Ifike mahala Watanzania tuache kusomea ualimu, supply imekuwa kubwa mno kuliko demand

Unaweza summarize kidogo uzi wako? Inaonekana una hoja ila uzi wako ni mrefu sana.
 
Marekani imeendelea kwa TEHAMA haifanyi hivyo. Ukiambiwa uwiano ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 40 maana yake sio kufundisha tu, mtaala wa elimu una mambo mengi.
 
Mkoa wa Geita peke yake una uhaba wa waalimu wa shule za msingi na sekondari elfu 7 (7000).

Serikali haijaamua kuajiri.
 
Umeandika dhania tu, hivi bila huo ualimu ungeweza kuwasilisha mawazo yako hapa? Jamii inayoubeza ualimu katika dunia hii ya tatu ni ya kusikitikia sana. Wanaofundisha uko VETA siyo walimu? Suluhisho la ajira siyo kuzalisha bidhaa tu, bila mzunguko mzuri wa fedha kwa wananchi. Wanaojilipa mifungu minono wapo, watoto wao wanasoma ng'ambo elimu hii hii inayobezwa hapa nchini. Na wanaporudi mnaanza kuwatafutia idara kwa kuwaundia mikoa mipya, na wilaya mpya, wapate kula keki ya taifa kwa kijiko. Halafu, mna wahadaa watoto wetu, wajiajiri kwa kusoma, VETA, utadhani gharama za kununua vifaa mnawapa wakiisha hitimu, ni watoto wengi nawaona wako vijiweni baada ya kuhitimu VETA, kwa kukosa mtaji na vifaa vya kujiajiri, ambavyo jumla yake siyo chini ya shilingi milioni moja na zaidi za Kitanzania. Yaani mnatengeneza tatizo juu ya tatizo lingine baadala ya kuyatatua. Muda ni mwalimu mzuri na umuhimu somo lake ujulikana baadae. Somalia, ni mfano mzuri, kwa wote wajipendeleao na koo zao wawapo madarakani.
 
Spot on....vyuo vianzishe vibadili mitaala ya wakati wa uhuru ambapo nchi ilikuwa inatafuta wafanyakazi wa serikali na mfumo.ulikuwa ujamaa, sasa waangalie zaidi skills za mtu kujiajiri na sio kuajiriwa.

Bila vyuo kubadili mfumo kwakweli vijana wanaendelea kuwa wafungwa wa fikra kisa degree....
 
Watazuiaje wakati wao na familia zao ndo wanaoingiza hayo makontena toka China?
 
Umejibu kisicho hojiwa, una elimu duni sana, hata kama umesoma.
 
Umejibu kisicho hojiwa, una elimu duni sana, hata kama umesoma.
Mimi n mwalimu tena wa history na literature lakini nafanya kazi kwenye NGO inayohusika na masuala ya kuelimisha jamii tatizo watu wamekariri kuwa mwalimu basi n kwenda kufundisha tu shuleni hy n mawazo mgando
 
Unaendelea kujibu nisicho hoji. Mimi nimesema watu wasisomee ualimu kwa sasa kwa sababu 1,2,3. Wewe unakuja kusema nimedharau ualimu. Umesoma lakini elimu yako ni duni.
 
Unaendelea kujibu nisicho hoji. Mimi nimesema watu wasisomee ualimu kwa sasa kwa sababu 1,2,3. Wewe unakuja kusema nimedharau ualimu. Umesoma lakini elimu yako ni duni.
We mwenyewe uwasilishaji wako m mbovu kajifunze communication skills unatumia command,badala ya kipropose kitu Elimu yako pia n duni kwasababu haikusaidii chochote zaidi ya kukurupuka,Fanya research ndo utoe proposal usikurupuke tu.
 
Sasa hapa umeandika nini, na unategemea nijibu nini. Hilo ni wazo sio lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…