nyumba ya watu bila idhini ya mhusika, miguu yake alikuwa ameikunja akiwa amepiga zake nne nzuri sana.

“Nashangaa sana mtu mkubwa kama wewe unaishi kisela sana namna hii na ni hatari sana kuishi bila mlinzi hata mmoja hapo nje mtu anaweza akafanya chochote ambacho anajisikia na akaondoka bila hata wewe mwenyewe kuwa na taarifa ni aibu sana nchi kuwa na watu kama wewe kwenye ishu nyeti za usalama wa nchi kubwa na nzuri kama hii” Catherine ndiye aliyekuwa amekaa hapo, alikuwa akiongea hayo maneno kijasiri sana huku akipunguza sauti ya redio ambayo ilikuwa imeunganishwa hapo, Mapande alielekea kwenye friji lake na kutoa vinywaji viwili ambapo kimoja alimrushia huyo mrembo.

Mtoto wa kike kaamua kijiingiza kwenye biashara ya wanaume, ataiweza kweli? Nakudokeza tu hakuna chochote ambacho unakijua kuhusu huyu bibie, kuna sababu ya msingi sana mpaka anaamua kuingia kwenye kesi nzito kama hii, nikopeshe akili yako nizidi kukupa madini.....50 inatia nanga hapa[emoji3578]

Bux the story teller
Kwa shilingi 3000 tu unaipata hadithi hii mpaka mwisho kabisa sehemu ya 100

Lipia kupitia namba
0621567672
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

Lakini kwa wale ambao wanahitaji kujiunga na group langu la WhatsApp ni shilingi 3000 tu kwa mwezi, namba za malipo ni hizo hizo[emoji2768].

Muda ni wako sasa

Wasalaam

Bux the story teller
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA

TULIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI.......

“Nashangaa sana mtu mkubwa kama wewe unaishi kisela sana namna hii na ni hatari sana kuishi bila mlinzi hata mmoja hapo nje mtu anaweza akafanya chochote ambacho anajisikia na akaondoka bila hata wewe mwenyewe kuwa na taarifa ni aibu sana nchi kuwa na watu kama wewe kwenye ishu nyeti za usalama wa nchi kubwa na nzuri kama hii” Catherine ndiye aliyekuwa amekaa hapo, alikuwa akiongea hayo maneno kijasiri sana huku akipunguza sauti ya redio ambayo ilikuwa imeunganishwa hapo, Mapande alielekea kwenye friji lake na kutoa vinywaji viwili ambapo kimoja alimrushia huyo mrembo.

ENDELEA..........................

“Mhhhh sio kirahisi sana namna hiyo bibie usijihalalishie kwamba hii nyumba unaweza ukaingia unavyotaka mwenyewe ila nimeamua tu kuwatoa walinzi ambao walikuwa wamejazana tu hapo nje sikuelewa hata kazi yao kubwa ilikuwa ni ipi” alijibu huku akiwa anakaa kwenye kiti cha ng’ambo yake.

“Ni sababu ipi imekufanya uwafukuze kazi watu ambao walikuwa wanayalinda maisha yako na wanahakikisha usalama wako?” Dickson hakujibu hilo swali bali alisimama na kwenda kuchomeka frash ndogo kwenye hiyo televisheni yake, dakika kama tatu ilianza kuonekana sura ya mtu ambaye ilimfanya Catherine atabasamu sana, walikuwa wakipiga stori unaweza ukadhani wanafahamiana muda mrefu sana ila kiuhalisia ilikuwa ni mara yao ya kwanza kuonana kwenye maisha yao, watu hatari huwa ni rahisi sana kufanya maongezi ya aina yoyote yale pale wanapokutana ila pia hata kubadilika kwao huwa ni sekunde tu wanakuwa viumbe tofauti kabisa, video hiyo ilileta ukimya mkubwa sana ambayo ilichukua takribani nusu saa nzima wakiwa wanaiangalia kwa usahihi sana kisha Dickson akaitoa frash hiyo na kuirudisha kwenye mfuko wake wa suruali alionekana wazi kabisa alikuwa akitembea nayo kila mahali anapokuwa.

“Hii ndiyo siku ambayo sikuona umuhimu wa kuwa na watu ambao wananilinda kwenye maisha yangu, ilikuwa siku ya kwanza kabisa mimi kuelewa nini maana ya hofu ya kifo. Wanadamu tumeumbwa na mioyo ya kawaida sana ila huwa tunajivika usimba ndani yetu kwa kuhisi tuna mioyo migumu kitu ambacho sio cha kweli kabisa, kifo kinatisha sana hasa pale unapo ona unaenda kufa na hauna msaada wowote ule. Huyo kijana unaye muona kwenye hiyo video ni bwana mdogo sana ila kupitia yeye nilipata somo kubwa sana kwenye haya maisha ndiyo sababu umeona hii video natembea nayo kila mahali, nikihitaji kufanya jambo la hovyo naiangalia sana hii frash inanikumbusha maisha ni zawadi kubwa sana ambayo tumepewa na MUNGU na ndicho kitu cha thamani zaidi kwenye maisha ya mwanadamu yeyote yule, kabla ya kukutana naye nilikuwa mtu mbishi sana ambaye kwanza sikuwahi kufikiria kuna mtu anaweza akanitishia mimi kwenye mapigano ila nilijilaumu sana kuaminishwa hicho kitu, mguu wangu unauma sana mpaka sasa nachoma sindano nyingi za ganzi pamoja na mkono kwa maumivu makali ambayo niliyapata kutoka kwa huyo bwana mdogo.

Ni kijana mdogo sana ila sitamani kukutana naye kwenye maisha yangu yote, ana nguvu za ajabu sana yaani kiufupi ni mtu hatari mno ambaye hahitaji hata sekunde kumi kukudondosha kwake kila sekunde moja inavyo hesabu ni ya mhimu sana na inaenda na hesabu zake kali mno, tukio lake la yeye kuja kituoni na kumchukua yule kijana lilinitisha zaidi lakini kuniacha hai kwa kupiga risasi kadhaa pembeni ya sehemu zangu za siri ni kitu ambacho kimenifanya nimuombee sana aishi maisha marefu popote alipo ila kwa bahati mbaya sana ni mtu ambaye amedhulumiwa maisha ya familia yake na wanao husika ni vigogo wakubwa mno kutoka serikalini hivyo ana nafasi ndogo sana ya kuishi na ndiyo sababu amepelekwa jela kwa kutengenezewa kesi isiyo mhusu lile tukio la mahakamani nimejikuta namuonea sana huruma”Maneno ya Dickson alionekana wazi kwamba ni mtu ambaye ujio wa Jamal ulimpa funzo kubwa sana kwenye maisha yake, Catherine alitabasamu sana mwanaume aliyekuwa anamuona kwenye hiyo video ndiye ambaye alikuwa amekuja kwa ajili yake kwenye nchi hii.

