Ifahamu Wizara ya Usalama wa taifa ya China na majukumu yake kwa nchi hiyo kubwa Duniani

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440

View: https://www.youtube.com/watch?v=j1UH7Yn6gSg

Hii ni makala ya pili inozungumzia nchi ambazo zina wizara kamili inoshughulikia Usalama wa taifa.

Wiki ilopita nilizungumzia umuhimu wa raisi ajae kufikiria kuanzisha wizara ya Usalama wa taifa ambayo itashughulikia usalama wa nchi na mipaka yake na kuhakikisha mikoa yote nchini ina mkono wa wizara hiyo na waziri wake atatoka katika moja ya vyombo ya ulinzi na usalama khasa jeshini.

China wana wizara ya usalama wa Taifa au Ministry of State Security ambayo ilianzishwa mwaka 1983, ikiasisiwa kutoka idara mbalimbali tokea miaka ya 1936, 1949, na mwaka 1955 ambapo shughuli za ujasusi zilikuwa chini ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China cha CCP kikiwa na idara ziloitwa Central Special Branch, idara ya jamii ya kamati kuu, idara ya uchunguzi ya kamati kuu hadi idara hizo zote zilipounganishwa mwaka 1983 na ilokuwa wizara ya usalama wa raia kuwa wizara kamili ya usalama wa taifa.

Wizara hii ya Usalama wa taifa ina watumishi wapatao 110,000 idadi inotajwa na mtafiti wa taarifa za kijasusi Alex W. Joske ambae kitaalam ni mshauri elekezi wa masuala ya athari huchunguza shughuli za kijasusi za chama cha kikomunisti. Pia kwa mujibu wa FBI kupitia mwandishi James Calder Walton ambae pia ni mwanahistoria za kijasusi na masuala ya usalama wa taifa yeye asema kuwa Wizara hiyo ya usalama wa China ina watumishi wapatao 800,000 ambao wametawanyika katika mikoa yote ya China.

Wizara hii yaundwa na waziri ambae ana manaibu watatu na afisa mtendaji ambae asimamia idara ya siasa wizarani hapo. Wizara hiyo yawajibika moja kwa moja kamisheni maalum mbili moja ya masuala ya usalama na ingine ya masuala ya siasa na sheria na hii ni kwa ajili ya kutoa miongozo kwa wizara hii pale inapokumbana na changamoto za aina hiyo. Chini kabisa ya muundo huo pana ofisi inoshughulikia usalama wa taifa pamoja na polisi wa Usalama wa taifa au State Security Police.

Pamoja na kwamba wizara hii imekumbwa na shutuma za kushughulikia wanaharakati wa kisiasa wa ndani na nje ya China lakini wizara hii ina mkono mrefu wa kuweka kufanya shughuli zake za kijasusi katika kiwango kikubwa ikitumia wahandisi na idara ingine iitwayo United Front Work ambayo shughuli zake kuu ni kuhakikisha Wachina walioko nje yaani Diaspora washirikishwa ili kuhakikisha maslahi ya China yaliyipo nje ya China iwe kisiwani HongKong, Taiwan na mataifa mengine yalindwa kwa gharama yoyote ile.

Jambo jingine la muhimu hapa ni kwamba Wizara hii ya Usalama wa taifa iko wazi kwa wananchi wa China na mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kama "WeChat" kusisitiza ujumbe wa kukumbushia umuhimu wa wananchi kuchukulia suala la usalama kuwa ni wajibu wao. Hata mabango mbalimbali ya matangazo na vituo vya usafiri huwa na alama ya wizara hiyo ikijitambulisha kwa wananchi.

Kipengele cha 4 (Article 4) cha Sheria ya uhalifu charuhusu maofisa wa wizara hiyo kukamata na kuweka chini ya ulinzi raia kwa makosa yanohusu usalama wa taifa chini ya uangalizi wa mahakama na kamisheni nilozitaja hapo juu. Pia Sheria ya Usalama wa taifa yawapa maofisa wa usalama uhalali wa kufanya shughuli za kijasusi ndani na nje ya China na hata kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi wale wanotuhumiwa kuvujisha taarifa nyeti na za siri zinohusu taifa la China.

