Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Maendeleo ya watu huletwa na watu wenyewe kwa kushirikiana na viongozi bora katka mazingira ya amani, utulivu na upendo.
Kiongozi ambaye siku zote ni kuchochea mpasuko na vurugu hafai hata kidogo.
Nitoe mfano hai kwa kiongozi kama Makonda. Kiongozi huyu ametuhumiwa na kwa ushahidi ulio wazi alipoteuliwa katika nyadhifa mbalimbali kuchochea vurugu ndani ya chama chake, kwa wafanyabiashara na watumishi wa umma. Amehisiwa sana kushiriki uvunjifu wa amani kwa wanasiasa kadhaa na sina haja ya kurudia yaliyosemwa.
Ukisikia lugha anayotumia akiwa jukwaani, siyo ya kimaadili ya kiongozi kwa nchi kama Tanzania. Hata Dr. Nchimbi - Katibu Mkuu CCM alishakemea wazi hadharani hasa matumizi ya lugha za vitisho,matusi kwa watumishi wa Serikali.
Kitendo cha Kiongozi kuhisiwa tu kuwa siyo msafi, muongo [ suala la cheti feki] kilitosha kumwondolea sifa ya uteuzi. Na ndiyo maana tuna vetting.
Swali langu ni je, endapo nia ya kuendelea kuteua watu kama hawa haiko bayana kwa wananchi anaowaongaza nini kifanyike? Je,kuna haja ya Wananchi nao kufanya vetting kwa kuwakataa hadharani viongozi kama hawa?
Ninajua Arusha ni moja ya Mikoa ya kimkakati kwenye tasnia ya utalii. Ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki .
Ni Mkoa unaopokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi. Inahitaji Mkuu wa Mkoa anayejitambua kwenye suala la utulivu, ubunifu, diplomasia nk.
Sina uhakika na maneno ya Mzee mmoja mstaafu aliyewahi kuniambia kuwa, "Ukifanikiwa kuivuruga Arusha,kimbilio la Watalii itakuwa ni Zanzibar" mwisho wa kunukuu. Sijajua kwa uteuzi huu ningefanikiwa kumwona huyo mzee angrlisema nini ukizingatia mteuaji ni kutoka ngambo ile.