Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Ifahamu Mahenge (Ulanga, Morogoro) na siri zake

Mwambie tuliwekewa kabisa na sehemu za kuchaji Kule Dining Hall. Yaani Head master anauliza wanafunzi kama Kuna mtu anauza vocha za Tigo [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mbna ilikua hataree hii. Khaaah
 
Mi nimesoma advanced pale 2007/2009, na sio kwamba shule nyingine za gavoo walikuwa wanaruhusu, hata shule niliyosoma ya o level simu ilikuwa ni kosa la kukufukuzisha shule, ila pale Kwiro simu tulikuwa tunaruhusiwa kuwa nazo
Duuuh bas ilikua hataree.
 
Ni kweli kabisa. Alichosema mkuu Kuna wakati hapo Kwiro sim ziliruhusiwa niliyokua Form 6 ndo zilikatazwa.

Ishu ilikua hivi walikuja wakaguzi wa Elimu sasa Kuna mwana mmoja akawa anaongea na simu pale karibu na bendera. Wale wakaguzi wakamgeukia Mkuu wa Shule almarufu kama Kimbunga vipi huku sim zinaruhusiwa??? Mkuu akajitetea kwamba kwa sababu shule ipo mbali sana waliona sio vibaya wanafunzi Kuwa nazo.

Kesho yake mkuu akaja assembly akasema " yaani Mimi nawaachia mtumie simu nyie mnakuja kuniabisha mbele ya wakaguzi???? Kuanzia leo hakuna ni marufuku simu kutumia kwa uwazi au kwenda nayo darasani"

Tukaendelea kutumia kisela. Sasa siku moja Kuna Dogo alihama pale(Dogo ana ndugu yake mkubwa tuu wizara ya Elimu inavyodaiwa) akahamia Malangali kama sikosei kufika kule akanyang'anywa simu.

Akalalamika mbona Nilipotoka (Kwiro boys) simu ni Ruksaaa yaani kama unanawa vile, matangazo ya vocha mpk chooni
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]yaani ukiwa unakata gogo ukiangalia mlangoni pameandikwa (Vocha za Voda njoo Chemba ya HP)

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Taarifa zikafika juu ndo mzee baba Headmaster akapigiwa simu moja kesho yake zile socket kule Dinning tunakuta zimetolewa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaah
 
Mto Kilombero kabla ya daraja kujengwa.
Screenshot_20220727-225524.jpg
 
Ivi ni mji gani hauna mchaga,ndio yale maneno ya yule mzee wa Efatha aliposema ukiona kwenye mji ama mtaa hakuna mchaga hama,ama hata jela ukikuta jela ama gereza hakuna mchaga hama,anasema sehemu isiyokuwa na mchaga hainaga maendeleo kamwe ndio naamini sasa
Na Mkinga
 
Uzi umenirudisha 1996-1999 nikisomea upadri kukaa Kasita Friary pembeni ya Kasita seminary. Kimasiara sana watoto wa Uponera village. Siku mkitoka out kwa Mama Choma anatuficha Askofu asitukamate. Igota,
Lupiro , itete Mtimbira Kalengakero mpaka Malinyi mchaga Mimi nimekatiza nchi khaaa. Tanzania nzuri sana.
Mseminari wa Mchongo.
 
Kwani Mahenge ni Jimbo kuu?.Nitajie Maaskofu wa RC wa Jimbo la Mahenge ambao walishafariki.
Jimbo katoliki la Mahenge (kwa Kilatini Dioecesis Mahengensis) ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Roma.

Makao makuu yake yako Mahenge katika mkoa wa Morogoro.

Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Dar-es-Salaam.

Askofu wake ni Agapiti Ndorobo.


Historia​


MaaskofuEdit

 
Back
Top Bottom