Ulimwengu ya mafundisho bila ya mateso pia ipo, watu wengi wanaishi maisha yao vizuri bila kujua shida - lakina kuna mambo mengine unayashika vizuri ukiyapitia mateso na changamoto. A father with an obese child might put him through a harsh regime of strict diet, rigid exercises and strict discipline. This doesn't mean that the father is punishing the child, it's more out of his concern for the welfare of the child. It's same with God, at times he takes extreme measures to bring his creation on the right track! Zote dhiki na faraja zinatoka kwa Mungu na sisi tukiwa na dhiki tunapiga magoti na kutubu na tukiwa na faraja pia tunapiga magoti na kushukuru! Kwako wewe Mungu ni sawa akileta faraja, lakini hafai akileta dhiki!
I must admit it's a total wastage of time kujadiliana na wewe!!!! Hii hoja ya kuwepo kwa Mungu imeshajadiliwa na wadau wengi humu na wengi wamekushinda. Lakini kila unapoona unatapatapa basi unaleta baseless, irrelevant arguments - eti unajua maana ya hii au kile?? Umesoma kitabu hiki? (safuher)kasome halafu njoo kujadili na mimi! Unajua square root ya mbili? (zurri) Hata sijui inaconnection gani na uwepo wa Mungu? Ya kushangaza baada ya kupigwa buti na hoja nzito za wadau, bado unajitokeza na hoja zile zile zilizochoka na zisizonamshiko. Well, you can fool some of the people some of the time, but you can't fool all the people all the time. While we can't deny you your right to express yourself but we can certainly choose to ignore you, and that's what I've decided to do!!
Unajibu swali ambalo sijauliza, wakati nililouliza hujajibu.
Sijauliza kama ulimwengu wa mafundisho bila mateso upo.
Pia, huo unaousema upo huna ushahidi wala uthibitisho kama upo.
Unaposema ulimwengu wa mafunzo bila mateso upo, kwa sababu watu wengi wanaishi Maisha yao vizuri bila kujua shida, hujaelewa swali langu na wala hujaelewa shida ni nini.
1. Hujaelewa swali langu ni nini, kwa sababu unafikiri kwamba, kukiwa na watu wengi wanaishi bila mateso, katika ulimwengu ambao watu wengi wanaishi bila mateso, basi una ulimwengu usio na mateso.
Hapo umekosa uelewa wa set theory, kwamba, ukiondoa mateso yote ya ulimwengu, ukambakisha mbu mmoja tu anayesababisha malaria, basi ulimwengu mzima umeingiliwa na mateso, na huwezi kusema huu ulimwengu hauna mateso.
2. Hujaelewa mateso ni nini, kwa sababu mtu yeyote ni lazima akutane na mateso katika ulimwengu.
Ataugua, atafiwa na anaowapenda, atakuwa na njaa, atashindwa kwenda anapotaka kwenda, ataonewa, atakabiliwa na mawazo kuhusu kifo, atakutana na majanga ya asili ,atatamani asichoweza kupata, atapata asichotaka kupata, atakufa.
Hakuna mtu hata mmoja atakayeepuka mateso haya ya dunia.
Kwangu hata ukisema habari za peponi ni hadithi tu. Na wewe hujathibitisha vinginevyo.
Nakuuliza kuhusu ulimwengu huu tuuonao na kuujua wote.
Mungu wako alishindwa kuuumba ulimwengu huu uwe na mafunzo bila mateso?
Yani unamfananisha Mungu na baba anayehitaji kumshurutisha mwanawe vikali ili mtoto aepuke unene uliozidi kiasi?
Unaelewa huyu baba hana control kuhusu ulimwengu, na Mungu unayemsema ana control zote kuhusu ulimwengu?
Unaelewa huyu baba ana excuse ya kusema ninemuamrisha mwanangu afunge kwa sababu nampenda, namtaka afunge ili apunguze uzito.Sina control juu ya process ya kupunguza unene zaidi ya za kiutu. Mtoto atasikia njaa, lakini kusikia njaa kutamsaidia kupunguza uzito. Sina jinsi ya kumfanya apunguze uzito bila kusikia njaa.
Unaelewa Mungu muweza yote hapo anaweza kumfanya mtu apungue uzito bila kufunga, indeed angeweza kuumba ulimwengu ambao uzito uliopita kiasi hauwezekani kabisa kuwepo?
Sasa kama Mungu aliweza kuumba ulimwengu ambao haiwezekani mtu kuwa na uzito uliozidi kiasi, kwa nini hajaumba hivyo na kaumba vinginevyo mpaka anashurutisha waja wake kufunga ili tu wapungue uzito?
Mungu wako alishindwa kuuumba ulimwengu huu uwe wa mafunzo bila mateso?