Tetesi: Idadi ya wabunge kupunguzwa

Wafanye yoote wapendayo ila CCM itambue kuwa kuna MWISHO!!

Magufuli ajifurahishe apendavyo ila atambue kuwa “YANA MWISHO”

Hakuna aliyewahi waza Sumaye na Lowassa Leo watakua upinzani!! Hawa watu Magu hawezi zifikia kariba zao hata robo lakini Leo tunaongea lugha moja!!

Muda ndiye hakimu wa yote!!

Nakumbuka riwaya pendwa ya KULI “lakini yana mwisho”


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo la kupunguza idadi ya wabunge si wazo baya; litaokoa fedha nyingi na labda linaweza kulazimisha mabadiliko ya utendaji wa Bunge hilo. Jambo la kwanza ni kuondoa wabunge wa viti maalum. Hawana wanayemwakilisha ambaye hawakilishwi na mbunge wa jimbo.
 
Lowasa alitegemewa awamu ya pili ya kikwete ilikuwa aondoke. Kila ishara zilituonyesha anaondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena waliona katiba mpya na tume huru haziwahusu wananchi walipopigia kelele walijiona wako Salama japo walikuwa na nafasi ya kushinikiza mabadiliko,Leo wanatamani mabadiliko kuliko hata MTU yeyote.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa hawa ndiyo wanaongeza mikoa kila kukicha matokeo yake kuongeza majimbo na hivyo idadi ya Wabunge.

Kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa kwa makusanyo ya kodi na baadhi ya nchi za wafadhili kusimamisha misaada yao serikali inaanza mikakati na kupunguza wabunge, haitoshi tu kupumguza wabunge ili kukabiliana na hizi issues mbili bali pia fagio la chuma serikalini halikwepeki kwa at least 25% or higher.

Matokeo ya kumsukumizia kichaa Ikulu.

 
Mbona uzi wako umekaa kishabiki sana mkuu
 
Tena waliona katiba mpya na tume huru haziwahusu wananchi walipopigia kelele walijiona wako Salama japo walikuwa na nafasi ya kushinikiza mabadiliko,Leo wanatamani mabadiliko kuliko hata MTU yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtandao wa Lowassa ndio ulituletea katiba pendekezwa lkn huyo huyo Lowassa Leo anaitamani katiba ya Warioba! Ni vizuri Magufuli ajifunze.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani tabu ni nini??

Si wapinzani wa merge na wapinzani wenzao

Na CCM wamerge na CCM wenzao


kuunganisha watu wenye itikadi tofauti ni UPUMBAVU
 
Mawaziri na washauri wa Rais ndio wangepunguzwa ...hawana lolote wanalofanya zaidi ya kutumbua hela za walipa kodi
 
Waanze kuwaondoa wanaoitwa "Wabunge wa viti maalum" inamaana wanawakilisha viti maalum au wananchi? Watolewe kwakuwa hakuna wanaowawakilisha.

Pili kusiwepo na wakuu wa wilaya as long as kuna Wabunge, Wakurugenzi watendaji na pia kuna makatibu tawala mkoa na wakuu wa mikoa pia.

Utumiaji mbaya wa pesa za walipa kodi kulipa mishahara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…