Idadi ya Wanaume duniani ni kubwa zaidi kuliko ya wanawake

Idadi ya Wanaume duniani ni kubwa zaidi kuliko ya wanawake

Hii ni taarifa maalum kwenu wadada wote mliojikatia tamaa kwamba hamuwezi kuolewa kisa wanaume ni wachache kuliko wanawake.

Ni wakati sasa wa kuachana na huzuni kisa umekosa mwanaume wa kukuoa. Ukweli ni kwamba wanaume ni wengi kuliko wanawake.

Ikiwa kuna idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume katika eneo au nchi yako, hiyo haioneshi ukweli wa kimataifa. Kwa idadi kubwa kama hii duniani ya wanadamu 8,118,835,999, kulingana na takwimu, Wanaume : wanawake = 1 : 1.

Kuna wastani wa..
wanaume 4,079, 164,815 na wanawake 4,039,671, 184 duniani. Hii inawasilisha 50.24% ya wanaume na 49.76% ya wanawake kwa idadi ya watu duniani. (U. N World Population Prospects 2024).

Katika nchi kama China, India, Saudi Arabia, UAE na Oman, wanaume ni wengi kidogo kuliko wanawake. Katika nchi nyingi za Ulaya Mashariki na Afrika Kusini mwa jangwani la Sahara wanawake ni wachache zaidi kuliko wanaume.

Uwiano wa asili wakati wa kuzaliwa kwa wavulana : wasichana = 107 : 100
Lakini wanaume wana muda mfupi wa kuishi kutokana na sababu mbalimbali za kijamii. Hivyo basi ikiwa wewe ni bachelor tambua kuwa maisha ni mafupi hivyo ni vyema ukajipatia popote duniani mwenza wako mapema kabla hajafa.

NB tunaishi katika global village unaweza kujipatia mwenza wa kukuoa popote pale duniani, wanaume ni wengi sana.

Ubarikiwe.
😂😂😂 kama kweli
 
Takwimu za kupika ,hapa nilipo naangalia ..Ofisini mwaka jana watu kama saba walipata watato ila wawili tu ndio wamepata wa kiume... Ukweli mchungu wanawake ni wengi nenda hospital pale kaangalie uone ..
Kwahiyo tafiti za ofisini kwako tu ndio umeshafikia hitimisho? Tuna watanzania wajinga sana. Note this, kwakawaida mtoto wakiume ana nafasi kubwa yabkuzaliwa kuliko wa kiume, omba takwimu za uzao Tanzania utakuta watoto wanazaliwa wengi Ni wakiume kuliko wa kike. Probability ya kuzaliwa mtoto wa kike Ni siku ya 11, 12, wakati wakiume Ni siku 13,14,15,16. ,, wanawake wanatuzidi kwenye miaka ya kuishi tu ndio maana ukiangalia kwenye sensa utakuta watoto wengi na vijana niwakiume lakini Wazee wengi Ni wanawake
 
Kuna wastani wa..
wanaume 4,079, 164,815 na wanawake 4,039,671, 184 duniani. Hii inawasilisha 50.24% ya wanaume na 49.76% ya wanawake kwa idadi ya watu duniani. (U. N World Population Prospects 2024).
  1. Kuna kundi halioi ila ni dungadunga sana halafu linashika clean books
  2. Tusaidie child population ratio kiume na kike
 
Takwimu za kupika ,hapa nilipo naangalia ..Ofisini mwaka jana watu kama saba walipata watato ila wawili tu ndio wamepata wa kiume... Ukweli mchungu wanawake ni wengi nenda hospital pale kaangalie uone ..
angalia mambo globally.

mleta mada katumia neno global village
 
Back
Top Bottom