IET na ERB zinatuangusha wahandisi

IET na ERB zinatuangusha wahandisi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Wahandisi tutoke vipi? taasisi ambazo zingekuwa zinatusaidia tupige hatua zimesinzia kabisa.

Kazi yao ni kuandaa safari za kutalihi tu kwenye miradi.

Mimi nilitegemea labda tusikie taasisi hizi zikipendekeza namna gani jamii inaweza kuwatumia wataalamu

Mimi nilitegemea kusikia labda wakipendekeza kwa serikali itunge sheria za kuwa na vizazi tofauti makazini kwamba ni lazima kuwe na wazoefu na wanaotafuta ujuzi.

Vijana wanamaliza na kukaa mitaani na hakuna anayeweza kushauri cha kufanya kwa serikali.

Je, waache kufundisha vijana wapya au ubunifu wa namna ya kuwaingiza vizazi vipya?

Wenye dhamana ya kusimamia taaluma hizi wamesinzia FOFOFO
 
Kazi yao kuzunguka na kufuatilia nani anajenga nini na kama kodi yao imelipwa. No strategic work and approaches.
 
Mkuu Uko Registered kwanza?
Una Muhuri?
Una Barcode?
[emoji3516][emoji2957][emoji851]
Hayo Mengine unayohitaji yatafuata Baadae
hili ndilo tatizo kuu, kwamba vyombo hivi vinatazama mafanikio ya wahandisi kwa kutazama usajili, kumiliki muhuri na barcode.

haya siyo mafanikio na wala siyo nyenzo za mafanikio.

jamii inataka kuona matunda ya fani hizi na hiyo inatokana na ubunifu wa wahandisi. ili wahandisi wawe wabunifu kuna mazingira chochezi yanayotakiwa kuandaliwa na vyombo vya usimamizi
 
daaah haya maisha bhana nimwendo wa roho mbaya na kukomoana. Nipo registered na ERB toka 2019, ila hadi Leo sijapata hata sehemu ya kujitolea.hata ukienda ruwasa au tarura unaonekana kama mwanga.ninamengi ila ngoja niishie hapa.SIJUI TUTOKE VIPI
 
Umekuwa registered kama GE,PE au CE? zungukia kampuni za wachina unaweza kupata nafasi..
 
Wahandisi tutoke vipi? taasisi ambazo zingekuwa zinatusaidia tupige hatua zimesinzia kabisa.

Kazi yao ni kuandaa safari za kutalihi tu kwenye miradi.

Mimi nilitegemea labda tusikie taasisi hizi zikipendekeza namna gani jamii inaweza kuwatumia wataalamu

Mimi nilitegemea kusikia labda wakipendekeza kwa serikali itunge sheria za kuwa na vizazi tofauti makazini kwamba ni lazima kuwe na wazoefu na wanaotafuta ujuzi.

Vijana wanamaliza na kukaa mitaani na hakuna anayeweza kushauri cha kufanya kwa serikali.

Je, waache kufundisha vijana wapya au ubunifu wa namna ya kuwaingiza vizazi vipya?

Wenye dhamana ya kusimamia taaluma hizi wamesinzia FOFOFO
Mkuu ERB mbona kwa nafasi yao wanajitahidi sana kusaidia wahandisi wachanga?
 
Hakuna wanachowasaidia

SEAP programe is a disaster

Wapo waajiri wengi hawaajiri tena wanachukua Trainee na ama hawawalipi na kuwafanyisha kazi wakitegemea walipwe na ERB kupitia SEAP programme au wanawalipa kidogo.

Kilichotakiwa ni taasisi hizi kushauri serikali kutunga kanuni zinazowezesha graduates kuajiriwa.

mfano kwa hapa tulipofika tunahitaji kuona vizazi tofauti vya kihandisi makazini, tunahitaji kuona shughuli za mtaani kwenye jamii zikiingizwa wataalamu.

serikali ikiwatengenezea fursa kupitia kanuni wataajirika na kuingia makazini na sio utaratibu wa sasa wa kuwapa uzoefu bila kutazama saturation ya fursa zilizokuwepo
 
Mbona graduates wanaajiriwa tu ...kumbuka mkuu huwa taasisi inaajiri mtu kwa uwepo wa uhitaji na si kanuni
 
kuna Eng. mwenzetu huku anafundisha hesabu shule za mtwara tena kwa kujitolea. hlf vyombo vinavyohusika na usimamizi vipo tu
 
GE, nisha zunguka kampuni kadhaaa ila hakuna tumaini
Pole sana itakubid urud ERB uwaombe wakusaidie upate ufadhili wa SEAP ambayo itaweza kukusaidia kupata uzoefu wa kazi na baadae kusajiliwa kama PE ambapo hautapata msoto wa kazi kama kuwa GE.
 
