Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #201
Wanabodi,
Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndiye mshindi wa urais Tanzania
Hivyo wakati wa kusikilizia kama atakuwa dikiteta kweli, the real dictator, or a benevolent one!. Ikitokea Magufuli kiwa the real one, yaani ni dikiteta kweli usipomjoin, umekwisha!, hivyo ikitokea Magufuli akawa dikiteta kweli, then Tanzania tunaelekea kwenye utawala wa totalitarian na authoritarian nakurudi kuwa nchi ya chama kimoja!. Ikitokea Magufuli akawa dikiteta kweli, faraja pekee kwa Watanzania itabaki kwa yule aliyemleta, ndiye atakaye mtwaa ili kulisuru taifa la Mungu!.
Hoja kuwa Magufuli ni dictator haina mjadala, kwa watu wenye jicho la tatu, wanaona the fire on his eyes, and then fear is the weapon on his heart kwa kutoa hotuba za ukali kama anagomba!, ambayo ni kiashiria cha seriousness ya hasira ambayo inaweza kugeuka chuki na kupelekea visasi toka moyoni mwake, kwa kila atakayetofautiana naye!, na wenye sikio la tatu wanaisikia tone ya ukali wa ukatili kwenye sauti yake!, hii ni ishara kuwa huyu sio mtu wa masihara, watakao tofautiana nae, wanaweza kuumia au hata ...(God forbid), hili likitokea, kutakuwa hakuna jinsi bali kitu kinachoitwa karma, kitaingilia kati na kurekebisha the situation.
Kitu cha muhimu sana cha kufanya kwa sasa ni sisi Watanzania wote, katika umoja wetu, kwa imani kuwa ni Mungu ndio anaweka tawala za mataifa, Tanzania tumefanya uchaguzi mkuu huru na wa haki, Magufuli ndiye ameshinda kihaki na kihalali, then Magufuli ndio chaguo la Mungu kwa Tanzania, akitenda kinyume cha Mungu ni Bwana ndie ameleta na Bwana ndie atatwa, na Jina Lake Lihimidiwe !.
Hivyo natoa wito kwa Watanzania wote wazalendo wa kweli kwa taifa lao na wenye mapenzi ya kweli na taifa hili, kumuombea tuu Magufuli kwa Mungu, tena kumuombea very seriously, maadamu ni Mungu ndiye aliyetupa Magufuli, then angalau Mungu huyu huyu amfanye kuwa ni a benevolent one ili huo udikiteta wake ulisaidie taifa letu kusonga mbele kiuchumi, kimaendeleo na kiustawi wa jamii japo is at a price of dead democracy!, vinginevyo akiwa the real one, tumekwisha!, tutajuta, mbele ya safari kutakuja kuwa na vilio na kusaga meno!, ila mwisho wa siku ni Mungu atatwaa, watu watapita, lakini Tanzania itabaki.
Paskali
Karibu mitaa hiiKama una maono kwa nini ujaona ...
p