Morobest ile ligi ilimshinda, wamebaki Kidinilo na Al Saedy tu.
Mara ya Kwanza naenda mahenge 2011 nilishangaa sana [emoji23][emoji23]nimezoea mabasi kutoka mikoa yetu ya kazkazini nikisafiri ukikata ticket seat yako ni yako Kuna luxury na semi luxury uwezo wako tuu.
Nimefika Msamvu nikapata ticket ya kesho yake Alisaed nakumbuka ilikua 17000/=mpk mahenge. Nikahakikishiwa kua basi litatoka Dar litafika Msamvu saa 4.
Kesho yake nimefika saa 3 Msamvu tumekaa mpk saa 5:30 hakuna kitu tunaangaliana tuu. Basi limefika tukaambiwa kila mtu abebe mizigo yake basi lipo Ofisini pale mbele kwenye sheli yao. Aisee sasa si mngesema mapema.
Kufika pale naingia ndani ya basi limejaa siti yangu ina mtu kaanzia Dar safari na yeye kakatiwa seat hiyo hiyo aisee nilichoka. Nikashuka nawaambia naona maneno meengi nikaishia kupata seat mwishoni kabisa. Wengine wamekalia vigoda na ndoo katikati. Nikasema amaaa kweli. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Safari ikaanza naona watu wapo bize wananunua mikate tuu sielewi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji50]tukavuka mikumi mbele huko kumbe hamna lami acha tuanze kurushwarushwa nikasema hapa kumekucha. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nauliza tunafika saa ngp wanauliza kwani nashukia wapi nikasema Mahenge wakasema kua mpole sana kwa saa hizi wewe unaweza kufika saa 4 usiku.
Tukafika mang'ora Kuna kona moja hivi basi likazama kwenye matope. Halichomoki. Tukashuka hapo ikachukua kama masaa 2mpk likatoka.
Safari ikaendelea mpk tunatoboa Ifakara saa kumi jioni. Nilikaa na mtoto wa Ifakara girls machipi ye Kashukia kibaoni.
Tumefika Ifoza naskia wanaoenda Mahenge watoe tickets tukatoa nenda kwenye buti uchukue mizigo. Nashangaaaa tuu nini hiki [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Tukamfuata yule mtu kufumba na kufumbua tumefaulishwa kwenye lori (canter la kimchongo) wenyewe wanaita mdedea nikasema Kwisha habari yangu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ilikua msimu wa mvua mwezi WA 2 hivi basi tumeenda na Lori mpk kivukoni tukavuka na Pantoni maji yalikua mengi sana kule ndani wakati wa kutoka na kuingia inabidi uvue viatu lile sijui ndo gata halifiki mwisho kwenye kingo. Ukitoka uvae viatu. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kula saana samaki pale safari ikaendelea giza likaingia story kama zote tumefika mbele dereva analalamika tumekua wazito Ndololo hatoboi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Likaja nyuma yetu Lori kubwa kidogo nakumbuka lilikua fuso wakashauri tuache mizigo kama ni mingi tuingie (tufaulishwe tena) kwenye fuso hasa wanaume tukaingia ndani saa 4 usiku tukatoboa Mahenge. Tumefika tunasubiri sasa canter Ifike huku tunasali kimoyomoyo kuhusu mizigo. Anyway kwenye saa 5 hivi likafika kila kitu kulikua sawa. Tukaingia Shule kumbe wanafunzi mle ndani tulikua 70%
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]