IDF Jeshi bora kabisa duniani na MOSSAD idara bora zaidi ya ujasusi duniani!

Smart...
Sijui umetumia vigezo vipi kusema Marekani ikiingia vitani ni Iran itashinda vita.
Marekani walishindwa vita na Vietnam 1975.

Kipi kitakachowafanya washinde vita na Iran?

Kuhusu vita vya Israel na Iran Mungu apishie mbali madhara yake yatakuwa makubwa sana.

Israel haiwezi kuhimili vita vya muda mrefu hata kama itasaidiwa na Marekani.
 
Ethiopia hawakutawaliwa na mkoloni, unawezaje kusema sio jeshi bora?
 
Nelson...
RankCountryPower Index
1United States0.0606
2Russia0.0681
3China0.0691
4India0.0953
5Japan0.1501
6South Korea0.1509
7France0.1702
8United Kingdom0.1717
9Egypt0.1872
10Brazil0.1988
11Turkey0.2098
12Italy0.2111
13Germany0.2186
14Iran (Islamic Republic of)0.2191
15Pakistan (Islamic Republic of)0.2364
16Indonesia0.2544
17Saudi Arabia0.3034
18Israel
Source: Ranked: Military Strength of Nations, 2020 (Comparing Global Armed Forces) - CEOWORLD magazine
 
Hilo ni jambo gumu inaweza kuleta vita ya tatu ya dunia kwanini?Israel inalindwa western countries ikiongozwa na US pili kidini wana wafuasi ambao wataenda kutetea nchi yao ya ahadi kwa damu na moyo wote...Kwa upande wa Iran wana pata support kwa nchi kama Russia china pia North korea ana weza kuingilia hivi vita lakini waumini Kishia popote duniani wana weza kuingia kuipigania Iran kumbuka Iran kijeshi yupo yupo vizuri sana sambamba na Israel...Kwa upande wa pili ambalo dunia ina ogopa ni matumizi ya nyuklia kwa pande zote mbili....Lakini Israel kikwazo chake kikubwa ni Iran hili kuitawala middle east kwa usalama wa haya mataifa mawili ni kuishi kwa chokochoko zisizo na madhara makubwa...
 
nadhani nakuelewa vizuri sana, wangekuwa tu na uwezo wa kiuchumi kama marekani au china au urusi wangekuwa hatari sana, na kipato kinawanyima fursa kadhaa za kutumia akili zao zaidi. Binafsi naona pia ni jambo jema huenda wengejiona sana, na huenda usalama wa majirani zao ungekuwa shakani zaidi, Mungu hakupi vyote.
 
Plumber...
Katika kitabu hicho hapo chini katika Epilogue yaani Jumuisho waandishi wanaeleza kuwa Israel inataka sana Marekani ipigane na Iran.

Waandishi wanahitimisha kwa kusema kuwa Israel bila msaada wa Marekani hawaiwezi Iran.

 
Mzee wangu Mohamed Said, ni maoni yangu kua Marekani atashinda vita dhidi ya Iran, na itakua vita ya upande mmoja kama ilivyo kwa Urusi na Ukraine. Ninazo sababu zifuatazo.

- Marekani ana uchumi imara. Anaweza kumudu kuendesha vita kwa muda mrefu na taifa lolote hapa duniani. Meanwhile, uchumi wa Iran sio imara. Na hauwezi kumudu vita vya muda mrefu.

- Silaha. Marekani ni taifa la pili kwa idadi ya nuclear warheads duniani. Maelfu ya ndege vita, vifaru, battleships, na mifumo imara ya ulinzi wa anga. Iran hana aircraft carrier hata moja, wakati marekani anazo 11. Nikiangalia n nguvu kazi ya kijeshi, naona Marekani yuko mbali sana kumzidi Iran.

- Washirika. Marekani anao washirika wengi zaidi na wenye nguvu kumzidi Iran. Kwa sasa Marekani amekua na vibaraka hadi kwenye nchi jirani ya Iran, kitu ambacho ni kinyume kwa upande wa Iran. Pia Iran amekua na migogoro na majirani zake, kitu kinachompa adui faida dhidi yake.

- Geographical advantage. Marekani na Iran wako mbali kijiografia. Lakini kijeshi, Marekani yuko karibu sana na Iran wakati Iran yuko mbali sana na Marekani. Hapa naongelea wingi wa military bases za Marekani zilizoko hapo mashariki ya kati. Hizi zinamuwezesha Marekani kumshambulia Iran kutokea karibu kabisa, wakati Iran atatumia umbali mrefu sana kumshambulia Marekani kwa sababu hana military base iliyoko karibu na Marekani.

Kwa uchache kabisa, haya yananifanya niamini Marekani atashinda vita kirahisi dhidi ya Iran.
 
Upo sahii kaka
 
Upo sahii kaka
 
Hizo ni data tu mzee wangu kwenye uwanja wa mapambano ni uhalisia!!!!Wanajeshi hawaishi kwa data bali wanaishi kwa uhalisia wa kinachotea mstari wa mbele kwenye eneo husika na ushiriki wa mapambano!!!!Taasisi yoyote inaweza kutoa data sikupingi mzee wangu
 
Smart...
Hakika hizo ni hoja nzito sana.
Hebu nielimishe ilikuwaje Marekani akashindwa Vietnam?
 
