Ibrahim Traore ni Gaddafi mpya wa Afrika?

Ibrahim Traore ni Gaddafi mpya wa Afrika?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kama kuna kiongozi Africa aliyekuzwa, kutukuzwa na kusifiwa sana kwa propaganda za kila aina na uongo mwingi sana barani Africa basi ni Muamar Gaddafi. Huyu bwana aliimbiwa sifa zote kiasi kwamba ungeweza kufikiri aliifanya Libya sawa na peponi ila uhalisia ulikuwa ni tofauti kabisa, alipewa sifa za kila aina ikiwemo kuharibu uchumi wa "mabeberu" Marekani kwa kukataa kuuza mafuta kwa $dola!

Bila shaka sasa aliyerithi nyota yake ya propoganda ni huyu kijana wa Burkina Faso, Ibrahim Traore. Kuna ujinga mwingi sana Africa.
Screenshot_20250129-081206_X.jpg


Screenshot_20250129-081333_X.jpg
 
Bila shaka sasa aliyerithi nyota yake ya propoganda ni huyu kijana wa Burkina Faso, Ibrahim Traore. Kuna ujinga mwingi sana Africa.
Sijui kwa nini hakuja Dar kwenye mkutano wa Nishati..

Majuzi tu alienda Ghana kuhudhuria uapisho wa rais mpya, mavazi yake na security detail yake ilikuwa comedy tosha.

Kavaa magwanda, 'mguu wa. kuku' kiunoni, upanga pajani na walinzi kibao waliovaa magwanda, kana kwamba kwenye sherehe ya kuapisha rais jijini Accra hakuna ulinzi.

Halafu mikononi kavaa gloves, anasalimia watu kwa kugonganisha ngumi tu..

View: https://youtu.be/schsRA5aFoc?si=CYvJQnd722Bd9rdg

 
Sijui kwa nini hakuja Dar kwenye mkutano wa Nishati..

Majuzi tu alienda Ghana kuhudhuria uapisho wa rais mpya, mavazi yake na security detail yake ilikuwa comedy tosha.

Kavaa magwanda, 'mguu wa. kuku' kiunoni, upanga pajani na walinzi kibao waliovaa magwanda, kana kwamba kwenye sherehe ya kuapisha rais jijini Accra hakuna ulinzi
Anajua vitu Waafrika wengi
ambo ni akili ndogo wanavyohusudu, kawakamata kwenye PR.
 
Huyo anatafuta kiki tu hana lolote. Katika nchi kama China, Vietnam, Thailand, Singapore, Malaysia na Indonesia kuna viongozi wamewahi kufanya maajabu lakini wala hakuna yowe iliyopigwa.

Shida inapokuja Afrika yaani inakuwa tabu sana na ndio maana hizo swagger waga hazidumu wala kufika mbali. Waafrika ni jamii ya watu wenye kupenda sifa zisizo na maana na ndio maana hata hapa Tanzania ccm ni kelele kibao huku sifa kuu ya nchi hii ni ufisadi mkubwa na ufukara wa wananchi.


View: https://youtube.com/shorts/mEwbeAhzUm4?si=iPPj_lvnYJqc7yS0
 
Vipi Libya ya sasa na ile ya Gaddafi ziko sawa?
Kila mmoja anataka aupate u-Qaddafi mpya.Nchi itatulia kweli hapo?Hakuna kitu hatari zaidi kama kumuonjesha na kumsogeza askari kwenye uongozi ambao fedha zipo usawa wa pua.Akinogewa atagoma kupisha wengine waongoze kiraia.Hapo ndipo utajua afe nani aachwe nani maana yake ni nini!
 
Back
Top Bottom