Salama wana jamii Amani na iwe juu yenu
Nimependa Leo nije na uzi huu juu Sifongo
Na Siki. Jambo ambalo halijazungumziwa Sana juu ya mateso ya Yesu wa Nazareth pia kuna jambo baya alifanyiwa na watesaji ambapo alipewa sifongo yenye siki utajiuliza ni kwanini alionja tu ile Sifongo alikata roho Luka 23:36 na Mark 15:36 mmoja wao alienda mbio akajaza sifongo katika chombo akatia katika mwanzi akamnywesha Alipoipokea akakata roho....
Sifongo ni kitu gani?
Enzi za utawala wa kifalme sifongo. Ilikuwa ikitumiwa na wawindaji na askari vitani kuua wanyama hatari. Kama dubu Simba mbwa mwitu pia ilitumiwa na wapiganaji vitani ambapo hutembea na sifongo siki katika chombo kisha huchovywa ncha ya mshale au mkuki katika chombo na huu tupa ambapo adui hupoteza maisha kwa sekunde chache maana sumu Kali sana(wataalumu wa usiku hizi. Wanaifananisha sumu Kali ambayo hupigwa. Kwenye mashamba kwa ajili ya kuua majani ikiwa haijachanganywa na maji) in short Sifongo kwenye siki ni sumu Kali sana tena sana
Je sifongo katika siki imetengenezwaje?
Kwa kifupi taarifa za awali zinasema hutumia mifupa ya aina ya Fulani ya nyoka na mafuta yake na taarifa nyingine husema ni mizoga na nyongo crocodile lakini haikujulikana taarifa za 100% kua hii ndio hasa ilitumika kutengenezea Sifongo iliotiwa Siki sumu kali sana
Muwe na mchana Mwema
tunashukuru kwa ufafanuzi. pamoja na yoote, ninamshukuru Mungu kwa mambo yafuatayo:-
1. YESU KRISTO WA NAZARETH ALIBEBA MASIKITIKO NA HUZUNI ZETU ZOOOOTE. how? Imeandikwa mwenyewe alibeba huzuni zetu zote na masikitiko yetu yote. Hii ilidhihirishwa pale Gethsemane alipokuwa akiomba, alihuzunika kiasi cha kutoa jasho kama matone ya damu. kisayansi inasemekana mtu akihuzunika beyond description anaweza kutoa jasho au machozi ya damu, na Yesu alihuzunika hadi kufikia mwisho kwasababu katika ulimwengu wa roho ili abebe huzuni zetu zote alitakiwa ahuzunishwe hadi point ya mwisho ambayo mwanadamu yeyote huwa anaweza kuifikia katika huzuni na kwa maana hiyo akatimiza andiko kwamba alizibeba huzuni zetu zote na masikitiko yetu yote. hata leo unaweza kuwa na stress, huzuni kubwa lakini mguso wa Roho Mtakatifu moyoni utafikiri umetulizwa kiu kwa maji baridi toka kwenye chungu. huzuni inafutika na kicheko kinakuja. Yesu aweza kufanya hivyo kwako leo na alishamaliza, alisema imekwisha akimaanisha huzuni, masikitiko, mateso na kila kitu kimeshalipiwa deni naye kwani alifanyiwa badala yetu na yeyote amkimbiliaye kwa kumwamini, kumkiri na kuamua kuacha dhambi atamtua mizigo yake yooooooote.
2. ALIDHARAULIWA BEYOND DESCRIPTION ILI SISI TUSIDHARAULIWE: Yesu alidharauliwa, alitemewa mate, alivuliwa nguo mbele ya kamamnasi, alidhihakiwa kwa dharau mbele ya kadamnasi, alifanywa yoote kuondoa utu wake badala yetu, alitukanwa mbele ya kila mtu. hii yote ilifanyika ili awe amebeba yote ambayo sisi tungefanyiwa, ukimkimbila aweza kuondoa kudharauliwa kwako; hata kama umedharaulika mno labda kwasababu hauna pesa, hauna watoto, hauna kazi, hauna nyumba, hauna chochote, una historia mbaya ya umalaya, ujambazi n.k Yesu alidharauliwa beyond description hivyo ili wale watakaomwamini wasidharauliwe. Trust me, niliwahi kudharauliwa kuwa mimi ni masikini nisiye na kazi hadi watoto wadogo walinidharau na nilifika kipindi hadi nikitembea njiani nilihisi majani/manyasi nayo yamenidharau. watu niliowaamini wangenitia moyo au wale niliowasaidia hadi wakafika pazuri walifika hatua kunidharau kuwa sina kitu mbele za watu na kunidhihaki. lakini Mungu alikuja kubadilisha kibao akarudisha miaka yangu yote iliyoliwa na parare na madumadu, sasahivi nimewazidi mbali mno na wanahangaika kunitafuta walau kupitia na wakifika lazima waruhusiwe na ps wangu ambaye ni strict.
