Mwalisu junior
New Member
- Nov 11, 2022
- 3
- 4
Aiseh Mwanza kuna mkate unaitwa tiktok...mkate ule ni grade A, yan unaweza kula bila chai bila blueband...ni mytaaaaaamu sanaUganda mbona mbali sana, Zamani Arusha walikua vizuri sana lakini IRINGA kwa mikate Tanzania nzima hawana mpinzani wana kitu cha Tosti hatari tupu, Dar hakuna mkate mzuri tunateseka tu
Mimi pia ni kinyozi ila nipo south Africa kwasasa,mapema mwakani nami ninatarajia kurudi nyumbani kuanza na hii biashara InshaAllahNipo kwenye utekelezaji wa idea namba Moja hapo mwenye frem kanipa mwezi huu wote wa kuweka vitu sawa.
Kuna mkate wa Kenya Super loafAiseh Mwanza kuna mkate unaitwa tiktok...mkate ule ni grade A, yan unaweza kula bila chai bila blueband...ni mytaaaaaamu sana
Safi mkuu umetoa wazo zuri sanaKama uko Dar, bakery usiiache mbali kwa sabab nimeona dar badala ya kulishwa mikate wanalishwa sponji. Kwa case study kula mikate ya uganda ndo utaona maana ya kuongeza thamani.
Usisahau baada ya corona watu wametambua umuhim wa kula kw afya, hivyo weka na mashine ya kutengeneza mkate wenye mboga za majan na matunda na ingredients nyingine zinazoongeza kinga ya mwili.
Ukiachilia watu binafs una soko kubwa la taasisi za serkali na binafs kupitia bajet ya hospitality!
Kama we sio muislam fikiria hata kiwanda cha GIN spirits na Vodka inalipa ukijua marketing na wateja ni wapi.
kila la heri.
NAPENDA NENO KUFANIKIWA HATA KAMA MFAIDIKA NI MWINGINE!
Pesa inazaa pesa. Naikubali sana hii biashara.Good idea.
Mimi umilionea niliuotea hivi.
Nilifungua DUKA LA UWAKALA WA LINE ZOTE KATIKA ENEO LA MPAKA WA KENYA NA TZ.
THEN NIKAWEKA MTAJI WA MILLION 15.
NIKATAFUTA LINE ZA KENYA ZA SAFARICOM MPESA.
KISHA NIKATAFUTA KUWA WAKALA WA BENKI.. CRDB WAKALA NA NMB NA NBC KWA TANZANIA.
THEN KWA KENYA NKAPATA UWAKALA WA BENKI YA EQUITY BANK NA KCB BANK
Hahaha hizo Biashara za msimu , walevi wakifunguliwa chimbo jipya wote wanahamaHizi biashara zinaweza kukufilisi vile vile, mi bado napambana saving angalau ifike 30m..
Akili inaniambia hela ipo kwenye night club/lounge au barbershop
Mkuu angalia vzr Uchambuzi yakinifu wako, Barbershop (Modern & Executive) - 13M ni ndogo saana. Hiyo hata vifaa tu unaweza usipate achilia mbali kodi ya pango, ukaranati, usajiri wa vinyozi (lazima utafte kinyozi bora na mwenye wateja), nk nk nkHabari Wakuu!
Sio kila mtu kwake mtaji ni tatizo, wengi wetu tuna pesa ndefu kiasi tu kwenye Acc, (20M+50M).
Personal, nilipanga kuanza kuwekeza kwenye biashara kwa Capital ya 30M, ambapo nashukuru mtandao wa JamiiForums chini ya Maxence Melo hatimaye nimeweza kuvuna idea 3 muhimu kupitia thread za humu JF.
Kwa miezi 2 nilijikita kufanya tafiti ya thread za zamani na mpya kuhusu aina ya uwekezaji naoweza kufanya kwa kiasi tajwa maxmum 30M. Ila busara ikanituma hiyo hela niwekeze kwenye biashara 2 tofauti kuliko kuwekeza mtaji wote kwenye single business ambapo ni risk.
Hivyo nimeamua rasmi kuwekeza kwenye biashara hizi,
1. Car accessories - 15M
2. Barbershop (Modern & Executive) - 13M
Idea iliyo pending mpaka sasa ni Bakery factory (Uokaji mikate), ambapo hii nitaanza baada ya hizo business 2 hapo juu kutake off.
