Tetesi: Idara kuwa 6 na Vitengo 2 tu

LGAs zote hazifanani katika umhimu wa sekta. Mafia kwa kilimo na mifugo ni tofauti na Geita.
LGAs zingependekeza idara wanazohitaji na kushauriana na PoRalg.
LGAs siyo idara za central government., wala siyo chombo chake.
 
Ifanyike hivyo na mishahara itelemshwe wasiopenda washafishwe Kama ma Ras na Makatibu wakuu huu ni mzigo mkubwa na watakaobaki mishahara yao iwe reasonable sasa hivi hw kuna wanaoishi peponi na mashetani inavunja sana mioyo
 

Idara ni zaidi ya mkuu wa idara; kuna katibu mhutasi, wahudumu wa ofisi nk. Hawa watapelekwa halmashauri kukusanya mapato.......ni maoni yangu
 
Kuwa na watu wengi ambao kazi yao ingeweza kufanywa na MTU mmoja ni Bonge LA Hasara.....hii nzuriiiii
 
Hakuna mtu atapoteza ajira bali wata hamishiwa kwenye vitengo vingine? Hivi unajua sheria za utumishi wa Umma? Kama mgelikuwa mna msikiliza waziri wa tamisemi bungeni wala msingalisema haya hili jambo halikuanza kuongelewa leo!
Tungemsikilizia wapi wakati walikua gizani?
 
Hakuna mtu atapoteza ajira bali wata hamishiwa kwenye vitengo vingine? Hivi unajua sheria za utumishi wa Umma? Kama mgelikuwa mna msikiliza waziri wa tamisemi bungeni wala msingalisema haya hili jambo halikuanza kuongelewa leo!
Tungemsikiliza vipi wakati mlizima TV mkaendesha bunge gizani! Tunataka bunge live.
 
Na tunakoelea, serikalini wataanza kufanya kazi kwa kpi kama private sectors
Target haijawa achieved unapenalaiziwa
 
Awamu hii wengi tunaisoma namba, wakuu wa Idara wengi walikuwa wapo upande wa chama Tawala kipindi cha uchaguzi kwa kujua kuwa wapo salama sasa imewageukia.
Hii mkuu wacha ije tu kwa kweli nilikuwa nakasirika sana unalikuta pumbavu likuu la idara eti linashabikia ujinga wa ccm! Sasa wacha yaisome namba, ila nashindwa kuelewa ufanisi utakuwaje maana mtu aliyesoma ushirika akawe mkuu wa idara ya kilimo, mifugo, uvivu, umwagiliaji na ushirika sijui itakuwaje aiseee!
 
Safi sana watu tufanye kazi Massa 8 kihalali lzm uchoke sio unakaa unajizungusha tu kwny kiti unasubiri kusaina vocha safari hii hapa kazi tu.
 
Kuna sababu gani ya kuweka idara ya maji n.a. miundombinu?
 
Lakini kwanini kubana matumizi imekuwa kwenye Local Gvt tu, Wakuu wa Wilaya na teuzi za Ma DAS mbna zinaendelea na hizi ndio nafasi za kisiasa? Sitting allowance imefutwa Halmashauri tu, Wabunge na wengineo wanaendelea kuchukua posho hizo, kwa huyu jamaa dhana yake ya kubana matumizi inatuhusu watumishi wa hali ya chini kada za juu hatagusa.
 
Kupunguza tu hakuwezi kuwa na solution ya kudumu,swala la msingi ni kuwa na Idara na vitengo kutegemea mahitaji ya Halimashauri husika,ili kuepusha kuwa na mtumishi ambaye ni useless.Kwa mfano mahitaji ya unjinia wa maji yapo zaidi kwenye halimashauri za wilaya ambako maji husimamiwa n halimashauri,wakati kwenye halimashauri za majiji,manispaa na miji maji husimamiwa na mamlaka za maji ambazo zipo kisheria
Halimashauri kama ya Ilala haina haja ya afisa kilimo,etc

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…