Idris Sultan afikishwa katika Mahakama ya Kisutu. Ashtakiwa kwa kumiliki laini ya simu isiyo na jina lake. Aachiwa kwa dhamana

Idris Sultan afikishwa katika Mahakama ya Kisutu. Ashtakiwa kwa kumiliki laini ya simu isiyo na jina lake. Aachiwa kwa dhamana

drisa kama Msanii anayetazamwa na watu wengi Aliidhihaki Picha ya Raisi na Watanzania wengi waliiona video clip yake.

Ile picha mnayosema alimdhihaki Rais sio Kweli kwani wakati picha ile ilipopigwa JPM alikuwa mbunge; alikuwa bado hajawa na wadhifa alionao sasa.!!
 
Ile picha mnayosema alimdhihaki Rais sio Kweli kwani wakati picha ile ilipopigwa JPM alikuwa mbunge; alikuwa bado hajawa na wadhifa alionao sasa.!!
Kwa nini hakuicheka wakati huo huo ?

Anaweza kufanya vile kwa baba yake mzazi ?
 
Kilaza mmoja alipiga milioni 500 big brother south Africa malaya wa Dar wamezikomba zote amebaki anaishi kwa kuombaomba mtaani
Daaah yaan mwanangu zile hela ningezipata mm ningekuwa kwenye list ya Forbes now[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Picha ikiwa nyumbani haina shida huo utakuwa ni utani ndani ya familia, mimi naongelea picha imepostiwa instagram kwa mfano picha ya baba yako akiwa amevaa mavazi yaliyochakaa then watu wanatoa comments za kejeli kwa hiyo na wewe utajiunga nao kutoa comments za kukejeli?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndio nitajiunga nao
 
Mkuu nijibu swali langu. Anyway ukiwa unafanya ujinga kama Is hakikisha uko clean(ni ngumu sana) vinginevyo ndio haya yatakukuta.
Hakuna sheria inayozuia kumcheka Rais ndiyo maana wameshindwa kumshtaki kwa kosa hilo.Alivyojitoa kuwa raia wa kawaida alipoteza privacy right nyingi sana.

Nikikucheka au kukudhihaki wewe hapo ni msala mkubwa sana ila siyo kwa Rais. Sasa huku Afrika kwa sababu watu wanaamini kuwa Rais ni Mungu mtu basi ukimcheka wanaona kuwa umetenda kosa kubwa sana
 
Picha ikiwa nyumbani haina shida huo utakuwa ni utani ndani ya familia, mimi naongelea picha imepostiwa instagram kwa mfano picha ya baba yako akiwa amevaa mavazi yaliyochakaa then watu wanatoa comments za kejeli kwa hiyo na wewe utajiunga nao kutoa comments za kukejeli?

Sent using Jamii Forums mobile app
kama kosa ndo ilo kwanini hajashtakiwa kwa ilo kosa...kama alichofanya si sahihi kwanini hamjamshtaki kwa icho ambacho si sahihi
 
Ujinga tu kwani kucheka Kuna tatizo gani Yani nchi za kiafrica sijui kwann maraisi wanawafanya miungu watu.
 
Hakuna sheria inayozuia kumcheka Rais ndiyo maana wameshindwa kumshtaki kwa kosa hilo.Alivyojitoa kuwa raia wa kawaida alipoteza privacy right nyingi sana. Nikikucheka au kukudhihaki wewe hapo ni msala mkubwa sana ila siyo kwa Rais. Sasa huku Afrika kwa sababu watu wanaamini kuwa Rais ni Mungu mtu basi ukimcheka wanaona kuwa umetenda kosa kubwa sana
Nimekuuliza, ukiona picha ya baba yako alivyokuwa sekondari unaweza kuicheka huku unarusha hicho kicheko mtandaoni?
 
Avune alichopanda. Huwezi kufanya dhihaka kwa Mkuu wa Nchi kiasi kile

Angejaribu kuwadhihaki wazazi wake kwanza
We kiaz kwenye mashitaka yake hakuna shitaka la kumdhihaki rais....punguza kuvuta bhangi maana umekua ka zoba fulan hvi
 
Picha ikiwa nyumbani haina shida huo utakuwa ni utani ndani ya familia, mimi naongelea picha imepostiwa instagram kwa mfano picha ya baba yako akiwa amevaa mavazi yaliyochakaa then watu wanatoa comments za kejeli kwa hiyo na wewe utajiunga nao kutoa comments za kukejeli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Anhaaa 😂😂😂
Najizuia kucheka sorry

Ila kidogo umebadili maudhui ingekuwa imechoka imechakaa Idris azingecheka wala, hapo alicheka ukubwa na design ya suti, si uchakavu ile inaonekana ilikuwa imetoka kwa fundi punde tu😄😄

Ila Magu ni baba yetu pia tumecheka suti yake nyumbani(tanzania)
 
Hisia hisia hisia...naona wengi tunaendshwa na mihemko bila sababu za msingi.
Wengine ohh angekua baba yako ingekuaje...sheria zipo nchi iendeshwe kwa kanuni na taratibu.
Mambo gani haya mtu anakaa lockup wiki nzima. Hivi tupo Iraq au Tz.
Kama amekosea wamsomee mashtaka yake awekwe ndani.
Sipo upande wowote ule msije nimwagia mapovu
 
Nimekuuliza, ukiona picha ya baba yako alivyokuwa sekondari unaweza kuicheka huku unarusha hicho kicheko mtandaoni?
Ipo hivi:
Siwezi kumcheka Baba yangu kwa sababu siyo Rais as long as ana privacy right zote, ila akiwa ni Rais kama kuna cha kumcheka kama Rais nitamcheka kama Rais wa nchi na wala siyo kama Baba
 
Unaelewa maana ya Dhihaka wewe.........Kakojoe ukalale huelewi ata haki za msingi za binadamu, nikusaidie........ tuna life, liberty and pursuit of happiness. Niambie kosa lake jamaa liko wapi..... nenda youtube mtafute Travor Noah nadhan utaelewa.
Kila jamii ina maadili yake na miiko yake. Tuweke siasa pembeni.
Tunachojisahau ni kwamba tunafananisha tamaduni za Taifa moja na Taifa jengine kisha tunahalalisha za Taifa jengine ziwe kama za Taifa jengine pasipo kutilia manani kuwa hizi ni jamii mbili zenye tamaduni, kanuni na miiko tofauti.

Travoh Noah yupo Amerika! Kwa anachokifanya kwa Amerika ni sawa, kwa sababu kanuni za kwao zinaruhusu. Lakini kanuni hizo hizo kwa nchi nyenginezo hazi ruhusu! Sifahamu sheria inasemaje kuhusu hili.

Mizaha au matani kimaadili kijamii yetu yanaruhusiwa lakini yanatofautiana mipaka ya rika kwa rika na muda mwengine jinsia inaingia. Alichokifanya Idris kimaadili si kitu kizuri. Magu ni mtu mzima kwake na ni rika la baba'ke. Magu ana watoto.

Umewafikria watoto wake wataipokea kwa namna gani alichofanyiwa baba yao? Kwa sababu baada ya Idris kufanya vile watu wali-comment! Wenye kukandia wakakandia zaidi. Umefikiria watoto wake mtawaweka kwenye hali gani?

Kama kwako hii ni sawa tutumie picha ya mzazi wako miaka ya nyuma jinsi alivyokuwa ana vaa tutamtafuta mtu maarufu aiposti kwenye mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom