Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Rais wa Burkina Faso ameanzisha viwanda, amewezesha kilimo kuchangia pato la Taifa kwa 30%, amenunua trekta na vifaa vya kisasa vya kilimo lakini pia amejenga nyumba zaidi ya 1000 na kuwapa wananchi wa hali ya chini.
Katika maadhimisho ya wanawake ameonekana akiwa mashambani kisha kufanya majadiliano na wamama wakulima. Ameshusha mishahara ya wanasiasa na kupandisha mishahara ya wafanyakazi wa chini wakiwemo walimu.
Baada ya wanasiasa kuonekana kutoridhika na kushushiwa mishahara amewafuta kazi na kuwapa wanajeshi kazi katika baraza la mawaziri. Amefuta mpango wa manunuzi ya magari ya kifahari na sasa wanasiasa wananunua gari za kawaida kabisa zisizotumia umeme.
Kama haya yamefanyika Burkinafaso penye makundi ya uhalifu kwanini Tanzania na nchi za Afrika zinapendelea kuishi kwa misaada? Hii misaada itatupa uhuru?