Ibrahim Traore ni Gaddafi mpya wa Afrika?

Ibrahim Traore ni Gaddafi mpya wa Afrika?

Chagpt yenyewe inasema hivi "During Muammar Gaddafi’s rule (1969–2011), Libya had a relatively high standard of living compared to many other African and Middle Eastern countries. Gaddafi implemented socialist policies that used Libya’s oil wealth to fund public services such as free healthcare, free education, subsidized housing, and interest-free loans. The country also had one of the highest GDP per capita figures in Africa."
Waafrika ni kama vile akili yetu tumeshikiwa na west. Wakisema huyu ni mbaya bai humu watu wanakomaa shingo kuwa ni mbaya hata kama wao wakienda kujifungua wanaambiwa walete pesa wakati wenzao hata operation zisizowezekana kufanyika nchini mwao walikuwa wanasafirishwa kutibiwa nje kwa gharama ya serikali.

True , USA ame destabilize uchumi wa libya kwa sasa hivi Imebaki magofu tu halafu kuna jitu linakwambia aliwahi kuwa kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea , hata ukiangalia wanayoyaita mapinduzi yalifanywa na NATO na kijikundi kidogo cha waasi hawafiki hata 10.
 
Ilo lokole la kupiga mikelele kwenye jua usisumbuke nalo uyo akisikia kuna udongo unauzwa Arusha anakwenda kununua!!!!!
Mambo imani yana uhusiano gn na alichoandka? Mbona kama una chuki na imani za watu wengne kwan imani yako haikamiliki bila kupambana na imani za wengne mkuu au bila kutusi imani za wengne
 
LIBYA ILIKUWA INAENDA KUWA FIRST CLASS COUNTRY
Ada bure kuanzia primary hadi university, matibabu bure, mafuta ya petrol/diesel robo dola kwa lita, usafiri bei rahisi, vijana wasio kuwa na ajira walipewa hela ya kujikimu, Duty free shops....
Kosa la Gadafi likawa kutaka kuunganisha Africa; mabeberu walivyo ona akiunganisha Africa na kuwatoa usingizini .....watakosa raslimali za viwanda vyao; wakaona wamtengenezee zengwe kuwa ni gaidi na Anamiliki Nuclear...BILA USHAHIDI WOWOTE!
Vijana wa Kiafrica walivyo rahisi kuwa manipulate wakahamasishwa na kupewa silaha ili wapigane.....
Sasa hivi wanalia na kusaga meno....
Binadamu tunakawaida ya kukinai,tatizo la viongozi wengi wa Afrika hawapendi kuweka mifumo imara ya uongozi wao wanapenda kuimarisha mifumo ya utawala ili waonekane kama Miunguwatu.
Kama Gaddafi angeweka mifumo imara ya uongozi Libya isingevurugika kama ilivyo leo.
 
Kama kuna kiongozi Africa aliyekuzwa, kutukuzwa na kusifiwa sana kwa propaganda za kila aina na uongo mwingi sana barani Africa basi ni Muamar Gaddafi. Huyu bwana aliimbiwa sifa zote kiasi kwamba ungeweza kufikiri aliifanya Libya sawa na peponi ila uhalisia ulikuwa ni tofauti kabisa, alipewa sifa za kila aina ikiwemo kuharibu uchumi wa "mabeberu" Marekani kwa kukataa kuuza mafuta kwa $dola!

Bila shaka sasa aliyerithi nyota yake ya propoganda ni huyu kijana wa Burkina Faso, Ibrahim Traore. Kuna ujinga mwingi sana Africa.
View attachment 3217287

View attachment 3217288
Ibrahim Traore ni mchawi tu anayebumbabumba.

Tatizo Waafrika wengi wanatapatapa, ni kama wafa maji ambao hata wakiona unywele tu wanaushikilia wasizame.
 
Kwani hata zipokuwa sawa ndio inafanya propaganda na uongo wa kumtukuza Gaddafi kuwa ukweli na uhalisia??
Siku zote ndoa ikivunjika kila mmoja hutafuta mchepuko alioupenda zaidi ili wafunge ndoa. Waafrika wengi ndoa zao (uzalendo) zinategemea wazungu wamesemaje
 
Usimfananishe Traore na Kiongozi wa hovyo kuwahi kutoka Africa aliyeitwa Ghadafi

🔹Huyu Ghadafi ndiye aliyeleta majeshi yake kuja kuua Watanzania wakati wa vita ya Uganda

🔹 Alitaka kuufuta ukristu Afrika ili kuleta u Moja wa Africa Moja yenye dini Moja ya kiislamu.

🔹 Alichochea vikundi vingi vya kigaidi afrika kwa kuvipa vifaa na FEDHA hasa vilivyokuwa na mrengo wa dini yake

🔹 Alikuwa anaingilia chaguzi za ndani za nchi za kiafrika kwa kuwapa FEDHA magari kuwarubuni baadhi ya wagombea njaa wabadilishe dini wafuate dini yake au wakubaliane na ajenda zake za kuongiza sheria na mifumo ya dini yake kwenye serikali

🔹 Misaada aliyokuwa anaitoa Africa mingi ilikuwa ya ujenzi wa misikiti na sio Barbara mahospitali au shule za umma.

🔹 Aliwahi kuudhihaki ukristu kati kati ya itali kwa kuwalipa ma changu na kuwabenesha vitabu vya dini yake kuzunguka mitaani wakiimba kuwa dini yake ndio dini sahihi

🔹 Alitengeneza Taifa la mazezeta kwa kutumia rasilimali za nchi kuwahonga vijana wanaotaka kuoa kuwalipia mahari. Haili lilifanya vijana wawe wajinga , kutokufanya kazi na kumwaachia yeye na familia yake rasilimali zote za nchi azitumie apendavyo. Hovyo kabisa ghadafi
Shida yako ni kwamba unachanganya chuki zako za dini na siasa

Kama Traole ni Muislam na mtoto wako atakuja kuandika comment kama yako kuhusu Traole maana atakuwa tayari ameshalishwa propaganda za uongo kutoka Marekani na Ufaransa kuhusu Traole

Unasemaje kuhusu waasi wa Goma wanaodhaminiwa na Ufaransa na Marekani Ili kuuwa watu na kuiba madini?
 
Kinachoshangaza raia huko Burkina Faso hawalalamiki lakini mashosti wa Ufaransa waliopo Tanganyika wanatoa milio kama wehu.
 
Kijana Acha uongo ndg,kwa Libya hicho unachosikia ni kweli.
Nimekaa wiki 3 yanayosemwa niliweza shuhudia
Hizo wiki 3 ulizokaa huko uliona elimu bure kama Tanzania??
 
Shida yako ni kwamba unachanganya chuki zako za dini na siasa

Kama Traole ni Muislam na mtoto wako atakuja kuandika comment kama yako kuhusu Traole maana atakuwa tayari ameshalishwa propaganda za uongo kutoka Marekani na Ufaransa kuhusu Traole

Unasemaje kuhusu waasi wa Goma wanaodhaminiwa na Ufaransa na Marekani Ili kuuwa watu na kuiba madini?
Soma vizuri kenge wee na uelewe kabla ya kukurupuka kuchangia. Nimempeongeza Taraore na lawama zote nilizoandika hapo ni za Kiongozi wa hovyo kuwahi kutoka Africa aliyeitwa GHADAFI ( Laana tulah)
 
Back
Top Bottom