“Kwanini umeniambia haya yote na asubuhi yote hii, kuna umuhimu gani wa wewe kuniambia haya mambo?” lugha ambayo ilitumika kwa mwanadada huyu kilikuwa ni kiingereza tu kiswahili hakukijua kabisa mwanamke huyu ila lilikuwa ni tatizo dogo sana kwa mtu kama Dickson.

“Unajua hii dunia ili uishi vizuri unatakiwa sana ujitahidi kwenda na kasi ya walimwengu jinsi walivyo vinginevyo utakuwa mtu ambaye utaachwa nyuma sana kwenye maisha ya zamani wakati wenzako wanayaishi maisha ya sasa, najua kuja kwako hapa sio bure lazima kuna kitu unakitafuta sio kawaida kwa mwanamke mrembo kama wewe ukaingia namna hii kwenye nyumba ya mtu bila wasiwasi bila kuwa na sababu ya msingi” Dickson baada ya kumaliza kuongea aliitoa simu yake ambapo alobonyeza tarakimu kadhaa kuna video ilitokea kwenye skrini yake aliiruhusu na kumgeuzia Catherine ambaye alisikitika tu kwani alijiona akiwa anaruka geti kwa spidi ya ajabu kama upepo lakini kulikuwa kuna kamera za siri kila sehemu hivyo kumbe ujio wa Dickson hapo sebuleni haukuwa wa bahati mbaya kama ilivyo onekana bali alijua wazi kwamba kuna mtu alikuwa anamsubiri asubuhi hiyo na mapema.

“Nilijua kwamba upo hapa sebuleni ndio maana niliamka na kuja
, sitaki mambo ya kuanza kumwagana damu siku hizi ukizingatia mwili wangu bado haujapona usije ukanimalizia bure mwanangu na mke wangu wananitegemea mno kwenye kila kitu haya niulize unachotaka kujua kwangu kisha uniache nikalale bado nina usingizi wa kuumalizia nimechelewa sana kulala” maelezo ya Dickson yalichanua tabasabu kwenye sura angavu ya mrembo huyo na kuufanya uzuri wake uweze kuonekana hadharani kabisa na kudhihirisha namna alivyokuwa amependelewa na MUNGU kuwa mrembo huku vishimo vidogo vikibonyea kwenye mashavu yake na kumfanya Dickson ameze mate kwa shida ila hakuwa na la kufanya kwa aina ya uingiaji wa mwanamke huyo alimuogopa alijua wazi huyo hakuwa mrembo kama macho yanavyoweza kukudanganya bali ndani yake kulikuwa na nafsi yenye roho ngumu sana ambayo kama ungejaribu kucheza nayo hovyo basi unaweza ukajikuta una maisha mafupi mno, aliwajua sana watu wa aina hiyo mara nyingi walikuwa wakitumiwa sana na usalama wa taifa ili kuwakamata wahalifu japo alijua huyu siyo mtanzania ndio maana aliamua kufupisha maelekezo ili waweze kuyamaliza kwa amani tu hakuhitaji tena kuvunjwa kiungo chochote kwenye mwili wake.

“Nimekujua baada ya kufuatilia kwa umakini kwa mara ya kwanza mtu huyo ambaye umemuonyesha kwenye video alipo onekana hadharani nilijua hapo lazima ndipo tatizo lilipo anzia kuwa kubwa, nimekuja kugundua kwamba palikuwa ni kituo cha polisi ndipo alipo jionyesha hadharani ikanilazimu nikifuatilie kituo hicho ili nikijue vizuri, nilibahatika kumkamata askari mmoja wa kwenye kile kituo, ana bahati sana ubishi wake ulitaka nimpotezee sifa ya yeye kuitwa mwanaume kwenye ulimwengu huu, huyu ndiye aliyenipa maelekezo yote ya juu ya kukamatwa kwa mtu ambaye ndiye Jamal aliye mfuata hapo ambaye bila shaka alikuwa kwenye mkono wako, hii ndiyo sababu kubwa ambayo imenifanya mimi nikutafute wewe kabla ya mtu yeyote yule kwa sababu unaonekana una taarifa za mhimu sana kuhusu hili jambo. Kuhusu wewe kunipa taarifa hizo sio kwamba nakuomba hapana ila wewe ndiye mwenye uamuzi kama unipatie kwa amani niweze kuondoka au nizichukue kwa lazima” sasa Dickson alijithibitishia mawazo yake alikuwa amekaa mbele ya mwanamke hatari sana ambaye huenda urembo wake ulikuwa ukiwahadaa watu wengi sana sio rahisi mwanamke wa kawaida kumpa mwanaume kama yeye machaguo kama hayo. Maamuzi yalikuwa yapo kwenye mkono wake kuamua kuzitoa kwa amani tu kisha waachane au alazimishwe ikimaanisha watumie njia ya kuweza kumwagana damu na kupunguzana viungo ambayo Dickson hakuwa tayari kabisa kuona inatokea hakuhitaji tena hayo mambo.

“Jioni moja nikiwa natoka kazini kwenye simu yangu nilishangaa naiona meseji ya pesa, nilidhani labda ni mshahara lakini nilivyopiga hesabu zangu hazikuwa tarehe za kuweza kupokea kabisa mshahara, nilitamani kupiga simu ila kwa bahati mbaya sana mtu aliyekuwa emenitumia pesa hizo alikuwa ametumia kadi ya benki hivyo sikuelewa ni nani. kilikuwa ni kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho hata mshahara wangu wa miaka kumi usingeweza kufikia zile pesa, sikuwa nikiyaamini macho yangu wakati nazihesabu zile tarakimu ambazo zilinifanya moyoni nijione mimi ni mwanadamu mwenye bahati sana kwenye maisha yangu basi ni siku ambayo nililala kwa furaha sana. Asubuhi yake wakati naamka simu yangu ilikuwa ikiita namba ilikuwa ni ngeni kabisa niliambiwa maneno machache sana na mtu huyo ambaye alikiri kwamba yeye ndiye aliyeweza kutuma hizo pesa, kuna mwanaume mmoja ambaye mtu huyo alikuwa anahitaji kumpata kama sio kuzipata taarifa za kifo chake pamoja na mtu mwingine ambaye alionekana kuwa lengo kuu zaidi na ndiye huyo ambaye unamwona kwenye hiyo video huyo ndiye anaye tafutwa sana na hao watu.

