- Source #1
- View Source #1
Wakuu nimekutana na Taarifa huko mtandaoni inayoeleza kuwa;
"#Kesi inayoikabili Tanzania juu ya mauwaji ya halaiki, rasmi ilianza kusikilizwa kwanzia tarehe 19 January ,na mpaka leo 21 January ambapo muafaka wa majibu yote umetolewa chini ya majaji wa 4 kuhusu swala la Hukumu hiyo, ambapo kila kitu pamoja na ushahidi umeonyesha kuwa ni kweli kila kila kitu kilichotokea siku iyo ya October 19
.
Nukuu: kila yoyote aliye husika katika mauwaji ya halaiki lazima sheria itafata utaratibu mpaka kumkamata lasi hivyo awasili mwenyewe mahakamani. ICC MEMBERS"

- Tunachokijua
- Madai
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Facebook amechapisha taarifa akieleza kuwa Majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wamekti na kati ya tarehe 19 na 21 Januari, 2026 na wamepenga kutoa hukumu ya kesi hiyo siku saba baada ya tarehe 21, Januari.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji wa kina na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Kupitia tovuti yao Mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya ICC katika ratiba yake kwa mwezi January hawakuwa na kesi ya kuhusu mauaji ya Tanzania.
Kupitia kalenda ya ICC inaonesha kuwa mahakama itafungua shughuli zake kwa mwaka 2026, tarehe 27 Januari na tarehe 28 wataendelea na kesi ya Khaled Mohamed Ali Hishri kutoka Libya.
Hata hivyo katika kumbukumbu za mahakama ya ICC kwa mwezi Januari hakuna taarifa kuhusu yaliyotokea Oktoba 2025 nchini Tanzania kujadiliwa na mahakama hiyo.
Ufuatiliaji kwa kutumia google reverse search umebainisha kuwa picha iliyotumika si ya mwaka 2025 na imekuwepo mtandao kuanzia mwaka 2019. Pichani ni aliyekuwa Rais wa mahakama hiyo Jaji Chile Eboe-Osuji Kati ya mwaka 2018 hadi 2021, akiwa katika kikao cha ufunguzi wa mwaka wa mahakama Januri 18, 2019.