Wazo la kuanzishwa kwa wizara ya Usalama wa taifa lililetwa na aliekuwa waziri mkuu bwana Zhao Ziyang na waziri wa usalama wa raia bwana Liu Fuzhi. Baadae katika mkutano mkuu wa sita wa chama cha CCP Wizara kamili ya Usalama wa Taifa ilianzishwa rasmi mwaka 1983 waziri wake wa kwanza akiwa bwana Ling Yun. Pamoja na kwamba wizara hii yafuata mlengo wa chama cha CCP na itikadi, lakini bado wizara ya usalama wa taifa haipo chini ya chama hicho bali chini ya baraza la Usalama wa taifa.

Kutokana na point hiyo hapo juu, mabadiliko ya katiba ya Tanzania yaweza kabisa kutenganisha shughuli za Wizara ya Usalama wa taifa ya Tanzania na zile za chama cha CCM na kukifanya chombo hicho kuwajibika na kuwajibishwa na baraza maalum la ulinzi na usalama na pia kuongozwa na sheria za uhalifu, mahakama pamoja na Bunge ambalo litaridhia waziri wake ambae jina lake litajadiliwa baada ya kupendekezwa na raisi.

Majukumu ya waziri wa usalama wa taifa.

Waziri wa usalama wa taifa atafanya mabadiliko ya kimuundo wa idara ya Usalama wa taifa kwa kuiondoa katika mikono ya ofisi ya raisi na kutoka mikono ya chama tawala cha CCM ili kuipa wizara nafasi ya kujivua gamba la uCCM, gamba la Ufisadi na gamba la matumizi mabaya ya ofisi na mali za umma. Waziri ataendeleza vipaji vya maofisa usalama na kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania ina wakurugenzi wenye sifa na weledi wa kazi.

Waziri pia atawezesha kuundwa kwa miongozo, kanuni na taratibu mbalimbali likiwemo suala la Vetting kwa wale wanopendekezwa na raisi kushika nafasi mbalimbali katika serikali. Wizara italeta ukaribu na wananchi ili kurahisisha ushirikiano na kuwapa fursa wananchi kufahamu shughuli za wizara kwa kushirikishwa katika mashindano kama vile sayansi na hesabu. Maofisa wapya na watarajiwa watakuwa chini ya uangalizi kabla ya kuajiriwa na wizara kupitia vyuo vikuu, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na jeshi kwa kupitia mitihani maalum.

Waziri pia atakuwa na majukumu ya kuhakikisha kunaundwa idara ndogo ambazo zitaangalia maeneo nyeti kama vile Chakula (Food Security) Nishati ( Energy Security) Afya ( Health Security Agency) pamoja na usalama wa miundombinu na mitandao au cuber security and infrastructure agency. Kwa mfano nchi ya Burkina Faso mwaka 2020 ilikuja na sera ya taifa ya usalama au Burkina Faso National Security Policy ambayo ambayo imeweka miongozo na malengo ambayo yaelezea kulinda maslahi ya taifa na pia usalama wa mtu au human security ambapo usalama wa chakula, afya, uchumi, mazingira jamii na hata siasa vyaangaliwa.

Bila kusahau bajeti ya wizara, waziri wa usalama wa taifa ataandaa bajeti ya wizara na miswada mbalimbali na kuifikisha bungeni kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kuwa sheria kamili.

