Mzee wangu
Mohamed Said napingana na wewe hapa. Unasema Israel ilionyesha udhaifu tangu Yom Kippur mwaka 1973 kwa sababu zipi. Iipigwa surprise invasion na majeshi ya Egypt na Syria, Syria wakachukua Golan heights na Egypt wakachukua Sinai kwenye battle za mwanzo. Israel ikapiga counterattack ikaichukua Golan heights nzima na hata eneo ambalo hawakuwahi kuwa nalo na mpaka leo ni lao. Udhaifu wao uko wapi, kama ni dhaifu si Syria ingeteka Golan heights ikabaki nayo, mpaka leo inadai lile eneo.
Eneo la Sinai ni la Egypt lilikuwa limekaliwa na Israel kimkakati kama ambavyo Golan heights ni ya Syria ingawa imekaliwa na Israel, Sinai ilirudishwa kwa Egypt ili Anwar Saddat aitambue Israel kama nchi halali. Ndio maana Egypt ikaondolewa kwenye Arab League. Win win situation kwa Israel na Egypt. Hata Syria inaweza rudishiwa milima yake inhabitable ikifikia makubaliano na Israel.
Saddat alisimamisha mapigano baada ya jeshi lake kuzingirwa na Israel. Hakulazimishwa kusimamisha mapigano, angeendelea ili jeshi lake lipigwe na mateka wawe wengi. 3rd Army ya Misri ilizingirwa na majeshi ya Israel yakiongozwa na General Adan na 401st Armoured Brigade. Wanajeshi 20,000 wa Misri wamewekwa katikati, Israel iko inafanya advancement kuitafuta Cairo iliyokuwa less than 40 miles. Ulitaka Anwar Saddat afanyeje, ujue Waarabu wanafiki kina Saudi Arabia na wenzake wametuma misaada kidogo wako wanakunywa kahawa uko Egypt na Syria zinateseka zenyewe.
Wakati huo pale Syria kama unavyojua Damascus ni mji uko located eneo baya huwa sipendi vile, Israel ilikuwa imepanga shambulizi na imebakiza 10 miles kuifikia Damascus na Al Assad yuko desperate anaomuomba Saddat apigane mpaka mwisho ili kuipa relief Syria. Ambacho hawa wakurupukaji hawakuzingatia ni kwamba kila mtu anapigana kwa interest zake, Egypt za kwake zikitimizwa Syria shauri yako.
USSR ikatishia kuingia vitani zaidi, kumbuka hapo walishatoa misaada wa kila aina. Marekani na Uingereza zimesaidia Israel na Arab League plus USSR zimesaidia Waarabu. Israel ikaachana na kuiteka Damascus ila ikabaki na Golan heights ili ifanye monitoring.
Hakuna aliyelazimishwa ceasefire. Wangeendelea kupigana waambulie kupoteza maeneo mengine.
Na hapo kwa Hezbollah. Hicho ni chama chenye military wing, wala Hezbollah haijawahi unda serikali ya Lebanon. Iko termed kama kundi la kigaidi na usijifanye hujui tofauti ya kupigana na magaidi na kupigana na nchi. Israel haikupigana na Lebanon mwaka 2006, walipigana na kundi la kigaidi. Ile vita ingekuwa ni dhidi ya Lebanon ingeisha mapema sana. Na hata hivyo Israel haikushindwa, iko palepale ilipokuwa hadi leo. Wewe mwenyewe unajua lengo la Hezbollah ni lipi, limekamilika?