Sikupewa taarifa za ndani sana za mtu huyo kuhitajika ila niliambiwa niende External kuna kijana nikutane naye anaitwa the spy huyo ndiye atakayeweza kunipatia majukumu ya kufanya, kweli niliweza kwenda pale nikakutana na kijana huyo ambaye alinipa picha za kijana ambaye nilitakiwa kumkamata ili aweze kunipatia taarifa juu ya watu hao. Nilimfuatilia kwa muda mrefu mpaka nikaja kugundua kwamba anaishi mitaa ya Kibangu huko na ndipo nilipowatumia vijana wangu kuweza kumpata mpaka nikamkamata kirahisi sana ila bahati mbaya mno nikiwa bado namhoji ndipo huyo mhusika mwenyewe alipofika pale na kumchukua mtu huyo kibabe na kuondoka naye, sikuweza kumzuia kwani nilipigwa vibaya sana ila baadae niliogopa sana baada ya kujua kwamba alikuwa ni komando mkubwa mno na aliahidi kunirudia nadhani ndiyo sababu iliyo mfanya mpaka akaja hapa kwangu” alicho takiwa kukifanya alikitekeleza kwa asilimia zote mr Dickson aliiheshimu sana thamani ya uhai kwenye maisha yake kwa wakati huu hakuhitaji kuingia kwenye mtafaruko na mtu yeyote yule ndiyo sababu alikubali kuyatoa maelezo kuhusu kile ambacho yeye binafsi alikuwa anakijua.

“Mhhhhhhh kivipi kirahisi sana namna hiyo kumkamata tu mtu ndo upewe pesa zote hizo ambazo umesema hata ingepita miaka kumi usingeweza kuzipata? Hakuna mwanadamu ambaye yupo tayari kuweza kupoteza pesa zake kirahisi sana namna hiyo kwenye ulimwengu wa sasa jua lazima kuna vitu ambavyo anategemea kuvipata baadae” Catherine alionekana kabisa kutoridhika na hicho kitu moyo wake ulikuwa mzito sana haiwezekani kazi ndogo kama hiyo mtu alipwe pesa nyingi sana namna hiyo kwani kama ni kumkamata mhalifu lilikuwa ni jukumu lake tayari haikuwa na haja ya mtu kuweza kumlipa tena.

“Hilo swali nilijiuliza sana ila sikupata nafasi ya kuweza kupata jibu lake niliona nitajiumiza sana kichwa changu bure nikaamua kuachana nalo kabisa kwa sababu lilikuwa halinihusu sana ila inaonekana huyu bwana mdogo ana kitu kikubwa sana ambacho anakimili kinatafutwa sana na hawa watu, na inaonekana wana historia ndefu sana ya kuweza kupata mtu ambaye alikuwa ameiteketeza familia yake pamoja na kuondoka na kichwa cha baba yake alisema anakitafuta sana” hizi stori zilikuwa ni mpya sana kwenye kichwa cha Catherine kwa sababu muda ambao alikutana na Jamal kule Cuba mwanaume alikuwa ameshapoteza kumbukumbu zake hakuwa akijijua yeye ni nani asili yake ni wapi hivyo taarifa hizi Catherine hakuwahi kuzipata kabisa leo ndo alikuwa anazisikia.

“Ni kwa kiasi gani unazijua hizi habari?”

“Sina taarifa zake nyingi sana hata hizo ni yeye aliniambia inaonekana kuna jambo kubwa sana ambalo lina historia iliyo jaa kisasi baina ya hawa watu hivyo ni lazima watamtafuta popote pale alipo kwa gharama yoyote ile”

“Unajua gereza alilofungwa liko wapi na linaitwaje?”

“Hizi nchi zina siri kubwa sana, kuna baadhi ya mambo huwa wanayajua watu wachache sana, kwa makosa aliyo yafanya yule mtu ni kazi ngumu sana kuweza kujua atafungwa wapi kwa sababu kwanza hawezi kuchangamana na wafungwa wa kawaida lazima atafungwa sehemu ambayo kuna watu wengine kama yeye na kwa bahati mbaya sana jela za hivyo huwa zinakuwa hazionekani kwenye macho ya kawaida ni watu wachache sana huwa wanaziona mpaka sasa uhakika wa kujua yuko wapi una asilimia tano tu basi hizo 95 hauwezi hata ufanye nini na huenda akauawa” maelezo ya Dickson yalimkatisha tamaa sana Catherine japokuwa hakulionyesha wazi wazi ila moyo wake ulikuwa uliungua sana kwa maumivu makali kumpoteza kizembe mwanaume wake huyo.

Sijui huyu bibie anatafuta nini kwa wanadamu ambao hawazoeleki kabisa ila 52 itatupa majibu, 51 niseme bye-bye.

Bux the story teller.
Habari, ni matumaini yangu mpo wazima wa afya kabisa.

Leo ni siku nyingine njooni msome hadithi huku mkiburudika na ofa ambazo hazielezeki kirahisi.

1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA kipande kimoja ni shilingi mia tu za kitanzania (100).

2. I WANT TO DIE JUDGE...kipande kimoja shilingi mia tu za kitanzania, lakini pia leo GEREZA LA HAZWA Leo natoa ofa ya Pekee.

3. GEREZA LA HAZWA.....Leo kipande kimoja kinauzwa 100 badala ya 150 hii ni kwa leo tu, ipo mpaka 82 kwa sasa.

Namba za malipo ni zile zile
0621567672
0745982347

Zote jina ni FEBIANI BABUYA, natuma Kote WhatsApp na kwa wale wa simu ndogo natuma messenger Facebook.

Njoo uburudike na kalamu yangu.
 
No hiyo mwisho ni 100 sema niliona kama watu hawaitaki hivi nikaibwaga
Siyo watu hawaitaki tatizo unaiweka mara moja kwa mwezi hata mzuka unapotea ww kama mwandishi unaechepukia inatakiwa uweke mara kwa mara maliza hata riwaya moja humu ikutambulishe usiweke mbele pesa wakati bado hujatambulika vizur ukiisha tambulika utakuwa unaweka kidogo kidogo kama hivo
Ni ushauri tu
 
Siyo watu hawaitaki tatizo unaiweka mara moja kwa mwezi hata mzuka unapotea ww kama mwandishi unaechepukia inatakiwa uweke mara kwa mara maliza hata riwaya moja humu ikutambulishe usiweke mbele pesa wakati bado hujatambulika vizur ukiisha tambulika utakuwa unaweka kidogo kidogo kama hivo
Ni ushauri tu
Hakika. Kuomba muendelezo kila mara Wakati kaileta mwenyewe inachosha.
 
