Mkkta Acha hizo! Kila Mbunge anaumuhimu wake kulingana na wananchi wa jimbo lake walivyoona anafaa, wewe usilaumu Mkatiba, Kazi ya Katiba ni kuwa Sheria mama ya nchi na kutoa miongozo mbalimbali na haimbagui raia wa nchi husika isipokuwa inawapa fursa, wenye sifa hizo za kuwa Wabunge hujitokeza na wakionekana wanafaa na kuchaguliwa na wananchi wawakilishe! Ni wajibu wao kuwawakilisha vema na ipasavyo waliowachagua. Zaidi ya hayo, Wakati wa kuandaa muswada wa sheria, Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kamati ya Bunge, Kikundi cha Wabunge au Mbunge atahakikisha kwamba anawashirikisha wananchi kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu ya muswada huo.