SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,106
- 8,043
Umemaliza. Sitii neno zaidi.
Sio tu kwa rais.
Kukubali au kukataa ushauri ni maamuzi ya kila mmoja wetu. Ushauri sio amri. Unaweza kuukubali au kuukata.
Labda kama ni mapendekezo au maamuzi ya baraza la mawaziri au chama.
Hata hivyo, si kila ushauri unafaa. Mfano suala la covid, watanzania wengi walimuunga mkono hayati JPM.
Na kwa kadri mama anavyoongea ongea ndio tunajua dhahiri kwamba, upinzani ulianzia ndani ya serikali. Swali la kujiuliza ni je, kama angesikilizwa,kukawa na lockdown, hali ya uchumi ingekuwaje?
Baada ya yeye (mama) kuwa rais, ni mabadiliko gani amefanya?
Jambo la kukumbuka ni kwamba, wapo waliokubaliana na itikadi za hayati JPM!
Kumsema vibaya hakutasaidia kuondoa itikadi (imani) ya watanzania waliomwamini! Na inawezekana, kutokana na kutokukubaliana kwao, kwa wakati huo siri nyingi za serikali zilivuja tofauti na sasa!. [emoji848]