Ifahamu nchi kubwa kuliko zote duniani

Ifahamu nchi kubwa kuliko zote duniani

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
IJUE NCHI KUBWA KULIKO ZOTE.

Je, unafahamu kuwa Urusi (Russia)/ USSR Ndio nchi inayo shika rekodi ya kua nchi kubwa kuliko nchi yeyote duniani?

Basi fahamu Kuhusu ukubwa wake, eneo lake kwa ukubwa ni 17,075,400km² za mraba (million17.1km²), ambayo sawa na 12,577mile kwa urefu.

Pia Urusi inachukua 11% ya eneo lote la nchi kavu duniani.

Na imepakana na nchi 14 ambazo ni North Korea, China, Norway, Finland, Ukraine, Georgia, Mongolia, Latvia, Estonia, Azerbaijan, Belarus, Lithuania, Abkhazia na South Ossetia.

Lakini pia nchi hii imepakana na Taifa la Marekani ikiwa imetenganishwa na Bahari. Iko karibu vilevile na maeneo ya Marekani (jimbo la Alaska liko ng'ambo ya mlango wa Bering) na Japani (kisiwa cha Hokkaido kiko ng'ambo ya mlango wa La Pérouse.

Urusi Pia inajumla ya wakazi 145,934,000 yaani Wanaume wakiwa 67,640,000 ambao sawa na 47% ya wakazi Wake na wanawake wakiwa 78,294,000 sawa na 53% ya wakazi wake wote.

Lakini pia Russia ni nchi ambayo imeingia (inapatikana) katika mabara mawili tofauti yaani Asia na Ulaya licha ya kuwa Russia rasmi hupatikana Bara la Asia
Pia maajabu yaliyopo ndani ya Russia ni kwamba kuna baadhi ya maeneo yanatofautiana hadi masaa 11. Yaani eneo moja la Russia linaweza kua saa 12 asubuhi wakati huo huo eneo jingine ni saa 10 jioni.

Hiyo ndo Russia na hayo ni machache kuhusu Urusi
 
Kuna uzi mmoja pia nimeoana humu ndani jmaa wanabishana kuwa urusi nayo imepakana na marekani

Sas wakifanikiwa kuitwa urkraen s ndio itakuwa kubwa zaid
 
Maji yanayotenganisha US(Alaska) na Russia yana upana ya 2.5 miles na yanaganda kipindi cha baridi, hivyo unaweza tembea kwa miguu toka US mpka Russia
 
nasikia ukienda soma Urusi urejeapo Tanzania, unakuwa ka umevurugikiwa iviii -mawenge mawengeee hahaaaaa nahisi ni zile toti za pombe kali kuliko k-vant asubuhi
 
Mada ya kijinga. Mtu yeyote aliyeishia darasa la saba akipewa atlas na kuulizwa maswali haya atayajibu yote!!!

Kipi kipya kuhusu nchi kubwa kuliko zote duniani na mipaka yake???
 
Fact nyingine
Nilisikia urusi ni kubwa kuishinda sayari kibete ya pluto
Kuna Muda hawa hutuambia mara sayari Fulani imepotea yaani shida tupu.

Ila huenda ikawa hivyo
 
IJUE NCHI KUBWA KULIKO ZOTE.

Je, unafahamu kuwa Urusi (Russia)/ USSR Ndio nchi inayo shika rekodi ya kua nchi kubwa kuliko nchi yeyote duniani?

Basi fahamu Kuhusu ukubwa wake, eneo lake kwa ukubwa ni 17,075,400km² za mraba (million17.1km²), ambayo sawa na 12,577mile kwa urefu.

Pia Urusi inachukua 11% ya eneo lote la nchi kavu duniani.

Na imepakana na nchi 14 ambazo ni North Korea, China, Norway, Finland, Ukraine, Georgia, Mongolia, Latvia, Estonia, Azerbaijan, Belarus, Lithuania, Abkhazia na South Ossetia.

Urusi Pia inajumla ya wakazi 145,934,000 yaani Wanaume wakiwa 67,640,000 ambao sawa na 47% ya wakazi Wake na wanawake wakiwa 78,294,000 sawa na 53% ya wakazi wake wote.

Pia maajabu yaliyopo ndani ya Russia ni kwamba kuna baadhi ya maeneo yanatofautiana hadi masaa 11. Yaani eneo moja la Russia linaweza kua saa 12 asubuhi wakati huo huo eneo jingine ni saa 10 jioni.

Hiyo ndo Russia na hayo ni machache kuhusu Urusi
Nahisi hujawataja majirani wote
Kazakstan,UsA
 
Mada ya kijinga. Mtu yeyote aliyeishia darasa la saba akipewa atlas na kuulizwa maswali haya atayajibu yote!!!

Kipi kipya kuhusu nchi kubwa kuliko zote duniani na mipaka yake???
Mkuu kuna wengine hawajui kusomaa atlas na c mbaya mleta mada akitujuzaa ,kwan ameyumia bando lako mkuu kuletaa hilii bandiko hapa achaa hasiraa
 
Back
Top Bottom