IDM ni software muhimu, kwanini watu wengi hata wenye uwezo kiuchumi hawataki kuinunua wapo tayari kuteseka na matoleo ya kuchakachua yanayosumbua

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Unaweza kuwaelewa watumiaji kama wanafunzi kutumia matoleo ya kuchakachua ila inakuwa too much mtu anaitumia idm miaka zaidi ya 10 na uwezo anao bado hataki kuinunua anakomaa na matoleo ya crack yenye changamoto nyingi kuanzia virus, ujumbe kutokea mara kwa mara wa kuinunua, ku expire, n.k.

1739386080458.png
 
Mie huwa nailipia hiyo pamoja na Spotify huwa nailipia lifetime yake ni 67200 pamoja na Spotify 6900
 
Duh! Umenikumbusha mbali sana kumbe hii aplikesheni bado ipo.

Ngoja nikailipie kama shukrani maana imenisaidiaga sana hapo miaka ya nyuma.
 
Unaweza kuwaelewa watumiaji kama wanafunzi kutumia matoleo ya kuchakachua ila inakuwa too much mtu anaitumia idm miaka zaidi ya 10 na uwezo anao bado hataki kuinunua anakomaa na matoleo ya crack yenye changamoto nyingi kuanzia virus, ujumbe kutokea mara kwa mara wa kuinunua, ku expire, n.k.

View attachment 3234691
Ukishakua na hela nadra sana kutumia idm, hii ni software ya watu wanaopenda kufanya Piracy.
 
Kwa bongo yetu hata mtu awe na pesa, wengi bado wanadownload movies

lakini nje ya hapo, hata kudownload vitu vya kawaida ni software nzuri
 
Bongo unaweza kuwa considered una pesa ila ukawa kwa level za kimataifa bado wa kawaida sana.

Movie ukitaka kununua bluray ni kama 50,000-70,000 kihalali, tuseme tu ukweli wenye hela ya kubadili mboga nchi hii wengi bado kuweza ku afford hili.

Alternative ni hizi service za kuazima movie kama Netflix, Dstv, Azam prime na wengineo, wengi wenye pesa kibongo bongo ndio wanatumia, na nadra kukuta wapo interested na kitu kama IDM.

Sisi walalahoi ndio tunatumia sana IDM.
 
Unaweza kuwaelewa watumiaji kama wanafunzi kutumia matoleo ya kuchakachua ila inakuwa too much mtu anaitumia idm miaka zaidi ya 10 na uwezo anao bado hataki kuinunua anakomaa na matoleo ya crack yenye changamoto nyingi kuanzia virus, ujumbe kutokea mara kwa mara wa kuinunua, ku expire, n.k.

View attachment 3234691
Inafanya kazi gani
 
Kwani inafanyaje kazi hiyo application?, wengine hata hatuijui,kama ni ya zamani,ipi mpya kwasasa?
 
Ni program ya kompyuta (IDM - Internet Download Manager) hii inatumika ku download vitu mtandaoni kwa speed sana ukilinganisha na download managers zingine, pia ina capture na ku download contents zingine ambazo sio rahisi (DRM protected content) na kuzi maneuver ili ku downloadika kwa njia ya kawaida...

Mfano Boomplay au SoundCloud ku download audios sio rahisi kama huna Premium subscriptions za hizo platforms ila ukiwa na hii kwenye PC iko integrated kwenye browser unayotumia basi unashusha tu, vile vile ku download videos za YouTube unatumia hii tu...
 
Asante mkuu
 
Torch ina speed nzuri ya kudownload kwa nini usumbuke. Sasa hivi natumia tubemate haina haja ya kusumbuka na app za bei. Watu wengi hawatumii kibiashara ndio maana wanatumia crake.
 
Back
Top Bottom