Idea mbalimbali za biashara kwa wenye mitaji mikubwa kuanzia Milioni 100 hadi 500

Hii haina maana mkuu, usitake kumjua mtu bali taka kupata mawazo yake ya kiuwekezaji na kimaendeleo ili ufaidike kama anavyofaidika
Ushasema wanapita kimya kimya mawazo yake utayapataje.

Humu jf hamna mwenye mpunga huo kama yupo invite him/her
 
Ahsante.

Huwa ninafuatilia mambo ya biofuel ndio maana.
 
Duh..
 
Yeah pamoja na majibu mengi kwa mtoa post..nadhani watu wamezoea mawazo madogo madogo ya kurisk pesa kiasi. Nijuavyo hata yale mawazo madogo yanaweza kuwa magnified kwa kutumia mtaji mkubwa wa kuanzia hiyo amount taja na hata zaidi.
NYONGEZA yangu ni kuwa IDEA yoyote kubwa ni vema kuingia gharama kidogo ya kufanya UPEMBUZI YAKINIFU ili wazo husika lipate JUSTIFICATIONS za uhalisia kitaalamu. Nashauri wenye mitaji mikubwa mawazo yapo ila wawekeze pia kwenye ushauri na maarifa ili kupunguza risks au kumanage risks na kuleta tija tarajiwa.
 
Kweli kibongo bongo 100m ni nyingi sana ila wapo wenye nazo na zaidi humu humu
Leteni idea acheni kupiga ramli
Mtu kauliza idea za over 100
Mbona zipo nyingi tu ingawa sio hela kubwa sana hiyo
Kama nyumba moja inasimama kwa bei hiyo na sio kali hivyo basi 100 wapo wengi wenye nayo ila acheni kujishusha

Kama mtu hana ni yeye
 
Kweli mkuu tunajishusha sana ..na ndio mana kimaisha bado tuna maisha magumu ya kuona ni haki yetu na sawa kuishi maishaa ya kimasikini.
 
Mkuu ukiwa na 100m ukaweka bond za serikali
Faida ippoje ukikokotoa
 
Kweli mkuu tunajishusha sana ..na ndio mana kimaisha bado tuna maisha magumu ya kuona ni haki yetu na sawa kuishi maishaa ya kimasikini.
Halafu wapiga ramli kibao humu na hata wachawi pia
Umasikini Walahi mbaya sana unamfanya mtu awe mchawi na hasidi kabisa

Kila mmoja anaweza kupambana akazipata ila kama mtu anapoteza kwa mfano masaa 6 kwa siku kukaa tu sehemu akiongea pumba basi ndio hawa hawa wanaopinga kuwa hakuna mwenye 100m humu
Hii hii mia ninayoijua mimi
 
Hili ndio lile swali "mfano ukiokota miliion mia (100ml) utazifanyia nini?
 
Mkuu ukiwa na 100m ukaweka bond za serikali
Faida ippoje ukikokotoa

Inategemea na asilimia ya faida siku anayonunua, say kama ni 13% kwa mwaka maana yake aliweka 100m maana yake anakunja 1.3m kila mwezi chukulia ana mshahara au ana biashara zingine! Ni ndogo kwa mfanyabishara (assuming that %ge) ila kwa mtu muoga na anayetunza pesa zake inamtosha sana anaona!
 
Wekeza baharini, nunua meli ndogo ya uvuvi au mizigo. Kwa zilizotumika nchini Ugiriki na Cyprus unapata kuanzia 250million.

Meli ya mizigo route ya Dar kwenda Comoro mizigo ni mingi sana.Pia unaweza ukaleta meli ya kubeba mifugo (Livestock Carrier) kutoka Tanzania kwenda Comoro.
 
Sasa mtu hapo alipo nyuma ya keyboard hata lunch hajapata unamuuliza idea ya 100mil

Mtu akishaziokota ndio atajua azifanyeje halafu sasa ndio mtoa mada amuulize ulizifanyia nini hizo milion 100
Mkuu mbona kuna mawaziri na wabunge humu?
Kuna wafanyabiashara wenye nazo hizo, wapo wa nje pia ambao ni mshahara wa mwaka huo
Ila ni walala hoi wamejaa sana lakini idea zote zimekuja kwa kubuni tu sio lazima hela bali mawazo tu

Kuna makampuni Ulaya kama bright ideas
Unawaandikia idea yako na unalipa kiasi kidogo tu kama haipo duniani umeula
 
Mkuu njooo tuwekeze kwenye biashara ya majeneza inalipa sana hautojuta!
 
Biashara yoyote unaweza kuifanya kwa mtaji wowote ni inshu ya diversification tu hata kuuza karanga unaweza kukufanya kwa mtaji wa bilion

Mimi mwenyewe nauza mitumba kwa mtaji wa 800mil
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…