Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Akwilina: Padri Mayanga ataka aliyeua awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania

Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Akwilina: Padri Mayanga ataka aliyeua awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania

Anayedhani yuko salama asikilize vizuri clip ya mama Aquilina akimwambia prof Ndalichako kwamba alikuwa akisikia kwenye vyombo vya habari watu wanauawa na polisi lakini hakutegemea hata siku moja kwamba hilo litatokea kwa mmoja Wa wanafamilia wake. AJIDHANIAYE AMESIMAMA AANGALIE ASIANGUKE.
Leo hii kuna matukio makubwa mawili yanafanyika ambayo yametokana na athari za maandamano yaliyofanyika siku ya Ijumaa Februari 16, 2018.

Tukio la kwanza ni la kuagwa kwa mwili wa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilin linalofanyika chuoni hapo; Tukio la Pili ni la Wafuasi wa Chadema waliokamatwa siku ya maandamano wakipandishwa Mahakamani.

Katika matukio yote mawili hatukumuona Mwenyekiti Mbowe aliyekuwa akiongoza maandamano haramu yasiyo na kibali ambayo yalisababisha madhara yote haya. Hajui pasipo kuitisha maandamano yasiyo na kibali pasingetokea madhara tunayoyaona leo?

Bado najiuliza, Mwenyekiti hajahudhulia msiba wa Akwilina kwa sababu hajaguswa nao? Ama sio wa muhimu kwake? Ama shida zetu sio zake? Inauma sana!

Kama haitoshi wale Wafuasi waliokamatwa wamekwenda Mahabusu kwa kukosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5 tu. Kweli wanakwenda Mahabusu kwa sababu wamekosa dhamana ya Tsh. Milioni 1.5?

Jambo la kushangaza, hakukuwepo hata kiongozi mmoja toka Chadema ambaye alikwenda Mahakamani kuwa nao bega kwa bega. Wanakwenda mahabusu kizembe kwa kuwasikiliza Wanasiasa ambao leo hii wamewatelekeza!!

Wamejikuta kwenye matatizo lakini wale waliosababisha wao wapate matatizo hawapo nao pamoja. Inauma sana!

Ninapofikia hapa nakumbuka ule msemo wa Rais Mstaafu Mzee Kikwete aliosema "Akili za kuambiwa, changanya na za kwako".

Hili ni funzo kwetu sote, tunapoambiwa na Wanasiasa tukafanye jambo ambalo tunajua tutakuwa matatani kisheria tuwe makini kuchanganya na akili zetu maana shida zitakazotupata zitakuwa ni zetu na si zao, mateso yatakuwa kwetu na si kwao.

Narudia tena kuwasihi, akili za kuambiwa changanya na za kwako.

*Na Thadei, Mwanaharakati Mpambanaji*

Bila bila
Mkuu,
Poise, huwa sishabikii vyama.vya siasa.

Jiulize, NEC na DED wa Kinondoni umewaona kwenye msiba wakisindikiza Akwilina!?

Au umewaona katika mahakama ya kisutu wakisomewa mashitaka ya kuwa chanzo kikuu cha kifo cha Akwilina B!?

Acha kufanya propaganda za kiuchwara mbuzi kwenye mambo yasiyohitaji siasa.

Tanzania, tatizo lake ni
CCM. CCM must go...

Kagame. Kagame must be stopped visiting Tanzania.
(Maana, amefanywa kuwa waziri na mshauri wa serikali ya ccm ndiyo matokeo yake hayo)

Management ya NEC na DED wa Kinondoni watumbuliwe wafungwe. Ndiyo wauaji polisi ilikuwa ni chaneli tu ya kuua ila.NEC, DED na CCM ndiyo wauaji.

Mwisho,
We need an immediate justice for our daughter Akwilina B.

R.I.P Binti, Akwilina A. B.
Ndoto zako zote zimezimwa ghafula kama vile mshumaa uzimwavyo.

Daima tutakukumbuka Binti, Kristo Yesu akuangazie mwangaza wake wa milele. Amina.
 
Jinyonge basi ndio hvyo ni shithole....[emoji23] nchi ya ngosha hii aka fidq
teh..teh... nauna sasa unataka tukupime mkojo!
ngosha ataondoka na atakuja mwingine naye ataondoka.
lazima ukubali mambo hayawezi kuwa sawa siku zote wakati mwingine tunakosea na inatupa fursa ya kujipanga zaidi na sio kukata tamaa na kujikataa hii haifai.
bado haijafikia hapo hii nitabisha mpaka bando liishe na nitatoa like mpaka zikatae lakini siwezi kukubali kuilinganisha nchi yangu na tobo chafu!
 
Hii shughuli iishe jamani maisha yaendelee. Tuendelee kuijenga nchi .

Ziroseventytwo
Mkuu,
Avatar yako na ID yako vinasadifu ulichokiandika.

Siku ikiwa kwako au kwenu utaelewa.

CCM must go...

Kagame must be stopped visiting Tanzania.

R.I.P.Binti Akwilina A. B.

Ndoto zako zote zimezimwa ghafula kama vile mshumaa uzimwavyo!!
 
Daah dunia hii hakuna haki kabisa, Dada wa watu walimpiga risasi na kumuua ili tu wasalie madarakani! Hatari sana hii, halafu kuna wapumbavu fulani nao wanaunga mkono harakati hizi!
 
teh..teh... nauna sasa unataka tukupime mkojo!
ngosha ataondoka na atakuja mwingine naye ataondoka.
lazima ukubali mambo hayawezi kuwa sawa siku zote wakati mwingine tunakosea na inatupa fursa ya kujipanga zaidi na sio kukata tamaa na kujikataa hii haifai.
bado haijafikia hapo hii nitabisha mpaka bando liishe na nitatoa like mpaka zikatae lakini siwezi kukubali kuilinganisha nchi yangu na tobo chafu!

