PostGE2025 Ibrahim Msengi: Kilichotokea Oktoba 29 ilikuwa ni uharamia

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Mkuu wa Mkoa mstaafu Dkt. Ibrahim Msengi kwaniaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam ameeleza kusikitishwa na uvunjifu wa amani uliotokea siku na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akiwataka wale wanaodai haki kutekeleza wajibu wao kwanza, huku pia akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume ya uchunguzi kufuatia vurugu za Oktoba 29, 2025.

Dkt. Msengi amebainisha hayo leo Jumatatu Novemba 24, 2025 Jijini Dar Es Salaam wakati wa Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mkoani humo akisema kilichotokea siku hiyi haikuwa maandamano bali ni uhalifu ulioandamana na ugaidi na kila aina ya uharamia nchini.

"Nishukuru kuwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ameshaunda Tume ambayo tunaiamini na ninaamini italeta majibu mazuri na hatua zitachukuliwa. Suala la usalama kwenye Ilani yetu ni suala la msingi na kama hakuna amani na usalama hakuna maendeleo."

"Lakini nikumbushe tu kwamba katika mambo mengi tunayoyasikia mtandaoni, linazungumziwa suala la haki pamoja na kuguswa kidogo suala la amani lakini sijasikia popote wakizungumzia suala la uwajibikaji. Unapotafuta haki lazima uwajibike kama mwananchi, kama raia. Sasa wote waliojitokeza na wale waliowatuma katika vurugu zile sijasikia wakizungumzia suala la uwajibikaji." Amesema Dkt. Msengi.

Kiongozi huyo mstaafu na Daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu kwaniaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam, akisisitiza suala la haki kuendana na uwajibikaji, amesema ikiwa kila mmoja atawajibika suala la amani na haki litakuwa na kudumu nchini, akitaka hatua za uwajibikaji zaidi zichukuliwe ili kudumisha tunu hizo za Taifa.

1764051617630.png

Naiheshimu sana MO29 Katu sikutegemea km watz wanaweza kuchangamsha hawa mabolizozo
Vyombo vya dola vilicheza kama Pele,wafanya vurugu walishobokea gari la wajeda,pale ubungo mpaka magomeni, wajeda walipokaribia mwembechai wakaongeza spidi, wafanya vurugu wakabaki wao kama wao pale mwembechai,polisi wakatokeza,wakatembeza njugu za kutosha halafu kikosi kile cha yule jamaa mwenye jezi ya yanga wakipitisha gari juu ya maiti kwenda kusaka wahalifu wengine, rudieni tena 9D
 
Vyombo vya dola vilicheza kama Pele,wafanya vurugu walishobokea gari la wajeda,pale ubungo mpaka magomeni, wajeda walipokaribia mwembechai wakaongeza spidi, wafanya vurugu wakabaki wao kama wao pale mwembechai,polisi wakatokeza,wakatembeza njugu za kutosha halafu kikosi kile cha yule jamaa mwenye jezi ya yanga wakipitisha gari juu ya maiti kwenda kusaka wahalifu wengine
*****,rudieni tena 9D
Zamu yenu inakuja.

Insha allah.

#9D save the date.
 
Mkuu wa Mkoa mstaafu Dkt. Ibrahim Msengi kwaniaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam ameeleza kusikitishwa na uvunjifu wa amani uliotokea siku na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akiwataka wale wanaodai haki kutekeleza wajibu wao kwanza, huku pia akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume ya uchunguzi kufuatia vurugu za Oktoba 29, 2025.

Dkt. Msengi amebainisha hayo leo Jumatatu Novemba 24, 2025 Jijini Dar Es Salaam wakati wa Mapokezi ya Waziri Mkuu wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Mkoani humo akisema kilichotokea siku hiyi haikuwa maandamano bali ni uhalifu ulioandamana na ugaidi na kila aina ya uharamia nchini.

"Nishukuru kuwa Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ameshaunda Tume ambayo tunaiamini na ninaamini italeta majibu mazuri na hatua zitachukuliwa. Suala la usalama kwenye Ilani yetu ni suala la msingi na kama hakuna amani na usalama hakuna maendeleo."

