Ifike hatua, wanawake muwe na huruma dhidi yetu wanaume

Wale wasumbufu sumbufu...michepuko kila kona..kudanganya danganya wadada kumi kidogo...hao lazima walipuke...
 
Eeh tulieni dawa iwaingie, mngechagua wenye uzuri wa kawaida yasingewakuta, mnachagua akina sanchoka , wacha wawanyooshe.
Kama una uzuri wa kawaida ni DM tufanye jambo.
 
Huu ni ukweli unaoumiza ,ila ni kukomaa tu. Japo kama Mwanaume unaweza ukawa ushakufa at age ndogo lkn ukasubiria miaka mingi kuja kuzikwa.
Lakin majanga meng mnayachuma wenyewe jamani. Hivi mngetulia mngeyapata wapi haya majanga?? Hata kama ni mechi za nje chezeni mara moja moja ikiwabidi...lakin mmegeuza sheria. Mmepafanya ibada huko nje. Na mbaya zaidi mnajisifu wazi wazi. Kazi mnayo..
 
Dawa ni kuwakataa tu,tafuta mke asiyekuwa na mambo mengi form four au six hata la saba owa muhimu msikilizane ndani ya nyumba.

Mke anayekusikiliza hawezi kukuendea kwa waganga kutafuta namna ya kula vyako zaidi atakuwa anakushauri cha kufanya maisha yenu na watoto yasogee hata akidokoa ni kwa ajili ya watoto siyo vinginevyo.
 
Hio huruma unayo waomba kaka sahau tu, tuendelee tu kuishi nao ki akili. Wanawake wana huruma kwa watoto wao tu. OVER!
 
Mke hafanyi haya, shida ni hawa tunaokutana nao barabarani,michepuko
 
Tunatulia, ila dawa zenu ndio hazitutulizi. Zinazidi kutupeperusha, mnatulipua 😅😅
 
Ni vile tu wanaume tunaponzwa na tamaa, kuepusha yote hayo tafta pisi yako moja kali itunze piga show ya maana hizi mambo za kurogwa ni outcomes ya uzinzi
 
Mwanamke anaenda kwa mganga kwasababu ya mapenzi mwanaume anaenda kwasababu ya kazi full stop

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…