Hali kadhalika, hizo business 2 nimeziweka kwa phase kiutekelezaji kwa miezi 3 kabla ya kuhamia uwekezaji mwingine. Hii yote ni control mechanism pia kuweka concentration ili kukuza biashara.
Nimeanza na bishara hizo sababu kwangu mimi zina low risk ya kupoteza mtaji pia hata margin profit yake ni nzuri, pia kwa kiusimamizi hazisumbui sana.
Asante JF, see you at the top.
Iyo biashar upate nahodha muaminifu tu otherwise huna njia ya kuwabana. utawabana vp wakat ww huingii kweny chombo ukaenda kuvua ? Kaz yako ww ni kukaa juu ukaletewa hela za mauzo waliyovua tu bcWabane wakose mianya ya kuiba, tena kwenye hiyo biashara mmiliki wa boti kuibiwa ni uzembe wako tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hongera sana...30M ni pesa ndefu sana ukiipangilia...mi nipo kwenye biashara muda mrefu sasa tokea 2014...
Komaa na car accessory naona haina stress tena ukikaa mwenyewe ili ujue wateja wanapenda nn utatoboa...hayo ya service (barbershop) achana nayo kwanza maana itabidi uwalinde vinyozi na dada wa kuosha...biashara ambayo buku inazalishwa na mtu zaidi ya mmoja ni stress kwa kuanzia...kinyozi akihama anaongoka na wateja...unless otherwise una uzoefu nayo..
Hiyo ya toyota coaster inakusumbua we ingia front kwenye car accessory ukipambana nayo hela utaiona...siku hizi mtu akinunua gari anataka radio ya android,rims poa,unyunyu,tinted na vitu vingine...
Ukipata eneo poa ambalo unaweza park gari angalau 2 za wateja maana mtu akija lazima uwe na sehemu ya kupimp na fundi wako mzoefu...
hata car wash ukipata sehemu nzuri pia inakulipa mkuu
Kweli kuna muda unaangalia viwanja vilivyokuwa vinajaza vilivyokimbiwa mpka unakata tamaa, ila bado kuna watu wanamantain.Hahaha hizo Biashara za msimu , walevi wakifunguliwa chimbo jipya wote wanahama
Kweli maana kupata sehem ya kueleweka kodi inaweza cheza laki 7 mpka milionMkuu angalia vzr Uchambuzi yakinifu wako, Barbershop (Modern & Executive) - 13M ni ndogo saana. Hiyo hata vifaa tu unaweza usipate achilia mbali kodi ya pango, ukaranati, usajiri wa vinyozi (lazima utafte kinyozi bora na mwenye wateja), nk nk nk
Mimi pia ni kinyozi ila nipo south Africa kwasasa,mapema mwakani nami ninatarajia kurudi nyumbani kuanza na hii biashara InshaAllah
Kaka nami ni mtanzania narudi nyumbani[emoji23]Baki huko huko mkuu sisi huku tupo milioni 60 tunatosha [emoji276]
Issue sio kupata nahodha muzuri, kwenye huo msafara wa kwenda kuvua basi hakikisha anakuwapo mtu wako mmoja mwenye akili na mwaminifu, kuibiwa itakuwa ngumu sana. Mimi nimeifanya hiyo business pale Mwanza miaka fulani.Iyo biashar upate nahodha muaminifu tu otherwise huna njia ya kuwabana. utawabana vp wakat ww huingii kweny chombo ukaenda kuvua ? Kaz yako ww ni kukaa juu ukaletewa hela za mauzo waliyovua tu bc
Hiyo ya Night Club kama hujawahi kuifanya utafilisika,hiyo ina usumbufu wa polisi kukufuatilia kila siku na inabidi uwe unawapa hela kila siku ili kuwatuliza na usipowapa wanavamia kila siku wateja wanapachukia panakosa mvutoHizi biashara zinaweza kukufilisi vile vile, mi bado napambana saving angalau ifike 30m..
Akili inaniambia hela ipo kwenye night club/lounge au barbershop
Umemwambia ukweli mtupu Mimi napata shida hiiHiyo ya Night Club kama hujawahi kuifanya utafilisika,hiyo ina usumbufu wa polisi kukufuatilia kila siku na inabidi uwe unawapa hela kila siku ili kuwatuliza na usipowapa wanavamia kila siku wateja wanapachukia panakosa mvuto