Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Afrika ni bara lenye vijana wengi zaidi duniani, huku zaidi ya 60% ya watu wake wakiwa chini ya miaka 25 (UN, 2023). Naija inaongoza, 56.9% ya watu wake wana umri chini ya miaka 18, ikifuatiwa na Uganda yenye 55% (UNICEF, 2024).
Swali ni: Je, idadi hii ya vijana ni fursa au mzigo?
Changamoto ya idadi kubwa ya vijana inakuja na uhitaji mkubwa wa rasilimali kwenye huduma za afya na elimu. Nchi nyingi za Afrika zinatumia zaidi ya 55% ya bajeti za huduma za kijamii kwa vijana, ambao wengi wao bado ni tegemezi (UNICEF, 2022). Ukosefu wa ajira pia ni tatizo, huku 29% ya vijana wakiwa hawana kazi wala elimu (Benki ya Dunia, 2023).
Vijana wa Afrika wanaweza kuwa nguvu kazi kwa nchi zinazokabiliwa na wazee wengi kama Japani (umri wa wastani wa wafanyakazi ni miaka 48) au Ulaya (20-25% ni wazee wenye miaka zaidi ya 65) (OECD, 2024). Afrika inaweza kutoa wafanyakazi wenye ujuzi kwa sekta za teknolojia na viwanda, lakini hii inahitaji uwekezaji katika mafunzo ya kiufundi.
Kuna ulazima wa kuwaandaa vijana na ujuzi unaohitajika kimataifa. Tofauti na India, ambayo inafaulu katika mafunzo ya teknolojia, chini ya 10% ya vijana wa Afrika ndio hupata elimu ya kiufundi (UNESCO, 2023). Uwekezaji dhaifu na miundombinu hafifu pia inazuia maendeleo, huku Afrika ikichangia 2% tu ya mauzo ya viwandani duniani (UNCTAD, 2024).
Njia za Kufanikisha Fursa
Idadi ya vijana wa Afrika ni fursa kubwa ikiwa itaandaliwa vizuri. Bila ya uwekezaji katika elimu za ujuzi shindani kwenye soko la ajira za kimataifa, wingi wa vijana Afrika unaweza kuwa mzigo. Uwekezaji katika ujuzi na miundombinu unaweza kubadilisha vijana wake kuwa nguzo ya maendeleo ya kiuchumi na kuvutia viwanda vingi kuja Afrika kufuta upatikaji wa vijana hao ambao watakuwa kuingia katika uzalishaji wa bidhaa tofauti zinazohitajika duniani kote.