Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Akwilina: Padri Mayanga ataka aliyeua awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania

Kuna wakati inabidi mtu uache kucomment tu,kwa sababu fulani.
 
Father Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohana Mbatizaji Ruhanga anayeendesha ibada ya kuaga mwili wa Akwilina katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) amesema serikali iache ujanja ujanja, imtafute aliyempiga risasi iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwiline.

"Mimi kama mtoto wa Mungu kama wengine walivyo watoto wa Mungu niwaombe tufanye kazi ya upatanishi na naomba wale ambao wana hiyo nafasi na kwa hili lililotokea kwa mwanetu Akwilina limetuumiza na kwa jinsi lilivyotuumiza nafikiri linahitaji kuponywa na namna moja tu ya kuliponya tunawaomba wale wahusika ambao wana madaraka ya kuweza kulisaidia. Huyu aliyefanya kitendo hiki baada ya kujulikana aliombe taifa hili msamaha ni hicho tu hatuna namna nyingine hata tukimfunga miaka 30 au 40 Akwilina hawezi kurudi amekwenda lakini aliyefanya huenda kwa nia nzuri ikitakoea bahati mbaya tunaomba vyombo vinavyohusika vikimaliza utaratibu wake akajulikana huyo mtu hata kwa kupitia TV awaombe wana Mungu msamaha" alisema Father Raymond

Father Raymond aliendelea kusema kuwa

"Kheri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu vinginevyo hatutafika mbali, tumuombe Mungu kila mmoja wetu katika imani yake leo ni Akwilina huenda kesho itakuwa ni wewe sasa hatutaki hilo liendelee, na hilo halitaendelea tu kama mtu atakubali kuomba msamaha kujinyenyekeza, kuwa mnyenyekevu na kukubali nimekosa mimi, nimekosa sana nawaomba msamaha kwisha tunaendelea kama familia hakuna asiyekosea. Lakini unapojaribu kutafuta mbinu ukaliweka hivi unaliweka vile unazidi kuumiza kwa sababu mimi kama mzazi sitaelewa

"Naomba nisema hapa bila hata kigugumizi nafikiri wenye nafasi hii si wengine ni serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaiomba kama ilivyojitolea kuweka haya mazishi katika level hiyo, tunawaomba pia watusaidie kwa sababu wao ndiyo wamepewa dhamana ya maisha yetu wote hapa, na sisi kama watoto wa familia hatulingani kama vidole vyetu tunaimani kwamba serikali yetu itatusaidia katika kulipatanisha, katika kurudi kufanya kazi kama watoto wa familia moja"

 
Yaani sana hawajemtendea haki marehemu leo hii ni kama wao ndugu wamempiga risasi nyingine kumaliza kabisa. shame kwa wote waliohusika katika hili. na siongelei serikali tu hata vyama sio sehemu yao.
 
Leo hii kuna matukio makubwa mawili yanafanyika ambayo yametokana na athari za maandamano yaliyofanyika siku ya Ijumaa Februari 16, 2018.

Tukio la kwanza ni la kuagwa kwa mwili wa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilin linalofanyika chuoni hapo; Tukio la Pili ni la Wafuasi wa Chadema waliokamatwa siku ya maandamano wakipandishwa Mahakamani.

Katika matukio yote mawili hatukumuona Mwenyekiti Mbowe aliyekuwa akiongoza maandamano haramu yasiyo na kibali ambayo yalisababisha madhara yote haya. Hajui pasipo kuitisha maandamano yasiyo na kibali pasingetokea madhara tunayoyaona leo?

Bado najiuliza, Mwenyekiti hajahudhulia msiba wa Akwilina kwa sababu hajaguswa nao? Ama sio wa muhimu kwake? Ama shida zetu sio zake? Inauma sana!

Kama haitoshi wale Wafuasi waliokamatwa wamekwenda Mahabusu kwa kukosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5 tu. Kweli wanakwenda Mahabusu kwa sababu wamekosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5?

Jambo la kushangaza, hakukuwepo hata kiongozi mmoja toka Chadema ambaye alikwenda Mahakamani kuwa nao bega kwa bega. Wanakwenda mahabusu kizembe kwa kuwasikiliza Wanasiasa ambao leo hii wamewatelekeza!!

Wamejikuta kwenye matatizo lakini wale waliosababisha wao wapate matatizo hawapo nao pamoja. Inauma sana!

Ninapofikia hapa nakumbuka ule msemo wa Rais Mstaafu Mzee Kikwete aliosema "Akili za kuambiwa, changanya na za kwako".

Hili ni funzo kwetu sote, tunapoambiwa na Wanasiasa tukafanye jambo ambalo tunajua tutakuwa matatani kisheria tuwe makini kuchanganya na akili zetu maana shida zitakazotupata zitakuwa ni zetu na si zao, mateso yatakuwa kwetu na si kwao.

Narudia tena kuwasihi, akili za kuambiwa changanya na za kwako.

*Na Thadei, Mwanaharakati Mpambanaji*
 
inasikitisha sana. ALIYE FYATUA RISASI NA KUSABABISHA MAUWAJI YUKO WAPI?
nilitarajia kichwa cha mada yako kiwe hivyo!!!
 
maandamano yapo kwenye katiba muulize huyu muuwaji wenu aliyetoa ruhusa ya kuuwawa watanzania kuchinjwa nk nk nk
 
inasikitisha sana waliomuua hawajakamatwa hadi sasa
 
R.I.P
 
Kuna wakati mtu unatoa machozi na uchungu mwingi moyoni, sikutegemea kudondosha chozi leo ila daah umeniliza we mtoto, am speechless ila hakika huyo alosababisha kifo chako damu yako itakaa juu ya kichwa chake daima. Rest in peace. Amen
 
Wameenda mahabusu kwa muda gani mkuu!? Dah! Inasikitisha sana, haswa kama wana familia zinazowategemea maishani.
 
Gone too soon Akwilina because of policcm
 
Raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani. Amina. x 3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…