"Lakini nikumbushe tu kwamba katika mambo mengi tunayoyasikia mtandaoni, linazungumziwa suala la haki pamoja na kuguswa kidogo suala la amani lakini sijasikia popote wakizungumzia suala la uwajibikaji. Unapotafuta haki lazima uwajibike kama mwananchi, kama raia. Sasa wote waliojitokeza na wale waliowatuma katika vurugu zile sijasikia wakizungumzia suala la uwajibikaji." Amesema Dkt. Msengi.

Kiongozi huyo mstaafu na Daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu kwaniaba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam, akisisitiza suala la haki kuendana na uwajibikaji, amesema ikiwa kila mmoja atawajibika suala la amani na haki litakuwa na kudumu nchini, akitaka hatua za uwajibikaji zaidi zichukuliwe ili kudumisha tunu hizo za Taifa.

Hiyo tume ndiyo muendelezo wa upumqvu wao ambao umekaribia mwisho. Hiyo tume haina tofauti na tume huru ya uchaguzi
 
Vyombo vya dola vilicheza kama Pele,wafanya vurugu walishobokea gari la wajeda,pale ubungo mpaka magomeni, wajeda walipokaribia mwembechai wakaongeza spidi, wafanya vurugu wakabaki wao kama wao pale mwembechai,polisi wakatokeza,wakatembeza njugu za kutosha halafu kikosi kile cha yule jamaa mwenye jezi ya yanga wakipitisha gari juu ya maiti kwenda kusaka wahalifu wengine
*****,rudieni tena 9D
Nakuona unavyofurahia damu za watu kumwagwa na utawala wenu maccm

Endelea,

Kwa tarifa yako, hao unaowatetea ndio hawana kabisa hiyo Amani, heri yao waliotangulia

Hata hawajui chochote unachowajadili, ila wamekuachieni laana ya milele nyinyi wauwaji hata vizazi vyenu vya mwisho

Pumbavu kabisa wewe
 
Vyombo vya dola vilicheza kama Pele,wafanya vurugu walishobokea gari la wajeda,pale ubungo mpaka magomeni, wajeda walipokaribia mwembechai wakaongeza spidi, wafanya vurugu wakabaki wao kama wao pale mwembechai,polisi wakatokeza,wakatembeza njugu za kutosha halafu kikosi kile cha yule jamaa mwenye jezi ya yanga wakipitisha gari juu ya maiti kwenda kusaka wahalifu wengine
*****,rudieni tena 9D
Mmeanza kukiri wauaji ni askari polisi na hao maghost wa abduli. Risiti zinaendelea kukusanywa.
 
Vyombo vya dola vilicheza kama Pele,wafanya vurugu walishobokea gari la wajeda,pale ubungo mpaka magomeni, wajeda walipokaribia mwembechai wakaongeza spidi, wafanya vurugu wakabaki wao kama wao pale mwembechai,polisi wakatokeza,wakatembeza njugu za kutosha halafu kikosi kile cha yule jamaa mwenye jezi ya yanga wakipitisha gari juu ya maiti kwenda kusaka wahalifu wengine
*****,rudieni tena 9D
jamani hii comment sio jibu tosha ? kuwa ni miongon mwao wale wauaji

Kama silaha ndo kiburi chenu bas muda na wakati waja wazenj wote mtalia sn na kutaman kuvuka bahari kwa mbizi
 
Wale aliyowataja Mwigulu ambao walikuwa na silaha na waliuwa polisi hao ni kina nani?
 
Kwani angesemaje? Aukate mkono unaomlisha? msengi, makala, mwigulu na kitila wote wanyiramba, naona mama anawakubali, sifa yao kubwa ni unafiki dunia nzima hawa ndugu zangu!
 
Muhimu amesikika na ninauhakika atafikiwa , inshallah.

Hawa ndiyo tunaowataka .
 
jamani hii comment sio jibu tosha ? kuwa ni miongon mwao wale wauaji

Kama silaha ndo kiburi chenu bas muda na wakati waja wazenj wote mtalia sn na kutaman kuvuka bahari kwa mbizi
Zenji,mi mndengereko we FALAsi
 
Back
Top Bottom