Nnajibu kwa kirefu kwa faida ya wote tu sio personal.
Sina experience ya kuwa na hela mingi ila najua mambo mawili matatu kuhusiana na Akili, Afya na Utajiri.
1. Unaweza kujidanganya kuwa, kuwa na Akili ni ile hali ya mtu kuwa na maarifa mengi lakini ukweli ninkwamba ni hali ya kuyatafuta maarifa. Curiosity. Udadisi ndio akili. Ni kitu endelevu na ndio maana ni rahisi kumkuta anayeitwa 'mwenye akili' anahangaika na makala, documentary, maktaba na maabara kila siku KUYATAFUTA MAARIFA.
2. Kwa ishu ya Afya pia, ni mara zote utakuta mwenye afya ndiye aliye bize kuitafuta afya kila siku. Utamuona yupo kwenye mazoezi, mara yupo kule anaandaa chakula bora. Ametulia kidogo unamsikia analeta stori za kunywa maji, na jinsi anazikata lita ngapi sijui kila siku!! Huyo ndiyo MWENYE AFYA, kazi yake ni KUIJENGA AFYA kila siku.
3. Tukija kwenye Utajiri nacho ni kitu hichohicho. Tajiri ni mtu mwenye kuutafuta utajiri bila kukoma. Ndio maana bilionea kumsikia yupo anawekeza tena mradi wa kuchakata sijui nini ili apige pesa ni kawaida kabisa maana utajiri ni UTAFUTAJI WA MALI ENDELEVU. Utajiri unatunzwa vizuri kwa kutoa huduma au hiyo bidhaa kwa watu wengi zaidi. Ukiurithi utajiri tambua umerithi JUKUMU, ukilikataa jukumu wewe ni tajiri NO MORE!.
Ni akili ya asiye na afya kusema, si umeshakuwa fit bro acha kujihangaisha na mazoezi. Ni akili ya asiye na akili kusema nishasoma sana sasa nimeelewa kila kitu nina maarifa na akili ya kutosha napumzika nizitumie. Pia ni akili ya masikini kusema sasa ndugu ushapata mali ya kutosha, acha kutafuta hela uanze kuzitumia.