Ifike mahali, Wananchi wawakatae Wakuu wa Mikoa wasiofaa. Uteuzi wa Rais siyo msahafu

Ifike mahali, Wananchi wawakatae Wakuu wa Mikoa wasiofaa. Uteuzi wa Rais siyo msahafu

Maendeleo ya watu huletwa na watu wenyewe kwa kushirikiana na viongozi bora katka mazingira ya amani, utulivu na upendo.

Kiongozi ambaye siku zote ni kuchochea mpasuko na vurugu hafai hata kidogo.

Nitoe mfano hai kwa kiongozi kama Makonda. Kiongozi huyu ametuhumiwa na kwa ushahidi ulio wazi alipoteuliwa katika nyadhifa mbalimbali kuchochea vurugu ndani ya chama chake, kwa wafanyabiashara na watumishi wa umma. Amehisiwa sana kushiriki uvunjifu wa amani kwa wanasiasa kadhaa na sina haja ya kurudia yaliyosemwa.

Ukisikia lugha anayotumia akiwa jukwaani, siyo ya kimaadili ya kiongozi kwa nchi kama Tanzania. Hata Dr. Nchimbi - Katibu Mkuu CCM alishakemea wazi hadharani hasa matumizi ya lugha za vitisho,matusi kwa watumishi wa Serikali.

Kitendo cha Kiongozi kuhisiwa tu kuwa siyo msafi, muongo [ suala la cheti feki] kilitosha kumwondolea sifa ya uteuzi. Na ndiyo maana tuna vetting.

Swali langu ni je, endapo nia ya kuendelea kuteua watu kama hawa haiko bayana kwa wananchi anaowaongaza nini kifanyike? Je,kuna haja ya Wananchi nao kufanya vetting kwa kuwakataa hadharani viongozi kama hawa?
Ninajua Arusha ni moja ya Mikoa ya kimkakati kwenye tasnia ya utalii. Ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki .

Ni Mkoa unaopokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi. Inahitaji Mkuu wa Mkoa anayejitambua kwenye suala la utulivu, ubunifu, diplomasia nk.
Sina uhakika na maneno ya Mzee mmoja mstaafu aliyewahi kuniambia kuwa, "Ukifanikiwa kuivuruga Arusha,kimbilio la Watalii itakuwa ni Zanzibar" mwisho wa kunukuu. Sijajua kwa uteuzi huu ningefanikiwa kumwona huyo mzee angrlisema nini ukizingatia mteuaji ni kutoka ngambo ile.
Acha wivu wa kimalaya malaya nyuma ya keyboard
 
Kumekucha.....mutu anapoporewa kila mahali bado USA EMBASSY
 
Hapo bado Makonda hajafika Arusha umeanza kuumwa. Atafika Arusha na Punda atapokelewa na maelfu ya wanaarusha.
 
Ungenijua usingeniandikia comment kama hii. Uliwahi kufika Arusha?
Mkuu mimi naongea uhalisia hakuna asiyejua kwamba Makonda ana ushawishi. Hakuna mtu asiyejua kwamba Makonda atakua maarufu Arusha. Yaani ni sawa na kusema Diamond akitoa nyimbo itakosa views kwenye mitandao ya kijamii.
 
Mama anachojali ni kumdhibiti lema asiingie bungeni hayo mengine hayamuhusu sijui viongozi wa kimataifa,maendeleo ya wananchi nk.
Lengo kumdhibiti Lema.
 
Mkuu mimi naongea uhalisia hakuna asiyejua kwamba Makonda ana ushawishi. Hakuna mtu asiyejua kwamba Makonda atakua maarufu Arusha. Yaani ni sawa na kusema Diamond akitoa nyimbo itakosa views kwenye mitandao ya kijamii.
Ana ushawishi kwenye nini? Na je, watu wa Arusha wanauhitaji huo ushawishi kwenye maendeleo yao?
Anachotaka kushawishi Arusha alishindwaje kufanya hivyo akiwa kwenye cheo alichotoka? Na kwa nini iwe Arusha?
 
Sema wewe unachuki binafsi na Makonda alafu unabisha uhalisia. Usiifundishe akili yako kuukata ukweli tengeneza hoja nyingine lakini sio kupinga kwamba Makonda hana ushawishi.
 
Back
Top Bottom