Vyanzo vilotumika kutayarisha mada hii:

African Confidential, African security Analysis, China Leadership Monitor, Economictimes.indiatimes.com na waandishi wa habari na historia za ujasusi Alex Joske na kitabu chake cha Spies and Lies - How China Greatest Covert Operations Fooled the World, kilochapishwa mwaka 2022 na Calder Walton ambae mwaka 2023 alichapisha kitabu chake kiitwacho SPIES- The Epic Intelligence War Between East and West.
 
mkuu kabla ya kuwa na wizara hii ya usalama kwanza kufanyike reforms maeneo mengi kuanzia bungeni,katiba..kwa sababu hapa kwetu Waziri lazima awe mbunge na ili uendelee kuwa mbunge lazima uwe na chama iwapo chama kikikufukuza basi unapoteza vyote..na sheria hizi ndio limefanya bunge lisiwe na meno.. kwahiyo uyo waziri unayemsema kwenye andiko hana kinga yoyote akienda kinyume na anachotaka rais ikiwa tu waziri ni mzalendo na rais muhuni anayependa madaraka..hivyo huwezi kuweka kitu kisafi( idara yenye weledi na uzalendo ) katikati ya uozo na uvundo uliojaa sasa lazima kwanza kiwekwewe msingi imara na kinga ya utendaji kikatiba na kisheria hapo ndio utaona matokeo chanya..na sidhani kama hayo mazuri tutayapata chini ya utawala wa CCM hii
 
Mkuu, ukisoma kuelekea mwisho wa mada nimeelezea mabadiliko ya katiba.
 
Tanzania ina hyo wizara kuanzia enzi mkapa
Wizara hyo ipo hadi sasa kwa jina lingine
Sema majukumu yake hayajawekwa waz
 
Mkuu, hiyo wizara kama ipo tokea wakati wa hayati Mkapa ilitumia jina lipi.

Na hilo jina jingine la sasa ni lipi?

Kulingana na madadiliko ya kidunia majukumu ya taasisi kama hii ni budi kuwekwa wazi kwa wananchi wake kwani hawataathri chochote.

Hata wakati wa kutafuta waajiriwa wapya kwa wenzetu huko nje nafasi hutangazwa isipokuwa ukiishachaguliwa hapo ndipo siri huanza na hata familia isifahamu shughuli zako.

Huko kujifichaficha ndo kwatoa mwanya kujipenyeza kwa watu wasojulikana na makundi ya wahuni.

Kwa sababu huko juu hakuna uangalizi wa kisheria na kikatiba.
 
Kulikuwa na waziri wa nchi ofisi ya rais(usalama wa taifa) na waziri wake alikuwa dr hassy kitine kipindi hcho akiwa mbunge kutokea jimbo la makete..
Nina wasi wasi kuna wizara kama wizara ya kazi maalum, wizara ya utawala ubora bila shaka znashughulika na majukumu hayo (ni wizara fiche kimajukumu sy lazma ziitwe hvo moja kwa moja)
 
Marekani ina mashirika zaidi ya Kijasusi zaid ya 10

Nawaambiaga watu wa CCM na Serikali ukitulinganisha na mataifa mengine sisi ni wanamgambo
Wingi wa mashirika ya kijasusi siyo uimara wa kijasusi/majukumu yake..
We ndo mgambo, siyo watanzania wote bali wewe ndo mgambo
 
Ujasusi maana yake ya msingi ni "Intelligence" ukiona Serikali inafikia hatua ya kungia chombo cha habari taarifa isienee ujue hakuna uongozi na hakuna hiyo "Intelligence"
 
Kila nchi ina utaratibu wake wa kujiongoza na si kufanana kama mayai.
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=j1UH7Yn6gSg

Hii ni makala ya pili inozungumzia nchi ambazo zina wizara kamili inoshughulikia Usalama wa taifa.

Wiki ilopita nilizungumzia umuhimu wa raisi ajae kufikiria kuanzisha wizara ya Usalama wa taifa ambayo itashughulikia usalama wa nchi na mipaka yake na kuhakikisha mikoa yote nchini ina mkono wa wizara hiyo na waziri wake atatoka katika moja ya vyombo ya ulinzi na usalama khasa jeshini.

