Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Mahenge ni wilaya inayopatikana kusini mwa mkoa wa Morogoro na kabila la Wapogoro ndio wanapatikana huko. Ikiwa eneo la juu (Mlimani) na hali ya hewa ya ubaridi na mvua mvua.

Wilaya hii ina vivutio na siri nyingi mno, kihistoria,kiserikali na hata kidini (Je, umewahi kuisikia Wilaya hii na unapata picha gani juu yake?)

Vivutio; kwa upande wa vivutio kuna;
1. Kabila lenyewe linalopatikana huko (wapogoro) asili yao na lugha yao,tamaduni na style yao ya maisha. (kuoana ndugu mradi wasitike nababu mmoja) Uzuri wa wanawake wao wana miili yenye nguvu mno..

2. Ardhi na landscape yake, jinsi kulivyo na miinuko na misitu na vile ambavyo mji umechongwa.

3. Majengo ya mjerumani (boma) ambalo linatumika kama ofisi kuu za serikali (wilayani) na jengo la mkuu wa wilaya . Lakini pia majengo ya wamisionari (kanisa katoliki la tatu kwa ukubwa la tanzania lilojengwa kwa mawe tupu na mji wake ikijumuisha na shule zilojengwa na wao)

4. Misitu na miti pekee, na alama zilowekwa juu ya milima na misituni na wakoloni, hivyo ni baadhi.

Siri zilizoko;
1. Kuna madini ya aina mbali mbali yanayopatikana na kuchimbwa huko (rubi, spinal, greentomalin, uno, dhahabu na hata almasi)

2. Kutokana ni mji wa kikoloni, Mjerumani na Muingereza walikuwako huko hivyo alama zao juu ya milima na misitu zinamaana fulani, je ni ipi?

3. Kwanini wilaya hii licha ya kuwa na vyote hivi lakini bado imefungwa kimawasiliano ya barabara??? njia ni mbovu lakini pia haitoki inatoka kwa njia za mikato pekee.

4. Toka miaka viongozi wake wamekuwa wakinifaidisha wao, maajabu maendeleo yao pia yamekuwa hayaonekani sio kwa wao tu hata kwa ndugu zao (viongozi walowahi kutoka huko kwa uchache Late Amati liyumba aliwahi kuwa BOT, Late Mama Celina kombani alikuwa mbunge kabla CCM hawakumpa asante ya kumuweka mwanae kuwa mbunge baada ya mama yake Bw. Goodluck Mlinga ambae ameshindwa kuchukua jimbo mara baada ya miaka mitano kuisha .Sasa linashikiliwa na Bw. Almasi.

Je, kwanini hakuna maendeleo?

Je, kwanini viongozi wa huko ni kama wanaogopwa na wapogoro?

Je, kwanini mpaka leo barabara ni ya vumbi na kuna muda inakuwa mbaya na chafu kabisa?? kama unaogopa mlima kitonga basi usiendeshe kwenda Mahenge kuna mlima unaitwa ndororo ni hatari mno..

Kwa nini Viongozi wanaweza kaa msimu mzima wakaenda tembelea jimbo mara moja? especially walopita!!

Mimi nimeeleza vitu baadhi, waeza jazia vingine vile unafahamu kuhusu mji huu pia kuweza kualika kiongozi unae mjua aje ajibu baadhi ya hoja. Pia hata kueleza maswahibu au vituko ulivyowahi kutana navyo kwa mji huu maana na hata uchawi upo na wanatumia live.

cc: Goodlucky Mlinga
cc: Mkuu wilaya Mahenge Ulanga na mkurugenzi wake..
cc: Mbunge wa sasa Bw. Almasi
Mahenge Kuna uchawi wa kijinga sana
 
Unampata Mama mwana?? Dada Jane(RIP) na wale wamama wa pale UTU [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Aahhhahhaah UTU
Ali Kiba jina la wimbo wake wa UTU atakuwa alilitoa Mahenge.

Nachopendea ni ule mnada wa Jumapili, tukitoka Kanisani tunapitia pale kununua ngadu wa kutosha na mihogo.
 
Aahhhahhaah UTU
Ali Kiba jina la wimbo wake wa UTU atakuwa alilitoa Mahenge.

Nachopendea ni ule mnada wa Jumapili, tukitoka Kanisani tunapitia pale kununua ngadu wa kutosha na mihogo.
ngadu ni kaa wanaishi kwenye mawe mtoni... kwa wadio fahamu jamani . . viumbe wana ganda km la yai na wana mikasi mikubwa mikali ya kubana.
 
Usisahau na wa Sri Lanka waliojazana mjini huku wazawa wakizidi kuwapisha nyumba..
Ni mji ambao wazazi hawana muamko sana wa elimu, asilimia 80 ya vijana wanapomaliza kidato cha nne huishia kaz za mgodini, hawajui shughuli zingine tokana na nature ya wilaya.
 
Tabia za wapogoro zikoje na tamaduni zao nataka kuoa upogoroni
Wakarimu sana na wana umoja, ila shida yao moja hawapendi kuona mwenzao kafanikiwa hawachelewi kukuloga. Machizi wengi wa huku wengi wao walilogwa na ndgu zao. Kwahyo uchawi upo na ukihisiwa basi unapelekwa kwa wataalamu unanyolewa nywele zote wanaamini hutakuwa na nguvu tena, na ukitaka kurudia uchawi tn basi utakufa. Unafiki pia haupo nyuma
 
Kuna kipindi huko nyuma kanisa katoliki lilikuwa na changamoto ya kufaeiki kwa maaskofu wake wanaoteuliwa kuongoza jimbo la Mahenge
 
Wakarimu sana na wana umoja, ila shida yao moja hawapendi kuona mwenzao kafanikiwa hawachelewi kukuloga. Machizi wengi wa huku wengi wao walilogwa na ndgu zao. Kwahyo uchawi upo na ukihisiwa basi unapelekwa kwa wataalamu unanyolewa nywele zote wanaamini hutakuwa na nguvu tena, na ukitaka kurudia uchawi tn basi utakufa. Unafiki pia haupo nyuma
upo mahenge madame??
 
Uzi umenirudisha 1996-1999 nikisomea upadri kukaa Kasita Friary pembeni ya Kasita seminary. Kimasiara sana watoto wa Uponera village. Siku mkitoka out kwa Mama Choma anatuficha Askofu asitukamate. Igota,
Lupiro , itete Mtimbira Kalengakero mpaka Malinyi mchaga Mimi nimekatiza nchi khaaa. Tanzania nzuri sana.
 
Kuna kipindi huko nyuma kanisa katoliki lilikuwa na changamoto ya kufaeiki kwa maaskofu wake wanaoteuliwa kuongoza jimbo kuu la Mahenge
hii hadithi mliwahi kuisikia na chanzo kilikuwa kiongozi wa kanisa katoloki wa hukohuko Mahenge.
 
Hao walikuwa wanapambana na O - Level, sisi Advance tulikuwa tunadeal na wadada na wamama wa mtaani kwanza walikuwa wanatuhonga misosi na penzi la bure hakuna kuhangaika[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] makubwaaaa khaaah
 
Back
Top Bottom