Idea 3 za Biashara zinazoenda kuniweka kundi la Milionea by 2025

Mawazo mazuri;
Naungana na wewe lkn kuna uchochoro fulani wa pesa ukifanikiwa kuwekeza kwenye uvuvi utapiga pesa zaidi.

Nunua fibre boat, nunua engine horse power 15, tafuta mpemba mpe mashine, awe anabeba wavuvi kwenda kuvua, kazi ifayike pwani ya Dar!
Utanishukuru baadae!!
 
Good idea.
Mimi umilionea niliuotea hivi.
Nilifungua DUKA LA UWAKALA WA LINE ZOTE KATIKA ENEO LA MPAKA WA KENYA NA TZ.
THEN NIKAWEKA MTAJI WA MILLION 15.
NIKATAFUTA LINE ZA KENYA ZA SAFARICOM MPESA.
KISHA NIKATAFUTA KUWA WAKALA WA BENKI.. CRDB WAKALA NA NMB NA NBC KWA TANZANIA.
THEN KWA KENYA NKAPATA UWAKALA WA BENKI YA EQUITY BANK NA KCB BANK.

Hapa nikawa nimepata access ya kuwa foreign exchange agency kwa sababu wateja wangu wengi walikuwa ni wasafiri na wafanyabishara wanaoutumia bandari ya Mombasa na kuchukua mzigo Nairobi. Mara zote wanapokuja kwangu huitaji kutoa voda mpesa then niwapatie ya kenya kuepuka usumbufu.
Kupitia tu hapa kwa siku nikawa nalaza hadi laki 6 faida.

Baada ya wateja kuniamini wakawa wananitumia fedha zao wakiwa mikoani (arusha, Dodoma, iringa) then mimi ninawatumia wauazaji wa mizigo yao.

Ukiwa mpakani utakuwa na wateja tofauti tofauti ni wewe tu kuwa muaminifu.
1. Wauzaji wa mirungi (kumbuka mrungi kenya huwà ni legal so wewe kama wakala mwenye access na uwakala wa nchi mbili unachokifanya ni kutakatisha fedha zao coz haziwezi kuwafikia directly so muuza mrungi wa TZ atakutumia wewe wakala kupitia line ya wakala mwingine kama float then wewe utamtumia muuzaji wa kenya wa mrungi kupitia mpesa safaricom).

2. Ukiwa mpakani pia unakuwa na access ya kuwa wakala wa CLEARING AGENCY, INSURANCE ETC.
 
Mkuu hongera sana...30M ni pesa ndefu sana ukiipangilia...mi nipo kwenye biashara muda mrefu sasa tokea 2014...
Komaa na car accessory naona haina stress tena ukikaa mwenyewe ili ujue wateja wanapenda nn utatoboa...hayo ya service (barbershop) achana nayo kwanza maana itabidi uwalinde vinyozi na dada wa kuosha...biashara ambayo buku inazalishwa na mtu zaidi ya mmoja ni stress kwa kuanzia...kinyozi akihama anaongoka na wateja...unless otherwise una uzoefu nayo..
Hiyo ya toyota coaster inakusumbua we ingia front kwenye car accessory ukipambana nayo hela utaiona...siku hizi mtu akinunua gari anataka radio ya android,rims poa,unyunyu,tinted na vitu vingine...
Ukipata eneo poa ambalo unaweza park gari angalau 2 za wateja maana mtu akija lazima uwe na sehemu ya kupimp na fundi wako mzoefu...
 
Biashara hiyo nadhani inalipa ila shida ni kuwapata wavuvi waaminifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…