3. ALIPATA MAUMIVU NA MATESO MAKALI KUPITA KIASI: Ili sisi tu sipate mateso hayo. amini usiamini, kiroho alishayabeba yote, hata kama kimwili utaumia kwa muda lakini utashangaa kiroho unashangilia. angalia kile kilichotokea kwa Stefano wakati alipopigwa mawe kwa ajili ya imani, alishangilia kifo. mateso ya Yesu yalikuwa makali mno, alipigwa mijeledi mbele za watu, mijeledi ile ilikuwa ya kirumi yenye misumari ikipigwa inatoka na nyama, Biblia inasema "n
a kwa kupigwa kwake sisi tumepona". Ilikuwa lazima afanyiwe vile ili mwili upate maumivu na mateso na maumivu makalii hadi point ya mwisho, ili kubeba maumivu yote ambayo mwanadamu angeweza kukutana nayo. ukiumwa unaeza kupata maumivu, kuna wakati mwili unaweza kupata maumivu, lakini kiroho yote hayo Yesu aliyabeba, na huwa inadhihirishwa kimwili pale unapomwamini kuwa atafanya. hata leo hii Yesu anaweza kukuponya magonjwa yako yote
kwasababu alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. kumbuka kwamba, imeandikwa mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele, lakini Yesu alijeruhiwa ili sisi tupone magonjwa yetu na tupone na kifo kwasababu alishinda kifo kwa kufufuka, yu Hai hivyo kifo na mauti havina uwezo juu ya wale wanaomwamini na kumfuata. ukitaka kuamini hayo kamuulize mchawi anayeoperate kiroho atakuambia amejaribu mno kuwaloga watu waliookoka wafe lakini uchawi ulishindwa. pia ilikuwa lazima apigwe sana mwili upate maumivuuuuu, ajeruhiwe apate maumivuuu ili awe amebeba maumivu yote ambayo mwanadamu angeweza kukutana nayo, na hayo yote Yesu alimaliza ndio maana alisema imekwisha, deni lote alilipa kwa ajili yako.
4. ALIMWAGA DAMU NYINGI SANA KAMA KAFARA KWA AJILI YANGU MIMI NA WEWE: Enzi za zamani, Mungu alipatana na wanadamu kwa njia ya kafara la kumwaga damu za wanyama kutokana na dhambi ulizozitenda. lakini tangu awali alipanga kuja kutoa kafara moja tu once and for all, kafara la Damu ya Yesu. imetabiriwa mno sitaweka mistari hapa hadi aje mtu mbishi ndio nitaweka, nataka haya niandikayo yatoshe hapa. zaidi ya kumwaga damu, lakini aliuawa kama mwanakondoo wa Mungu ili kuichukua dhambi ya ulimwengu wote, na alifanya hivyo. Isaya 53 kasome, hadi wayahudi imefika kipindi sura hii wanashindwa kuikwepa kwasababu ilitabiriwa miaka mingi sana kabla ya kuzaliwa kwake. hii inadhihirishwa na utendaji kazi wa Damu ya Yesu,
Ufunuo 12:11 imeandikwa "nao wakamshinda shetani kwa Damu ya Mwana Kondoo na kwa Neno la Ushuhuda wao". Damu ya Yesu hata leo hii ukiitia inaponya, inafukuza mapepo, inafukuza majini, inafukuza magonjwa, inafukuza wachawi, inafungua vifungo vyote, inaweza kukuweka huru. hii ni kwasababu Shetani mwenyewe kama mwanasaheria anayefuata sana sheria, anajua mbele ya Damu ya Yesu kila deni lililipwa, deni la magonjwa, deni la vifungo, deni la mateso, umasikini, etc vililipwa, ukiona anakushikilia ujue anakutapeli ila ukimwendea kwa Damu ya Yesu atoke kwa kumpa ushuhuda kwamba Yesu alilipa deni lote hivyo shetani hakudai kitu, huwa hana namna anaondoka. pia hili ni Bom, kama kweli moyoni upo na Mungu ukimtamkia tu ni moto ulao ataondoka bila hata kuomba ruhusa kwasababu itamuunguza.