China wana wizara ya usalama wa Taifa au Ministry of State Security ambayo ilianzishwa mwaka 1983, ikiasisiwa kutoka idara mbalimbali tokea miaka ya 1936, 1949, na mwaka 1955 ambapo shughuli za ujasusi zilikuwa chini ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China cha CCP kikiwa na idara ziloitwa Central Special Branch, idara ya jamii ya kamati kuu, idara ya uchunguzi ya kamati kuu hadi idara hizo zote zilipounganishwa mwaka 1983 na ilokuwa wizara ya usalama wa raia kuwa wizara kamili ya usalama wa taifa.

Wizara hii ya Usalama wa taifa ina watumishi wapatao 110,000 idadi inotajwa na mtafiti wa taarifa za kijasusi Alex W. Joske ambae kitaalam ni mshauri elekezi wa masuala ya athari huchunguza shughuli za kijasusi za chama cha kikomunisti. Pia kwa mujibu wa FBI kupitia mwandishi James Calder Walton ambae pia ni mwanahistoria za kijasusi na masuala ya usalama wa taifa yeye asema kuwa Wizara hiyo ya usalama wa China ina watumishi wapatao 800,000 ambao wametawanyika katika mikoa yote ya China.

Wizara hii yaundwa na waziri ambae ana manaibu watatu na afisa mtendaji ambae asimamia idara ya siasa wizarani hapo. Wizara hiyo yawajibika moja kwa moja kamisheni maalum mbili moja ya masuala ya usalama na ingine ya masuala ya siasa na sheria na hii ni kwa ajili ya kutoa miongozo kwa wizara hii pale inapokumbana na changamoto za aina hiyo. Chini kabisa ya muundo huo pana ofisi inoshughulikia usalama wa taifa pamoja na polisi wa Usalama wa taifa au State Security Police.

Pamoja na kwamba wizara hii imekumbwa na shutuma za kushughulikia wanaharakati wa kisiasa wa ndani na nje ya China lakini wizara hii ina mkono mrefu wa kuweka kufanya shughuli zake za kijasusi katika kiwango kikubwa ikitumia wahandisi na idara ingine iitwayo United Front Work ambayo shughuli zake kuu ni kuhakikisha Wachina walioko nje yaani Diaspora washirikishwa ili kuhakikisha maslahi ya China yaliyipo nje ya China iwe kisiwani HongKong, Taiwan na mataifa mengine yalindwa kwa gharama yoyote ile.

Jambo jingine la muhimu hapa ni kwamba Wizara hii ya Usalama wa taifa iko wazi kwa wananchi wa China na mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kama "WeChat" kusisitiza ujumbe wa kukumbushia umuhimu wa wananchi kuchukulia suala la usalama kuwa ni wajibu wao. Hata mabango mbalimbali ya matangazo na vituo vya usafiri huwa na alama ya wizara hiyo ikijitambulisha kwa wananchi.

Kipengele cha 4 (Article 4) cha Sheria ya uhalifu charuhusu maofisa wa wizara hiyo kukamata na kuweka chini ya ulinzi raia kwa makosa yanohusu usalama wa taifa chini ya uangalizi wa mahakama na kamisheni nilozitaja hapo juu. Pia Sheria ya Usalama wa taifa yawapa maofisa wa usalama uhalali wa kufanya shughuli za kijasusi ndani na nje ya China na hata kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi wale wanotuhumiwa kuvujisha taarifa nyeti na za siri zinohusu taifa la China.

Wazo la kuanzishwa kwa wizara ya Usalama wa taifa lililetwa na aliekuwa waziri mkuu bwana Zhao Ziyang na waziri wa usalama wa raia bwana Liu Fuzhi. Baadae katika mkutano mkuu wa sita wa chama cha CCP Wizara kamili ya Usalama wa Taifa ilianzishwa rasmi mwaka 1983 waziri wake wa kwanza akiwa bwana Ling Yun. Pamoja na kwamba wizara hii yafuata mlengo wa chama cha CCP na itikadi, lakini bado wizara ya usalama wa taifa haipo chini ya chama hicho bali chini ya baraza la Usalama wa taifa.