Chiwa
Mkuu,
Nataraji hii sentence inakubalika.
African countries they have shithole leaders.
 
Asante sana mleta mada!
Rip Aqulina
 
Wandanba Uwe na aibu jp kidogo acha kutetea upuuzi au kwakuwa ni msiba wa mwenzio. Ipi siku utakuwa kwako hutasema ujinga wako huo
 
Father Raymond Mayanga wa Parokia ya Yohana Mbatizaji Ruhanga anayeendesha ibada ya kuaga mwili wa Akwilina katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) amesema serikali iache ujanja ujanja, imtafute aliyempiga risasi iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwiline.

"Mimi kama mtoto wa Mungu kama wengine walivyo watoto wa Mungu niwaombe tufanye kazi ya upatanishi na naomba wale ambao wana hiyo nafasi na kwa hili lililotokea kwa mwanetu Akwilina limetuumiza na kwa jinsi lilivyotuumiza nafikiri linahitaji kuponywa na namna moja tu ya kuliponya tunawaomba wale wahusika ambao wana madaraka ya kuweza kulisaidia. Huyu aliyefanya kitendo hiki baada ya kujulikana aliombe taifa hili msamaha ni hicho tu hatuna namna nyingine hata tukimfunga miaka 30 au 40 Akwilina hawezi kurudi amekwenda lakini aliyefanya huenda kwa nia nzuri ikitakoea bahati mbaya tunaomba vyombo vinavyohusika vikimaliza utaratibu wake akajulikana huyo mtu hata kwa kupitia TV awaombe wana Mungu msamaha" alisema Father Raymond

Father Raymond aliendelea kusema kuwa

"Kheri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu vinginevyo hatutafika mbali, tumuombe Mungu kila mmoja wetu katika imani yake leo ni Akwilina huenda kesho itakuwa ni wewe sasa hatutaki hilo liendelee, na hilo halitaendelea tu kama mtu atakubali kuomba msamaha kujinyenyekeza, kuwa mnyenyekevu na kukubali nimekosa mimi, nimekosa sana nawaomba msamaha kwisha tunaendelea kama familia hakuna asiyekosea. Lakini unapojaribu kutafuta mbinu ukaliweka hivi unaliweka vile unazidi kuumiza kwa sababu mimi kama mzazi sitaelewa

"Naomba nisema hapa bila hata kigugumizi nafikiri wenye nafasi hii si wengine ni serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunaiomba kama ilivyojitolea kuweka haya mazishi katika level hiyo, tunawaomba pia watusaidie kwa sababu wao ndiyo wamepewa dhamana ya maisha yetu wote hapa, na sisi kama watoto wa familia hatulingani kama vidole vyetu tunaimani kwamba serikali yetu itatusaidia katika kulipatanisha, katika kurudi kufanya kazi kama watoto wa familia moja"

View attachment 699840
Maneno mazito
 
Chiwa
Mkuu,
Nataraji hii sentence inakubalika.
African countries they have shithole leaders.
ehe... hapa umesema kweli na sahihi zaidi lakini eti africa nzima yenye mali kibao tuite vile hii hapana
 
Hizi kazi za kuamrishwa amrishwa madhara yake ndiyo hayo. Unashika bunduki unaambiwa Piga wewe unapiga tu. Tunapaswa kulinda Amani siyo kuingia Vitani
 
Anayedhani yuko salama asikilize vizuri clip ya mama Aquilina akimwambia prof Ndalichako kwamba alikuwa akisikia kwenye vyombo vya habari watu wanauawa na polisi lakini hakutegemea hata siku moja kwamba hilo litatokea kwa mmoja Wa wanafamilia wake. AJIDHANIAYE AMESIMAMA AANGALIE ASIANGUKE.
Mmh maneno ya mama nmeyaelewa vzur
 
So sad.... Pumzika kwa amani Mrembo; damu yako haitamwagika bure lazima inakwenda kutenda jambo.
 
Baadhi ya waombolezaji katika ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwamo ya kumtaka waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kujiuzulu.

Ibada hiyo inafanyika leo Februari 22, 2018 katika viwanja vya NIT, Mabibo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu, wakiwamo viongozi mbalimbali wa Serikali.

Waombolezaji hao walinyanyua mabango hayo baada ya waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako aliponyanyuka kutoa salamu kwa wafiwa kama walivyofanya viongozi wengine, akiwamo mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Baadhi ya ujumbe katika mabango hayo ni; “muuaji hawezi kujichunguza na Mwigulu, Sirro kwa mauaji haya bado mko ofisini.”


Juhudi za kuwataka waombolezaji hao kushusha mabango ziligonga mwamba kutokana na baadhi ya watu waliokuwa karibu yao kuja juu, wakitaka waachwe kwa maelezo kuwa wana haki ya kufanya hivyo.


Katika salamu zake za rambirambi, Profesa Ndalichako alisema: “Rais Magufuli ameshaagiza uchunguzi ufanyike na mimi kama waziri nasisitiza vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi haraka.


“Matukio ya aina hii hayapaswi kuendelea, nimehuzunika kwa msiba huu na naomba Watanzania waungane kuiombea familia.”
Soma: Padri ataka aliyempiga risasi Akwilina awekwe wazi, awaombe radhi Watanzania -VIDEO
 

Attachments

  • mabango%2Bpic.jpg
    mabango%2Bpic.jpg
    35.4 KB · Views: 60
Dogo Bangi mbaya. wapi unakwama? mabango husika yapo wapi
 
Back
Top Bottom