Hakika. Kuomba muendelezo kila mara Wakati kaileta mwenyewe inachosha.
Sana unajua laiti angekuwa mwandishi mkubwa wala hata isingekuwa shida mm binafsi nanunua sana riwaya za wandishi wengi humu akiwemo singanojr sababu tayar wameshajijengea jina ila kwa yeye ambae bado inatakiwa ajenge jina kwanza
 
Siyo watu hawaitaki tatizo unaiweka mara moja kwa mwezi hata mzuka unapotea ww kama mwandishi unaechepukia inatakiwa uweke mara kwa mara maliza hata riwaya moja humu ikutambulishe usiweke mbele pesa wakati bado hujatambulika vizur ukiisha tambulika utakuwa unaweka kidogo kidogo kama hivo
Ni ushauri tu

Siyo watu hawaitaki tatizo unaiweka mara moja kwa mwezi hata mzuka unapotea ww kama mwandishi unaechepukia inatakiwa uweke mara kwa mara maliza hata riwaya moja humu ikutambulishe usiweke mbele pesa wakati bado hujatambulika vizur ukiisha tambulika utakuwa unaweka kidogo kidogo kama hivo
Ni ushauri tu
Hii sio hadithi ya kwanza kuileta humu, kuna hadithi ilisha isha kabisa kurasa zote 76 mpaka final humu humu, unfortunately kuna changamoto ambazo ni ngumu kwa wewe kuziona kupitia hichi nacho kifanya nazo kutana nazo. Shukrani kwa ushauri pia
 
Hii sio hadithi ya kwanza kuileta humu, kuna hadithi ilisha isha kabisa kurasa zote 76 mpaka final humu humu, unfortunately kuna changamoto ambazo ni ngumu kwa wewe kuziona kupitia hichi nacho kifanya nazo kutana nazo. Shukrani kwa ushauri pia
Inaitwaje?
 
Mkuu FEBIANI BABUYA ni kigezo gani unakitumia kujua kwamba watu wahaitaki hii riwaya?
emoji28.png

Mkuu FEBIANI BABUYA ni kigezo gani unakitumia kujua kwamba watu wahaitaki hii riwaya?[emoji28]
Kaka sidhani kama ni salama sana kuweka kila kitu public, waandishi wadogo kuna changamoto nyingi sana tunakumbana nazo huku chini unfortunately msomaji yeye anajali kusoma na kusema tu waandishi wadogo wana tamaa ya pesa, nikiona mtu anaongea hivi huwa nasikitika sana na kuwasikitikia mno wale ambao nao wananitafuta na kuniomba ushauri kuhusu kuandika. Anyway inaendelea kuanzia leo
 
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI

TULIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA.......
“Hizi nchi zina siri kubwa sana, kuna baadhi ya mambo huwa wanayajua watu wachache sana, kwa makosa aliyo yafanya yule mtu ni kazi ngumu sana kuweza kujua atafungwa wapi kwa sababu kwanza hawezi kuchangamana na wafungwa wa kawaida lazima atafungwa sehemu ambayo kuna watu wengine kama yeye na kwa bahati mbaya sana jela za hivyo huwa zinakuwa hazionekani kwenye macho ya kawaida ni watu wachache sana huwa wanaziona mpaka sasa uhakika wa kujua yuko wapi una asilimia tano tu basi hizo 95 hauwezi hata ufanye nini na huenda akauawa” maelezo ya Dickson yalimkatisha tamaa sana Catherine japokuwa hakulionyesha wazi wazi ila moyo wake ulikuwa uliungua sana kwa maumivu makali kumpoteza kizembe mwanaume wake huyo.

ENDELEA...........................

“Naomba maelekezo ya kumpata huyo mtu ambaye umeniambia alikupa maelekezo kwamba yupo External sijui” haikuwa kazi ngumu hata kidogo kupewa picha pamoja na maelekezo ni wapi the spy anapo patikana.

“Kwani huyo kijana ni nani hasa kwako mpaka mwanamke mrembo kama wewe utoke nchi za mbali huko uje kumhangaikia kijana wa kitanzania huyu” Mapande aliuliza kama kejeli tu wakati huo Catherine alikuwa amefika mlangoni alitabasamu

“Huyo mtu ndiye ambaye ana robo tatu ya moyo wangu wote maana yake kama hayupo basi moyo wangu hauwezi kufanya kazi tena” maneno hayo yalimfanya Dickson acheke alielewa mwanamke huyo mapenzi yalikuwa yamemtia mbavuni hakuwa na cha kujitetea alifurahia kuona kumbe bado kwenye dunia kama hii kuna watu wana mapenzi ya dhati namna hiyo.





Jiji lilikuwa limetulia sana, watu hawakuwa wengi sana japo hawakuisha kabisa kama kawaida ya siku zote alikuwa akionekana mtu mmoja mmoja mtaani na kuufanya usiku huo kuwa wa kutisha ukitoa maeneo ya kumbi za starehe ambako watu huwa hawalali mpaka pale inapokuwa inafika siku nyingine, ndani ya mitaa ya External kuna mtu alikuwa anafukuzwa sana na mtu ambaye alikuwa amevaa maski usoni, kukimbia kwake hakukuwa kwa kawaida alikuwa anajihami kuweza kuyaokoa maisha yake. Spidi kali alizokuwa nazo zilimfanya kujihisi atakuwa salama sana aligeuka nyuma yake hakuweza kumuona mtu ambaye alikuwa akimkimbiza kwa spidi zote hizo alienda na kusimama kwenye uwanja wa shule ya msingi kwenye njia ya kuelekea tabata alikuwa akihema sana. Kumbukumbu zake zilirudi nyuma kwa dakika kadhaa zilizopita baada ya kutoka kwenye mishemishe zake za udereva bajaji ambao alikuwa anazuga tu hapo mtaani ila uhalisia wake alikuwa ni mafia wa kutisha sana kijana huyu na ilikuwa ni siri yake kubwa sana ambayo hakuna mtu yeyote yule mtaani alikuwa akiijua, majira hayo ya usiku wa manane alikuwa amekaa kwenye vichochoro na wenzake wakiwa wanacheza kamali huku wanavuta bangi ndipo walipo muona mtu amesimama mbele yao mkao wake tu alionekana wazi kwamba alikuwa ni mwanamke hiyo iliwafanya wafurahi sana kwani walijua kupitia mwanamke huyo watazisuuza nyoyo zao vizuri sana siku hiyo.