Kutokana na point hiyo hapo juu, mabadiliko ya katiba ya Tanzania yaweza kabisa kutenganisha shughuli za Wizara ya Usalama wa taifa ya Tanzania na zile za chama cha CCM na kukifanya chombo hicho kuwajibika na kuwajibishwa na baraza maalum la ulinzi na usalama na pia kuongozwa na sheria za uhalifu, mahakama pamoja na Bunge ambalo litaridhia waziri wake ambae jina lake litajadiliwa baada ya kupendekezwa na raisi.

Majukumu ya waziri wa usalama wa taifa.

Waziri wa usalama wa taifa atafanya mabadiliko ya kimuundo wa idara ya Usalama wa taifa kwa kuiondoa katika mikono ya ofisi ya raisi na kutoka mikono ya chama tawala cha CCM ili kuipa wizara nafasi ya kujivua gamba la uCCM, gamba la Ufisadi na gamba la matumizi mabaya ya ofisi na mali za umma. Waziri ataendeleza vipaji vya maofisa usalama na kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania ina wakurugenzi wenye sifa na weledi wa kazi.

Waziri pia atawezesha kuundwa kwa miongozo, kanuni na taratibu mbalimbali likiwemo suala la Vetting kwa wale wanopendekezwa na raisi kushika nafasi mbalimbali katika serikali. Wizara italeta ukaribu na wananchi ili kurahisisha ushirikiano na kuwapa fursa wananchi kufahamu shughuli za wizara kwa kushirikishwa katika mashindano kama vile sayansi na hesabu. Maofisa wapya na watarajiwa watakuwa chini ya uangalizi kabla ya kuajiriwa na wizara kupitia vyuo vikuu, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na jeshi kwa kupitia mitihani maalum.

Waziri pia atakuwa na majukumu ya kuhakikisha kunaundwa idara ndogo ambazo zitaangalia maeneo nyeti kama vile Chakula (Food Security) Nishati ( Energy Security) Afya ( Health Security Agency) pamoja na usalama wa miundombinu na mitandao au cuber security and infrastructure agency. Kwa mfano nchi ya Burkina Faso mwaka 2020 ilikuja na sera ya taifa ya usalama au Burkina Faso National Security Policy ambayo ambayo imeweka miongozo na malengo ambayo yaelezea kulinda maslahi ya taifa na pia usalama wa mtu au human security ambapo usalama wa chakula, afya, uchumi, mazingira jamii na hata siasa vyaangaliwa.

Bila kusahau bajeti ya wizara, waziri wa usalama wa taifa ataandaa bajeti ya wizara na miswada mbalimbali na kuifikisha bungeni kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kuwa sheria kamili.

Vyanzo vilotumika kutayarisha mada hii:

African Confidential, African security Analysis, China Leadership Monitor, Economictimes.indiatimes.com na waandishi wa habari na historia za ujasusi Alex Joske na kitabu chake cha Spies and Lies - How China Greatest Covert Operations Fooled the World, kilochapishwa mwaka 2022 na Calder Walton ambae mwaka 2023 alichapisha kitabu chake kiitwacho SPIES- The Epic Intelligence War Between East and West.

Una idea nzuri ila kwa tanzania hii ya akina samia et al., jua halitowezekana na hata kama hiyo wizara ikundwa jua kabisa lazima atawekwa kada wa ccm na akiwekwa kada yataendelea haya haya tunayo yaona.

Kama tukitaka iwezekane ni vyema kwanza vyama vyote vya siasa vifutwe kwenye hii nchi hasa ccm. Alafu tuanze mwanzo kwa kuhakikisha hakuna mtu aliye wahi kuwa kada wa ccm anashika uongozi popote!

Sasa ukiangalia hii ni kwamba hilo jambo haliwezekaniki labda miaka 100 au 1000 ijayo.
 
Marekani ina mashirika zaidi ya Kijasusi zaid ya 10

Nawaambiaga watu wa CCM na Serikali ukitulinganisha na mataifa mengine sisi ni wanamgambo
USA na shirika yake yapo 18 yote yanadili na Usalama
 
View: https://www.youtube.com/watch?v=j1UH7Yn6gSg

Hii ni makala ya pili inozungumzia nchi ambazo zina wizara kamili inoshughulikia Usalama wa taifa.