5. YESU ALIKUFA NA KUFUFUKA, AMESHINDA MAUTI NA KUZIMU", ilishatabiriwa kuwa siku ya tatu atafufuka. na kweli alifufuka akaishi hapa duniani siku 40 ndio akapaa. Ilikuwa lazima afe kabisa kabisa akate roho, ili Neno litimie, ili kafara la dhambi zetu litimie, alishuka kuzimu akamnyang'anya shetani funguo za mauti na kuzimu, anazo, sio funguo kama hizo za mlangoni kwako, na NGUVU NA MAMLAKA, hivyo Yesu na kwa Jina lake tunayo mamlaka juu ya mauti na kuzimu, hautakufa kama Mungu hajaamua kama utakuwa ndani ya Yesu, nguvu za kuzimu hazina nguvu kwako hadi pale utakapowapa nafasi wewe mwenyewe. imeandikwa, k
wa Jina la Yesu kila goti litapigwa la vitu vilivyoko juu, vilivyoko duniani na vilivyoko chini ya nchi, na kila ulimi ukiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana. kwanini tunasema alikufa? baada ya kukata roho, askari wa kirumi alimchoma mkuki ubavuni damu na maji vikatoka. kutoka maji ni udhihirisho kwamba kafa. mtu akifa au mnyama yeyote akifa ukimtoboa utaona damu na maji vimeanza kugawanyika, hivyo kwa kutoka damu na maji ilithibitisha kwamba Yesu alikufa. lakini baada ya siku tatu alifufuka kwa kuishinda mauti, mauti haikuwa na nguvu kumshikilia, ndio maana hata kufufuka kwake hata walinzi wa kaburi walishughulikiwa. hii ina maana kwamba anazo nguvu kushinda mauti juu yako ili usife kama utamkaribisha maishani mwako. Hautakufa bali utaishi uyasimulie matendo makuu ya Mungu.
6. ALIPAA MBINGUNI NA ATARUDI TENA: Yesu alipaa mbinguni, lakini kiroho anaishi na wale wanaomwamini hapa duniani pia. atarudi tena kuwachukua wale wanaomwamini, na kuihukumu dunia. Biblia inasema dhambi ya kwanza ambayo watu watahukumiwa nayo ni ile ya kumkataa/kutomwamini Mwana wa Mungu (Yesu Kristo wa Nazareth), hii ni kwasababu alitoa gharama kubwa sana ya uhai wake lakini watu walimkataa. kataa usiwe na dhambi hii. pia ameenda kuandaa makao ili pale alipo nasi tuwepo baada ya hukumu pale atakapo wagawanya watu kama vile mchungaji agawanyavyo koondoo na mbuzi, kondoo mkono wa kulia na mbuzi mkono wa kushoto, wengine wapate uzima wa milele na wengine aibu na kudharauliwa milele. Amini nakuambieni, ukiona leo hii u mzima, unapumua, unao uwezo kuongea, jua Mungu anakupenda. Neno la Mungu linasema
WEMA WA MUNGU UNATUHIFADHI ILI PENGINE MAISHA YETU YATABADILIKA, tunamtenda dhambi Mungu anatuangalia tu sio kwamba hakasiriki au hana uwezo kutusambaratisha, anatuacha tu kutupatia chance nyingine pengine tutabadilika kwasababu Mungu anachukia kifo cha mtu mwenye dhambi anataka wote watubu na kuacha uovu ili wasiangamie. hivyo unakumbushwa tafakari maneno haya, mpokee Yesu awe Bwana na Mwokozi wa Maisha yako ingali chance ipo, kuna watu wapo ICU hata kunyanyua ulimi waseme Yesu nisamehe dhambi au nipokee huko mbinguni haawana, na ili uokoke lazima ukiri kwa kinywa chako na uamini moyoni. kuna nguvu na mlango katika ukiri. hivyo leo nenda chumbani kwako, piga magoti, kama hujaokoka tafuta waliookoka wakusaidie maombi, kama tayari na unajujia hueleweki vizuri piga magoti omba kwa moyo wako woote wa ndani kabisa, ongea na Mungu na dhamiria kuacha uovu.
7. JINA LA YESU HALIFANYI KAZI KWA WADHAMBI: kuna kipindi raia wa kawaida kadhaa waliimitate yale yanayofanywa na mitume/paulo, wakawa wanaenda kwa wenye mapepo wanasema "kwa jina la Yesu yule anayehubiriwa na kina Paulo toka" mapepo hayakuwasikia, yaliwasambaratisha wengine waliondoka bila nguo. hii ina maana kwamba, yote yaliyosemwa hapo juu huna haki nayo na hayatafanya kazi kwako kama hautakuwa part and parcel of Yesu, lazima uungane naye akae moyoni mwako ndipo utakuwa na mamlaka ya kutumia Jina la Yesu na Damu ya Yesu. hii inadhihirishwa na watu wa dinia mbao wamesoma sana dini, wamekariri sana mistari ya Biblia, wamesoma miaka mingi seminari huko lakini hawana nguvu za Mungu kwasababu Mungu hayupo mioyoni mwao. kwahiyo ili uinjoy matunda ya Jina la Yesu na Damu ya Yesu, lazima uokoke, ujazwe Roho Mtakatifu na uishi maisha matakatifu, usiishi kidini, usiwe farisayo, ishi Kiroho, abudu kiroho, imba kiroho etc.
MUNGU AWABARIKI,
MWENYE SIKIO NA ASIKIE, NIMENAWA MIKONO, DAMU YENU HAITADAIWA JUU YANGU. MBARIKIWE.