“Kama kuna mtu ambaye siyo the spy hapa aondoke haraka sana” kauli hiyo iliwafanya vijana wote kama watano ambao walikuwa hapo wamgeukie mmoja wao huyo aliyejulikana kwa jina la The spy kama alivyokuwa maarufu sana mtaani kwake hapo hasa hasa kwenye suala la kuwaunganishia vijana wenzake madili mengi mengi ambayo yaliweza kuwapatia fedha za kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

“Oya taita huyu mtoto mzuri naona kama anakutaka hivi vipi ndilo goma lako jipya nini au anashoboka tu” mmoja wao aliongea kwa kulegeza sauti yake ya kilevi ambayo ilijaa uvundo wa bangi na ugoro.

“Ondokeni haraka sana kabla sijabadilisha maamuzi shida yangu ni huyo mmoja tu pekee ninaye mtaka nyie wengine kalaleni makwenu” Catherine aliyarudia tena maneno yake kwa ukali wakati huu alisogea zaidi huku uso wake ukiwa umefunikwa yakibakizwa macho, pua na mdomo tu pekee

“We mtoto wa kaha….” kijana mmoja kati yao wakati anasimama kauli yake ilimponza alitaka kumuita kwa dharau mwanamke huyo bahati mbaya sana kwake alizamishiwa kisu kwenye shingo yake ambacho hakikujulikana kimeingia sangapi, wenzake walirudi nyuma kwa uoga wakati huo mwenzao alikuwa anagala gala chini alihitaji msaada lakini hakuna ambaye angempa msaada kwa wakati huo haikupita muda mrefu alikakamaa na kutulia hapo hapo. Vijana walikuwa wamebaki wanne jumla yao watatu walichomoa bisibisi wanazotumia kuvamia watu pamoja na visu vyao dakika moja tu wote walikuwa wapo chini wameshika shingo zao, haikujulikana ni kasi ya aina gani ya mwanamke huyo anaitumia ila huo ndio uhalisia wote walikuwa wamekufa kikatili mno sasa alibaki mlengwa pekeyake pembeni akiwa ametulia, aliupanga mkono wake wakati huo mwanamke huyo alikirudisha kisu chake kiunoni mwake.

“Unaweza ukanijibu maswali yangu nikupe nafasi ya kuishi” lugha ya mwanadada huyu ilionekana huenda itakuwa tatizo kubwa kwa the spy lakini haikuwa hivyo alikuwa akikijua kiingereza kwa usahihi sana hicho ndicho kitu kilicho muaminisha kwamba the spy hakuwa mtu wa mtaani kama watu wengi walivyokuwa wakimjua, alicheka kwa dharau sana na kumsogelea mrembo huyo ili kuweza kumpiga ila alikuwa na bahati mbaya sana mkono wake ulidakwa kwa usahihi alivutwa na kupigwa ngumi sita za tumbo kiasi kwamba alitapika damu, alipigwa teke la ghafla la kidevu na kusindikizwa na teke la uso ambalo lilizungushwa kama kuna mtu anatumia limoti, lilimpeleka mpaka kwenye kona ya nyumba moja iliyokuwa jirani na hapo alikuwa anaona nyota nyota mbele yake, macho yake yalivyokuja kuona vizuri alikuwa akishuhudia goti likishuka kwa nguvu kwenye uso wake alilikwepa kwa kujizungushia upande wa pili sehemu ambayo goti la mrembo huyo lilifikia ilibonyea na kuifanya nyumba hiyo kutikisika sana sasa the spy alielewa mtu aliyekuwa mbele yake kilikuwa ni kifo hakuweza kusimama tena na ndiyo sababu kubwa iliyo mfanya akimbie sana ili kuyasalimisha maisha yake mbele ya mtu huyo aliyekuwa akimkimbiza kwa kasi kubwa bila kujua alikuwa akihitaji nini kwake.

Alimaliza kukumbuka alichokuwa anakiwaza kichwani mwake, alikuwa amepumzika tayari na uchovu wa kukimbia baada ya kumchenga mwanamke huyo ambaye alikuwa anayasakama sana maisha yake, aligeuka ili aondoke hiyo sehemu lakini alihisi kama moyo wake unapasuka baada ya kumuona mtu huyo amesimama nyuma yake tena alionekana wazi kwamba alikuwa hapo kwa muda mrefu kidogo. Aliogopa sana jasho ambalo lilianza kupotea kwenye mwili wake lilirudi sana kwa kasi kitu ambacho hakukitarajia siku yake ilikuwa imekuwa mbaya sana, aligeuka ili akimbie hakufika hata hatua tatu alidondoka chini akiwa ameishikilia shingo yake akapoteza fahamu.

Hakuelewa ni muda gani ulikuwa umepita ila alikuja kushtuka sehemu ambayo ilikuwa na kiza kinene sana kichwa chake kilikuwa ni kizito mno alijaribu kukiinua ila mbele yake hakuona kitu chochote, alijaribu kutikisika hakuweza aliishia kukuzungusha kiti ambacho ni wazi kilikuwa cha chuma kwa makelele ambayo kilikuwa kinapiga, aligundua kwamba alikuwa amefungwa alijitahidi sana kuweza kuona kama kulikuwa na nafasi ya yeye kuweza kujiokoa lakini alitulia baada ya kuona alikuwa akijiumiza tu aliisubiri hatima ya mtu ambaye alikuwa amemuweka hapo ndiyo iamue urefu wa maisha ambayo alikuwa anaweza akaendelea kuyaishi mpaka muda huo. Mwanga mkali sana uliyamulika macho yake, ilikuwa ni ghafla sana hivyo macho yake yaliweza kumuuma mno aliyafumba kwa muda wa dakika zaidi ya mbili kwa mbele yake alikuwa akisikia mlio wa buti ambalo bila shaka kwa aina ya kiatu hicho kilikuwa kikivaliwa na wanawake hicho ndicho kilicho mkumbusha tukio lililopita la mtu ambaye alikuwa anamfukuza sana, alikuwa anayameza mate kwa nguvu kubwa sana hakujua kama mtu huyo alikuwa yupo tayari kumuachia.

“Who are you (wewe ni nani)?” ilikuwa ni sauti yenye utulivu sana ndani yake hapo ndipo alipopata bahati ya kuisikia sauti hiyo akiwa kwenye utulivu mkubwa sana aligundua huyo lazima alikuwa mwanamke mrembo sana.