Wiki ilopita nilizungumzia umuhimu wa raisi ajae kufikiria kuanzisha wizara ya Usalama wa taifa ambayo itashughulikia usalama wa nchi na mipaka yake na kuhakikisha mikoa yote nchini ina mkono wa wizara hiyo na waziri wake atatoka katika moja ya vyombo ya ulinzi na usalama khasa jeshini.

China wana wizara ya usalama wa Taifa au Ministry of State Security ambayo ilianzishwa mwaka 1983, ikiasisiwa kutoka idara mbalimbali tokea miaka ya 1936, 1949, na mwaka 1955 ambapo shughuli za ujasusi zilikuwa chini ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China cha CCP kikiwa na idara ziloitwa Central Special Branch, idara ya jamii ya kamati kuu, idara ya uchunguzi ya kamati kuu hadi idara hizo zote zilipounganishwa mwaka 1983 na ilokuwa wizara ya usalama wa raia kuwa wizara kamili ya usalama wa taifa.

Wizara hii ya Usalama wa taifa ina watumishi wapatao 110,000 idadi inotajwa na mtafiti wa taarifa za kijasusi Alex W. Joske ambae kitaalam ni mshauri elekezi wa masuala ya athari huchunguza shughuli za kijasusi za chama cha kikomunisti. Pia kwa mujibu wa FBI kupitia mwandishi James Calder Walton ambae pia ni mwanahistoria za kijasusi na masuala ya usalama wa taifa yeye asema kuwa Wizara hiyo ya usalama wa China ina watumishi wapatao 800,000 ambao wametawanyika katika mikoa yote ya China.

Wizara hii yaundwa na waziri ambae ana manaibu watatu na afisa mtendaji ambae asimamia idara ya siasa wizarani hapo. Wizara hiyo yawajibika moja kwa moja kamisheni maalum mbili moja ya masuala ya usalama na ingine ya masuala ya siasa na sheria na hii ni kwa ajili ya kutoa miongozo kwa wizara hii pale inapokumbana na changamoto za aina hiyo. Chini kabisa ya muundo huo pana ofisi inoshughulikia usalama wa taifa pamoja na polisi wa Usalama wa taifa au State Security Police.

Pamoja na kwamba wizara hii imekumbwa na shutuma za kushughulikia wanaharakati wa kisiasa wa ndani na nje ya China lakini wizara hii ina mkono mrefu wa kuweka kufanya shughuli zake za kijasusi katika kiwango kikubwa ikitumia wahandisi na idara ingine iitwayo United Front Work ambayo shughuli zake kuu ni kuhakikisha Wachina walioko nje yaani Diaspora washirikishwa ili kuhakikisha maslahi ya China yaliyipo nje ya China iwe kisiwani HongKong, Taiwan na mataifa mengine yalindwa kwa gharama yoyote ile.

Jambo jingine la muhimu hapa ni kwamba Wizara hii ya Usalama wa taifa iko wazi kwa wananchi wa China na mara nyingi hutumia mitandao ya kijamii kama "WeChat" kusisitiza ujumbe wa kukumbushia umuhimu wa wananchi kuchukulia suala la usalama kuwa ni wajibu wao. Hata mabango mbalimbali ya matangazo na vituo vya usafiri huwa na alama ya wizara hiyo ikijitambulisha kwa wananchi.

Kipengele cha 4 (Article 4) cha Sheria ya uhalifu charuhusu maofisa wa wizara hiyo kukamata na kuweka chini ya ulinzi raia kwa makosa yanohusu usalama wa taifa chini ya uangalizi wa mahakama na kamisheni nilozitaja hapo juu. Pia Sheria ya Usalama wa taifa yawapa maofisa wa usalama uhalali wa kufanya shughuli za kijasusi ndani na nje ya China na hata kuwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi wale wanotuhumiwa kuvujisha taarifa nyeti na za siri zinohusu taifa la China.