Mbona graduates wanaajiriwa tu ...kumbuka mkuu huwa taasisi inaajiri mtu kwa uwepo wa uhitaji na si kanuni
Jambo usilolielewa ni kwamba kila mwaka vyuo vinazalisha wataalamu wengi tu.

Lakini ukienda mtaani sehemu zinazoajiri ni zile zile na kwa kuwa hakuna usimamizi kuna sehemu walitakiwa kuajiri engineer lakini unakuta wanakwenda tu na technician.

kanuni zinakuja kwa serikali kutunga utaratibu wa kazi kwa sema labda kila anaye jenga ghorofa kuanzia sasa lazima kwanza lisanifiwe na architecture. hakuna swala la kuchukua ramani yamtu ukaanza kujenga. pili lazima ujenzi uhusishe mtaalamu wa structure, umeme na plumber.

kwa hiyo tungeona magorofa yanayochipua kwa kasi yanachochea upatikanaji wa ajira kwa wataalamu.

au kama unavyoona kwamba ili ufungue duka la dawa lazima udhaminiwe na dakitari basi hata kufungua ofisi ya umeme lazima udhaminiwe na mhandisi wa umeme, ili ufungue gereji au kijiwe cha kuchomelea lazima udhaminiwe na mechanical engineer.

kwamba ili ufungue biashara ya chakula lazima udhaminiwe na mtaalamu wa lishe.

hizo ndizo kanuni ambazo serikali ilitakiwa kukaa inatazama jamii na kubuni wataalamu wetu tunawapeleka wapi.

Lakini ni ngumu kwa serikali yenyewe kuwaza haya bali wahandisi wenyewe kupitia vyombo vyao ndiyo wanaoibua haya. vyombo vyenyewe vinavyotakiwa kuibua haya ni kama IET na ERB lakini wapo wamelala FOFOFO
 
Serikali ihakikishe kila kampuni ya level fulani Tanzania inakuwa na apprentice programes + trainee programs for engineers na wawalipe... hii itasaidia junior engineers kupata uzoefu.

Serikali ihakikishe mtaala wa science na masomo mengine unaendana na uhalisia wa dunia, dunia iko mbali sana kwenye teknolojia, Ni vyema wahitimu wakaandaliwa kulinga na dunia ilipo..Katika hili pia mashuleni elimu iwe ya vitendo sana kuliko nadharia...study tours ziwe za kutosha maviwandani, maofisini, migodini nk..

Serikali ifute kabisa elimu ya kidato cha sita na muda wa elimu ya msingi upunguzwe sambamba na elimu ya chekechea kutolewa mkazo kwa wazazi kupeleka watoto wakiwa na miaka mitatu, na lakwanza iwe miaka 6 huku elimu ya msingi ikiwa miaka mitano...mbadala wa kidato cha sita iwe diploma level kuanzia law, engineering, uhasibu nk huku vyuo hivi vikiwekeza sana kwenye elimu kwa vitendo na wanaotoka na matokeo mazuri wanakwenda vyuo vikuu..

Kuanzia elimu ya msingi na sekondari wanafunzi wawe wanapewa projects na kufanya presentation wao kwa wao mbele ya wazazi, hata kwenda kwenye taasisi tofauti tofauti na mashule mengine tofauti tofauti...

Kwasasa Inasikitisha sana kiwango cha wahitimu wetu kutoka mashuleni na vyuoni ni hatari sana kwa hiki kizazi na uelekeo wa dunia...Serikali ijaribu kuwa sikivu na kuweka nguvu haraka na mapema katika hili vinginevyo Taifa hili litabaki kuwa la watu walalamishi, watu watumwa nk..
 
HATUNA SHIDA KWENYE TRAINING TUNA SHIDA KWENYE LIFE AFTER TRAINING

tunavyo vyuo vingi vinazalisha wahandisi katika jamii yetu na shida imekuwa je hawa wahandisi wanaenda wapi kufanya nini?

tunataka sehemu zilizokuwa na mhandisi mmoja sasa kanuni zielekeze system iwe na mhandisi mkuu na mhandisi msaidizi (experienced na junior anayejifunza kwa huyu experienced.

kila shughuli ya kihandisi inapofanyika lazima ihusishe mhandisi.

na kila mhandisi abaki katika eneo lake la taalauma yaani mtaalamu wa zege abaki kwenye zege, mtalamu wa chuma abaki kwenye chuma n.k
 
Back
Top Bottom