“The spy”

“I know it then what are you (wewe ni nani)”

“The spy”

“Ok” watu walikuwa wapo kwenye kazi kijana huyu alionekana kama analeta sana masiara, huwa unashauriwa pale unapokutana na mwanamke kwenye matukio ya kutisha sana kwa mfano kuvamiwa na majini au makomando unatakiwa kuwa mpole na kumjibu vile anataka kwa ufasaha, hawa viumbe wakibadilika wanatisha na ni hatari sana, wana hasira mno, ni viumbe ambavyo huwa vina roho ngumu sana japokuwa ndivyo viumbe bora zaidi kuwahi kuishi kwenye hii dunia na wana huruma sana ila usije ukaomba wakakubadilikia hii dunia yenyewe utatamani uikimbie. Mrembo huyo ambaye kiuhalisia alikuwa ni Catherine Yudel alitembea kwa mikogo sana na umbo lake ya kumtoa akili mwanaume yeyote yule rijali alienda kwenye kona moja ambapo palionekana kulundikwa kwa nondo zilizokuwa zinatumika kujengea jengo hilo kubwa ambalo lilikuwa bado halijaisha. Nondo ndefu ilizamishwa kwenye paja la kijana wa watu kwa hasira ikatokezea mpaka chini kabisa kelele zake zilimponza alipigwa ngumi nzito kwenye uso wake ilimtaka kuwa mkimya bila makelele yoyote yale kwani hayo mambo aliyahitaji mwenyewe laiti kama angekuwa amejibu mapema kile alichoulizwa hayo mambo yasingeweza kumkuta kabisa.

“Such a beautiful woman how could you be such a monster?” hakuamini kama mwanamke mrembo kama huyo anaweza kuwa na roho ngumu ya kutisha sana kiasi hicho.

“Binadamu wengi huwa wanapotea kwa sababu ya kuchanganywa na uzuri wa vitu ndiyo maana mapenzi ndicho chanzo cha vifo vingi sana duniani kwa sababu huwa wanakuwa na matamanio na vitu vizuri bila kuujua uhalisia wa vitu hivyo kwani macho yao huwa yanapelekeshwa sana na tamaa hivyo huwa hawaoni vitu vingine vyovyote vile sasa nahitaji uniambie wewe ni nani” maumivu huwa hayavumiliki hata kama ukivumilia lazima itafika muda mwili wako wenyewe utakuhukumu tu pale unapokuwa umechoka kupokea mateso na hauwezi kuhimili tena ilimlazimu the spy kwa jina alilokuwa amejulikana kuongea ukweli ili aweze kuyaokoa maisha yake.

“Jina langu halisi naitwa Ismail Mwandepo ni mzaliwa wa jiji la Mbeya, nimemaliza masomo yangu ya komputa kwenye chuo cha MBEYA UNIVERSITY OF SCIENCE AND TECHNOLOGY miaka mitano iliyopita kuna ndugu yangu ambaye alipotea mpaka leo huwa hajulikani alipo alinifuata na kuniambia kwamba amenitafutia kazi hapa mjini, kutokana na maisha yalivyokuwa magumu kule nyumbani basi nilimshukuru sana hiyo neema kunidondokea mimi. Mwanzoni nilishangaa kidogo kwa sababu sikuwahi kupelekwa sehemu ambayo ina ofisi ya hiyo kampuni ambayo niliambiwa na wala sikuwahi kuijua jina lake mpka juzi hapo nilisikia kwamba inaitwa M96 OWNER’Z sijui kwa usahihi kwamba hiyo kampuni inajihusisha na nini hasa kikubwa mpaka wawe wanawalipa wafanyakazi wake pesa nyingi sana namna ile sikutaka kufuatilia sana kwa sababu shida yangu ilikuwa ni pesa tu lakini kwenye makaratasi inajulikana kama inasindika nyama hiyo ndiyo kampuni ambayo mimi huwa nafanya kazi hapo mpaka leo japokuwa sijawahi hata siku moja kufika makao makuu ya kampuni hiyo namimi huwa napita kama wapitaji wengine tu wakiliangalia jengo hilo kwa mbali” alitulia baada ya kujielezea kidogo nidhamu ilikuwa imemkaa.

“Kwenye hiyo kampuni wewe unafanya kazi gani?”

“Mimi ni informant (mtu wa taarifa)” huwa napewa taarifa na mahali pa kuzifikisha kwa muda mwafaka kisha ikihitajika nazirudisha tena”

“Nani huwa anakupa kazi ya kutuma na kurudisha hizo taarifa?”

“Ni swali gumu sana kwa sababu watu hao wakinihitaji huwa wananifuata mwenyewe na hajawahi kuja mtu mmoja mara mbili kila anavyokuja mtu huwa anakuwa ni mwingine kwahiyo sijawahi kumkariri kwani wanabadilika sana hawamtumii mtu mmoja”

“Sasa wewe hizo taarifa huwa unazirudishaje kwa hao watu wanao kuagiza?”

Unaambiwa ni bora ukutane na shetani ila sio pale mwanamke anapo badilika huwa wanakuwa viumbe wa kutisha sana The spy alikuwa ameingia cha kike Leo kuzoea watu asio wajua.....52 niseme bye-bye
Bux the story teller
STORY: I WANT TO DIE JUDGE (NATAKA KUFA HAKIMU)
STORY WRITER: FEBIANI BABUYA
STORY TELLER: Bux the story teller
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU

TULIPO ISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI.......

“Ni swali gumu sana kwa sababu watu hao wakinihitaji huwa wananifuata mwenyewe na hajawahi kuja mtu mmoja mara mbili kila anavyokuja mtu huwa anakuwa ni mwingine kwahiyo sijawahi kumkariri kwani wanabadilika sana hawamtumii mtu mmoja”

“Sasa wewe hizo taarifa huwa unazirudishaje kwa hao watu wanao kuagiza?”

ENDELEA...............................

“Kukiwa na taarifa za mhimu huwa wanakuja wao wenyewe kuzichukua na wanaondoka kwa sasa sijawahi kufanya nao mawasiliano ya simu kabisa”

“Kwahiyo nikihitaji kukutana nao inabidi niende moja kwa moja kwenye kampuni yao?”

“Pale uwe makini sana kama utaenda kwa sababu ile ni kampuni kama kampuni zingine na shughuli zinazo fanyika pale ni za halali hivyo kama ukienda kichwa kichwa utafunguliwa mashtaka serikalini kwa sababu wanapewa kipaumbele sana na serikali kwani ni watu wanao jitoa sana kwenye jamii huwezi ukajua chochote kinacho endelea hapo hata kama ukifanya kazi miaka kumi ndio maana mimi mwenyewe mpaka leo huwa sijui kampuni ndani yake kuna nini mpaka tunalipwa pesa nyingi sana namna hii kazi yangu napewa taarifa kuzituma na kurudisha majibu basi kwa mwezi naingiziwa milioni hamsini” maelezo yake the spy yalikuwa kama masiara sana ili huo ndio uliokuwa uhalisia watu wanafanya kazi kwa weledi sana siku hizi hauwezi kupewa kila kitu cha mhimu kinacho endelea ndani ya kampuni ni watu wachache sana wanaweza kuzipata taarifa nyeti za kampuni husika. Catherine aligundua kijana huyo hakuwa anahusika moja kwa moja kwenye hayo matukio ni njaa tu ndiyo ilikuwa inamsumbua japo alishangaa sana kazi nyepesi kama hiyo mtu analipwa milioni hamsini za kitanzania na namna jinsi makampuni yanavyolipa pesa ndogo alijawa na hamu ya kuwajua sana hao watu.

“Pole sana kwa nilicho kifanya kwa marafiki zako”

“Mambo ya kawaida tu hayo”

“Kwanini unajiita the spy?”

“Kwa sababu kazi yangu haina utofauti sana na wapelelezi unajua mtu mwenye taarifa za mhimu ndiye huwa ana maana kubwa kuliko hata watu wanaozitaka taarifa hizo ina maana yeye akiamua kuzivujisha au kupotea nazo inakuwa ni hatari sana”

“Vipi hauna familia labda huko kwenu”

“Familia ipo tena kubwa tu”

“Kwanini usiache hizi kazi ukaishi na familia?”

“Wanajua kila kitu kwenye maisha yangu na hicho ndicho kitu ambacho huwa wanawashinda watu wengi sana wanautumia udhaifu wako kwa ajili ya kukufanya uzifanye kazi zao kwa usahihi ukienda nao kinyume tu familia yako yote hakuna mtu wanamuacha wanaweza wakamuua kila mtu. Hivyo nikisema niache kazi kwa hawa watu lazima nitajiingiza kwenye hatari kubwa sana, huwa nawatumia familia yangu pesa nyingi sana ambazo kiufupi zimebadilisha sana maisha ya nyumbani saivi baba na mama yangu wanaishi kwenye nyumba nzuri, kaka zangu wote na dada zangu nimewafungulia biashara, wadogo zangu wote wanasoma shule za gharama kwa pesa ninazo zipata na wana furaha kubwa sana sasa angalia mwenyewe nikiacha kazi maana yake ile furaha yote ya familia inaenda kutoweka nitaonekana mwanadamu wa hovyo sana hata mbele za mwenyezi MUNGU kwa kuiua familia yangu kwa mikono yangu mimi mwenyewe.” Catherine alishusha machozi kwa kumuonea huruma kijana huyu, “siku zote maisha yanakupa somo la kuto mchukulia mtu poa kwa sababu ya mwonekano wake au kwa sababu ya udhaifu wake fulani mdogo ambao huenda wewe unauona machoni pake ila maisha yana mafunzo mengi sana mwanangu jitahidi sana kuwa mtu wa watu, pesa ziko kwa watu, maisha wanayaishi watu, dunia ni watu, amani ni watu kuna kufa na kutoweka duniani fanya mambo makubwa ya kuinufaisha jamii ili uje ukumbukwe na watu” ni jioni moja anakumbuka maneno hayo alikuwa anaambiwa na baba yake baada ya kutoka kuapishwa kuwa komando wa nchi ya Cuba baba yake alimuasa sana asiweze kutumia nguvu yake vibaya kwa sababu ya kuwatesa watu, nguvu yake itumike kwenye kuwalinda watu, aitumie kwenye kutetea amani ya watu, ilete furaha kwa watu na hayo ndiyo maisha ambayo anapaswa kuyaishi mwanadamu yeyote yule sehemu yoyote anayokuwepo.

Kijana Ismail waweza kumuita the spy alikuwa ni mfano wa kuigwa kwa vijana wote wengi wa rika lake, mjini alikuwa akiishi maisha ya kawaida sana wengi wakimjua kama dereva bajaji na mzee wa mishe mishe mjini ambapo aliwaunganisha wenzake wengi sana kuweza kuwapatia mishe za kuingizia chochote kilichofanya mikono yao kwenda kinywani kila siku na walimshukuru sana kwa hilo, hakuja mjini kuishi maisha ya starehe ambayo vijana wengi wakipata pesa kidogo tu wanaenda kuzitupa huko, alikuwa halali usiku kucha lakini familia yake nzima ilikuwa inaishi maisha mazuri sana huku usiku aking’atwa na mbu kila siku na hivi ndivyo mwanaume anavyo takiwa kuwa, Ismail alikuwa na kila sifa ya kuwa baba bora wa familia Catherine alijikuta akimsikitia sana kijana huyo alikuwa akistahili kuishi maisha bora sana lakini kuna neno linaitwa dunia ambalo ndani yake kuna wanadamu hawa ndio viumbe ambao wamnafanya wenzao kupitia kwenye mazingira magumu sana kama haya. Hakuwa na haja ya kuendelea kumtesa tena alimfungulia kamba alizo mfunga kisha alifungua koti lake na kutoa dawa fulani ya unga unga alimwagia eneo ambalo alikuwa ameizamisha nondo kikatili sana, Ismail aliyafumba macho yake yakitoka machozi kwa maumivu makali sana ya dawa hiyo ambayo alikuwa amewekewa, alishangaa kidonda kinaanza kukauka.

“Hiyo dawa utaitumia mara tatu kuweka hapo baada ya wiki moja mguu wako utakuwa umepona kabisa na hiyo alama itakuwa imetoka hapo, kumbuka tu kuwa mtu mwema siku zote siku moja nitarudi na kukutafuta nikiwa na mwanaume wa ndoto zangu goodbye the spy” dunia ilimjaza ujinga ila leo watu ambao wapo duniani walikuwa wanampa somo la maisha, licha ya kufunguliwa pale the spy alibaki amekaa kwa muda mrefu sana akiwaza na kuwazua namna mwanamke huyo alivyokuwa mrembo lakini alikuwa anatisha sana kukutana naye, alikuwa anapigania penzi lake la dhati na kijana huyo aliahidi atamuombea afanikishe hiyo safari yake salama japo alijua wazi safari hiyo lazima ingekuwa ngumu sana kwa upande wake, mpaka kunakucha asubuhi na mapema ndio muda ambao alitoka humo ndani.