Wazo la kuanzishwa kwa wizara ya Usalama wa taifa lililetwa na aliekuwa waziri mkuu bwana Zhao Ziyang na waziri wa usalama wa raia bwana Liu Fuzhi. Baadae katika mkutano mkuu wa sita wa chama cha CCP Wizara kamili ya Usalama wa Taifa ilianzishwa rasmi mwaka 1983 waziri wake wa kwanza akiwa bwana Ling Yun. Pamoja na kwamba wizara hii yafuata mlengo wa chama cha CCP na itikadi, lakini bado wizara ya usalama wa taifa haipo chini ya chama hicho bali chini ya baraza la Usalama wa taifa.

Kutokana na point hiyo hapo juu, mabadiliko ya katiba ya Tanzania yaweza kabisa kutenganisha shughuli za Wizara ya Usalama wa taifa ya Tanzania na zile za chama cha CCM na kukifanya chombo hicho kuwajibika na kuwajibishwa na baraza maalum la ulinzi na usalama na pia kuongozwa na sheria za uhalifu, mahakama pamoja na Bunge ambalo litaridhia waziri wake ambae jina lake litajadiliwa baada ya kupendekezwa na raisi.

Majukumu ya waziri wa usalama wa taifa.

Waziri wa usalama wa taifa atafanya mabadiliko ya kimuundo wa idara ya Usalama wa taifa kwa kuiondoa katika mikono ya ofisi ya raisi na kutoka mikono ya chama tawala cha CCM ili kuipa wizara nafasi ya kujivua gamba la uCCM, gamba la Ufisadi na gamba la matumizi mabaya ya ofisi na mali za umma. Waziri ataendeleza vipaji vya maofisa usalama na kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania ina wakurugenzi wenye sifa na weledi wa kazi.

Waziri pia atawezesha kuundwa kwa miongozo, kanuni na taratibu mbalimbali likiwemo suala la Vetting kwa wale wanopendekezwa na raisi kushika nafasi mbalimbali katika serikali. Wizara italeta ukaribu na wananchi ili kurahisisha ushirikiano na kuwapa fursa wananchi kufahamu shughuli za wizara kwa kushirikishwa katika mashindano kama vile sayansi na hesabu. Maofisa wapya na watarajiwa watakuwa chini ya uangalizi kabla ya kuajiriwa na wizara kupitia vyuo vikuu, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na jeshi kwa kupitia mitihani maalum.

Waziri pia atakuwa na majukumu ya kuhakikisha kunaundwa idara ndogo ambazo zitaangalia maeneo nyeti kama vile Chakula (Food Security) Nishati ( Energy Security) Afya ( Health Security Agency) pamoja na usalama wa miundombinu na mitandao au cuber security and infrastructure agency. Kwa mfano nchi ya Burkina Faso mwaka 2020 ilikuja na sera ya taifa ya usalama au Burkina Faso National Security Policy ambayo ambayo imeweka miongozo na malengo ambayo yaelezea kulinda maslahi ya taifa na pia usalama wa mtu au human security ambapo usalama wa chakula, afya, uchumi, mazingira jamii na hata siasa vyaangaliwa.

Bila kusahau bajeti ya wizara, waziri wa usalama wa taifa ataandaa bajeti ya wizara na miswada mbalimbali na kuifikisha bungeni kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya kuwa sheria kamili.

Vyanzo vilotumika kutayarisha mada hii:

African Confidential, African security Analysis, China Leadership Monitor, Economictimes.indiatimes.com na waandishi wa habari na historia za ujasusi Alex Joske na kitabu chake cha Spies and Lies - How China Greatest Covert Operations Fooled the World, kilochapishwa mwaka 2022 na Calder Walton ambae mwaka 2023 alichapisha kitabu chake kiitwacho SPIES- The Epic Intelligence War Between East and West.

Huku DG-EYE-S wetu NTU WA DILI.
 
Back
Top Bottom