Kikwazo itakuwa israel kwa sababu mpaka sasa dunia haina kinga yoyote ya kuzuia bomu la nyuklia kwa mujibu wa US Iran anazo na pia Israel anazo hii itakuwa sio vita tena ya pande mbili bali ya dunia nzima..Kwa mantiki hiyo hiyo vita haiwezi kutokea kati ya Iran na Marekani...
 
Nelson...
Ulikuwa unayajua haya?
Mimi yamenishtua sana.

Inaelekea hukupendezwa na ukweli huu.

Nelson jifunze kuandika vizuri.
Usiweke !!!

Si kama ukifata ninachokufunza utakuwa umedhalilika.

Hapana sote tumefunzwa na watu pale tulipokuwa hatujui.

Nakuambia hivi kwa kuwa unasomwa na watu na haifai utoe picha ya mtu asiejua kuandika vizuri.

Wataitilia shaka elimu yako.
 
Smart...
Hakika hizo ni hoja nzito sana.
Hebu nielimishe ilikuwaje Marekani akashindwa Vietnam?
Mzee Mohamed Said, kwanza kabisa naamini unafahamu kua USA Vs Vietnam haikuwa full-scale war. USA alifanya mashambulizi na kuisupport kijeshi Vietnam kusini dhidi ya Vietnam kaskazini.

Mpaka hapo, tofauti inaonekana kua nguvu inayotumika kwenye full-scale war ni tofauti na nguvu inayotumika kwenye hizi military operations. USA alikua na silaha za nyuklia wakati wa vita ya Vietnam, lakini hakuzitumia. Ni kama military operation ya Urusi pale Ukraine, nguvu anayoitumia Urusi ni kiasi kidogo kulinganisha na uwezo wake halisi.

Aidha, kuna mambo kadhaa yaliyochangia Marekani kushindwa vita ya Vietnam.

- Mgawanyiko baina ya wamarekani. Raia wengi wa Marekani hawakuona umuhimu wa hii vita. Wamarekani wengi waliipinga hii vita . Joto la cold war halikuwapata wamarekani wote, kwahiyo upinzani wa Marekani kwenye vita ukaanzia hapohapo Marekani kwa raia wake wenyewe.

- Upande wa mbinu za kimedani, Marekani alikua anapambana na vikundi vidogo vidogo vya wapiganaji wa msituni, ambavyo vilikua vikijificha kwenye mapori manene na kufanya guerilla attacks. Wamarekani hawakua na uzoefu wa mapambano ya namna hii. Kiufupi, ilikua rahisi kwa hivi vikundi kuwashambulia wamarekani, kuliko wamarekani kuwashambulia hawa wapiganaji wa Vietnam.

- lakini pia, Marekani alikua "invading force", wakati Vietnam ilikua inapambana kuilinda ardhi yake. Hapa morali ya upiganaji lazima iwe tofauti.


Naamini mzee wangu Mohamed Said unaiona tofauti kubwa iliyopo kati ya Vietnam na Iran.

Badala ya kupigana na un-industrialized country, inayotumia guerilla tactics, this time atakua anapigana na industrialized country tena ya miji ya kueleweka. It's going to be a direct war, na sio mapigano ya kujificha. Badala ya kutupa mabomu porini ambamo haijulikani kuna watu wangapi, mabomu yatashushwa kwenye miji kama Tehran iliyobeba miundombinu muhimu ya adui.

Lakini pia this time, Marekani atakua anapambana na real threat, adui anaeweza kushambulia badala ya adui anaejilinda pekee. Itakua ni full-scale war!
 
Nelson...
Ulikuwa unayajua haya?
Mimi yamenishtua sana.

Inaelekea hukupendezwa na ukweli huu.
Nina data kama hizo kutoka vyanzo zaidi ya kumi ila hazina uzito!!Ubora wa majeshi haupo kwenye orodha ya data za Google mzee wangu!!!Tunajadili ufanisi katika operation za uwanja wa mapambano!!!
 
Smart...
Hakika wewe "smart" Mashaallah kama jina ulilochagua.

Umenisomesha.

Allah akuongeze elimu itunufaishe wengi.
 
Mzee wangu fani yetu hatuandiki sana ni watu wa vitendo na codes!!!!Nadhani itakua busara ukijitolea kunifundisha kuandika vizuri mzee wangu sababu naamini hiyo ni fani yako!!
 
Nina data kama hizo kutoka vyanzo zaidi ya kumi ila hazina uzito!!Ubora wa majeshi haupo kwenye orodha ya data za Google mzee wangu!!!Tunajadili ufanisi katika operation za uwanja wa mapambano!!!
Nelson...
Unadhani wewe unaweza kutegemewa kwa elimu za mambo kupita Google?

Unadhani inawezekana kukuweka wewe kama source ikapuuzwa Google?

Source hata 100 zinaweza zikashindana lakini wewe huna nafasi hapo.

Haiwezekani kwani hapo ni ushindani wa wataalamu na tafiti zao.

Wewe huna nafasi.
 
Unazungumza kama raia nakuelewa mzee wangu na upo sawa kabisa!!!Ila medani za kiintelenjisia tuna lugha tofauti kabisa linapokuja suala la sources (Vyanzo vya habari)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…