DERISHRAWAR PRISON
Mponda street Vingunguti

“Mitaa maarufu sana ndani ya jiji la Dar es salaam ambayo inasifika sana kwa uchinjaji wa nyama hususani nyama ya Ng’ombe, kuna mhindi mmoja alikuwa akigeuza macho yake huku na huku kuona kama kuna mtu yeyote alikuwa anamfuatilia alivyo jiridhisha hakukuwa na mtu yeyote yule nyuma yake alikatiza kwenye maeneo ya machinjioni hayo alipanda ukuta akatokezea upande wa pili akawa anashuka njia moja ambayo ilikuwa imekunja kwenye kichochoro kimoja ambacho kilikuwa kimekomea sehemu na mbele yake kulikuwa na nyumba nzuri ya kawaida kwa mtu mwenye maisha yake ambayo sio ya wasiwasi sana. Aliruka kwenye fensi ya hiyo nyumba akafika mlangoni na kutoa funguo yake kwenye mfuko akafungua na kuufunga mlango huo ndani, sebule haikuwa na kitu chochote kile hata kimoja lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwa sababu nyumba kama hiyo ilitarajiwa kuwa na samani za kutosha ndani yake. Alipitiliza moja kwa moja chumbani ambako nako kulikuwa na kitanda kimoja tu,godoro na komputa ndogo ya mkononi kuna pafyumu aliitoa kwenye begi lake akaipulizia kwenye kila eneo ambalo alikuwa amewahi kushika akiwa ndani ya nyumba hiyo ambayo ilikuwa ni ya kwake mwenyewe lakini alikuwa akiingia kwa machale sana na alionekana hiyo sehemu huwa anafika mara chache sana mhindi huyu ambaye hakujulikana kipi kilikuwa kimemsibu mpaka awe na wasiwasi sana namna hiyo.

Baada ya kumaliza hakufunga sehemu yoyote zaidi ya kuweka laptop yake kwenye begi kisha kitandani akamwagia tindikali, lilikuwa ni suala la sekunde tu kitanda na godoro vyote vilimomonyoka, akavaa kofia yake kichwani ambayo ilimsaidia kuuficha uso wake kwa kiasi fulani kisha akatoka humo ndani alionekana kuwa na haraka kupita kiasi, wakati anatembea kuelekea sehemu ambayo alipita mara ya kwanza kuingia humo ndani mbele yake aliona kuna mtu amekaa ile sehemu akiwa anaizungusha bastola kwenye mkono wake.

“Mbona mapema namna hiyo ndugu yangu unahitaji kuikimbia mpaka nyumba yako wakati unajua kabisa kuna wageni wanakuja, haya nipe sababu inayokufanya nyumba yako mwenyewe unaingia kwa machale sana namna hii haufungui hata mlango” sauti ambayo ilionekana wazi haikuwahi kuwa ya mapenzi ilimtoka mwanaume ambaye alikuwa amekaa hapo chini akiwa anaizungusha bastola yake.

“Hapa ni kwangu sasa wewe inakuhusu nini hata nisipo pitia mlangoni?” aliongea kwa ujasiri mhindi huyu na kiswahili chake kilicho pinda pinda kiasi.

“Hujanijibu swali unaniuliza swali naomba begi lako hilo kisha uende na usije ukarudi tena kwenye ardhi ya nchi hii” mwanaume huyo aliongeza tena akiwa ameangalia chini bastola yake bado ilikuwa ipo kwenye mikono yake.

“Sio kirahisi hivyo ndugu yangu”

“Kwa sababu unajua ulicho kifanya sio, sasa utaileta kwa lazima” Mwanaume huyo alinyanyuka na kuanza kumsogelea huyo mhindi ambaye taratibu alianza kurudi nyuma hatua zake zilikoma ghafla baada ya kugundua nyuma kulikuwa na watu ni kweli walikuwa wapo wanaume wawili ambao walikuwa wakipokezana sigara nao muda huo walisimama mmoja wao akaizima sigara hiyo. Kilichokuwa kimebakia kwenye mkono wake ilikuwa ni kujitetea tu basi vinginevyo asingeweza kutoka kwenye hilo eneo akiwa bado ni mzima wa afya, aliihesabu miguu yake kwa makadirio ya kuwafikia watu waliokuwa nyuma yake, hesabu zake zilienda sawa na alidhihirisha kweli hesabu duniani chimbuko lake ni kwenye bara la Asia kwenye nchi hiyo inayosifika sana kwenye mapenzi duniani naizungumzia India hapa sio China. Aliwafikia watu wale baada ya kujigeuza na kuwapatia maumivu ya vifua kisha kuna sindano ndogo aliwachoma wakiwa wananyanyuka hawakuendelea tena kusimama walilala chini kwa usingizi mzito, mwanaume aliyekuwa na bastola mbele yake alikuwa amesimama tu anamuangalia anacho kifanya bastola yake ikiwa mkononi, mhindi huyu aliogopa sana kwani kama angefanya hata kosa la sekunde tu risasi hizo zilikuwa tayari ni sehemu ya maisha yake kuwa mafupi hakuna namna angeweza kuzikwepa.

“Nakupatia nafasi ya mwisho ya kuishi nairusha hii bastola hewani ambapo itaenda umbali wa mita hamsini kupanda juu ni nzito sana hii bastola ni tofauti na za kawaida kama ikirudi chini hapa ukiwa bado haujadondoka chini basi mimi mwenyewe nakupa ruhusa ya kwenda nchini kwenu India na hilo begi japo lina kitu cha hatari sana ila nakupa hiyo nafasi itumie vizuri” mwanaume huyo maelezo yake yaliendana na vitendo vya moja moja mkono wake ulikunjwa misuli iliyoshiba sana ilituna kwenye mikono hiyo akiwa ameishikilia bastola nzito mno ambazo huwa ni adimu sana kuzipata duniani na huwa zinatengenezwa maalumu kwa ajili ya watu maalumu pia ilirushwa hewani ikawa inapandisha juu haikuonekana tena mhindi alikuwa anatapika damu chini ujio wa mtu huyo hata hakuuona amekuja sangapi alishangaa tu begi lake lipo pembeni nayeye yupo chini anavuja damu alijinyanyua kwa sarakasi nzuri bahati mbaya sana kwake alikutanishwa na goti la kiuno hakuwa na uhakika kama atakuwa na uwezo wa kusimama tena, mguu mpana na mnene uliokuwa umejaa kwenye buti moja ambalo lilikuwa limesafishwa sana ulijaa usoni kwake alianza kuona kama kuna nyota zinapita hewani hakuelewa nini kinacho endelea alikuja kushituka risasi zinazama kwenye mwili wake mifupa ya kwenye miguu ilikuwa imevunjwa kwa risasi hizo nzito pamoja na mikononi, kiunoni alipigwa risasi moja.

DERISHRAWAR PRISON ni gereza la namna gani, linamhusu nani, huyu Mhindi ni nani, kwanini aishi kwa machale kwenye nyumba yake mwenyewe hili begi ambalo linamhatarishia maisha yake Lina nini hasa ndani yake kikubwa cha namna hii????......53 inafika mwisho usikose mwendelezo bado hujaijua michezo ya akili✍️

Bux the story teller
 
Back
Top Bottom