"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

MKuu ww ungekua yeye ungeweza kumshambulia rais kuwa ni kilaza? Naye ana maisha mengine nje ya haya.
 
Tatizo kubwa ulilo nalo ni kuwa huna msimamo, hausimamii haki, unasimamia maslahi yako na sifa. Ukweli ni kitu muhimu, sikatai kuwa unayo elimu. na intelligence lakini uneshindwa kuitumia vizuri. Nimeona unavyoongea una uwezo mkubwa, lakini Kwa nini umechagua weakness.
 
Wao wameanza kujizungusha huko kwa machifu na kuwataka watuloge sisi tunaoonyesha makosa ya huu mkataba (kutukumbusha kuwa kuna chifu mangungo wa Msovero aliwahi kuuza nchi na watu).

Wao wanasema wameshasaini, sisi tukae kimya. Wamejisahau kuwa wao ni wawakilishi wetu sisi lakini sisi si wawalilishi wao.

Hawajui kuwa tunaweza kuamua kujiwakilishq wenyewe. TUKIAMUA
 
Wakili Pascal Mayalla umeitendea haki fani yako, kwa bandiko hili,

Dominica njema
 


Mtu aliyesoma anielekeze jamaa anapinga au ana support, maana vichwa vya habari vya Paschal havijawahi eleweka.
 
Kawaida yangu huwa sishambulii Mtu Bali hoja yake. Ukija vizuri nakusifu ukija vibaya nakudunda. Japokuwa wewe ni kama mvua za vuli hujulikani utanyesha wapi, lakini Kwa hili bandiko na yale mawili ya Jana umeitendea haki taaluma ya sheria.
Kuna kitu kimoja umekisahau kwenye bandiko lako japo unaweza kusema mhusika umemjumuisha kwenye neno "Serikali". Lakini ungemtenganisha na serikali ingependeza Kwa sababu yeye ana kofia mbili ya Mkuu wa Serikali na Mkuu wa nchi. Swali lako la Tatu lingekuwa Je, tuna Rais wa ajabu?
Maana ukiangalia katika hili yeye ndiye binafsi aliyempa mamlaka ya Kisheria Waziri wake Mbarawa kusaini Kwa niaba ya serikali na nchi ya Tanzania. Anafanya hayo huku akiona wenzake wametoa madaraka Kwa Kakampuni tu badala ya Mtu mwenye mamlaka serikalini. Yaani kampuni ya DPW imekaa kama serikali wakati wa kusaini IGA (hata kama imepiwa power) na ikifika wakati wa HGA hao hao DPW watasimama kama kampuni. Yaani kisoka tunasema DPW ni kocha mchezaji. Mchezaji wa timu A (TPA) akigombana na mchezaji mwenzake (DPW) atatakiwa kulalamikia Kwa kocha wake (Serikali ya Tanzania) ambaye kabla ya yote atatakiwa Kwanza kumuita kocha mwenzake (DPW) ili wawasuluhishe Wachezaji wao. Ukiweka Serikali ya Tanzania iwe mzazi na TPA awe Mtoto na DPW atakuwa Mzazi na Mtoto Kwa wakati mmoja. Wewe uliona wapi ukilaza wa Aina hii?
 
Mungu ametupa NCHI Nzuri mno DUNIANI nzuri sana.

Lakini Bahatimbaya kabisa Tumekuwa na LAANA ya Raslimali.

Hakuna kitu, hakuna wizara, haKuna SEKTA tunayoweza KUJIVUNIA kwa Miaka 60 ya Uhuru.

TUMEJAA UBABAISHAJI.
Hakuna tuwezacho zaidi ya Rushwa, Wizi, Uhujumu uchumi, ubadhirifu wa mali za umma, kujilimbikizia Mali na uchawa.
 
KILA TAASISI KAMA NI URAIS, MAHAKAMA, SERIKALI , POLISI N.K KAMA KUNA UDHAIFU WANAUONESHA HUU WOTE NI KUTOKANA NA KATIBA. KWA KATIBA YA SASA VIONGOZI WOTE NA TAASISI ZOTE LAZIMA KUPOKEA NA KUTII MAAGIZO TOKA KWA RAIS YAWE YA HAKI AU YAWE YASIYOHAKI. DAWA NI KATIBA MPYA TENA ITAKAYOWAPA WANANCHI MAMLAKA KUMPITA YEYOTE HATA RAIS. NASIHI KATIBA IJAYO IITWE KATIBA YA KIDEMOKRASIA NA MAMLAKA YA WANANCHI WA JAMHURI YA TANZANIA.
 
Leo Paskali amendika mambo mazito na muhimu sana. Bandiko ninja kizalendo mno. Pengine una chuki naye tu binafsi. Japo siku hizi ukisikia Prof Shivji kashambuliwa, Dr Slaa kashambuliwa, Prof Tibaijuka kashambuliwa, Lossu kashambukiwa, Jaji Warioba Kashambuliwa, Butiku kashambuliwa, Mwambukuzi kashambuliwa, Mbowe kashambuliwa, Nshala Kashambukiwa n.k., basi ujue wamegonga mahali ambapo watetezi wa Waarabu hawakutaka kusikia
 
Mayala, mara zote mabandiko yako niyauelimishaji jamii lakini cha ajabu serikali ya CCM huweka pamba kwenye masikio na bunge la CCM ndiyo usiseme limekuwa ni bunge la vibweka wanadhani wanaakili kuliko watanzania wote hata waliopewa dhamana Nadhani wanateuliwa kwa ujasiri wao wa kuongea na sio vinginevyo. Taifa limefika hapa tulipo kwasababu ya jamii kujitoa ufahamu, (unyumbu). Herding behavior is an occurrence of entrusted people suspending their individual reasoning because of group objectives, (conflict of interest) or fear of their leaders, (amygdala), by Ipyana Haraba. The aftermath of this behavior is lack of individual decision making and the end result will be disaster or uncertainty inherent
 
Andiko zuri sana.Nawaza hata kama viongozi wetu wanawaza kwa kufikiria matumbo yao ni tumbo gani hilo lisiloshiba?Siku ya mwisho wataondoka Sana Sana nasuti moja vyote walivyokusanya wataviacha.Nenda Loliondo uone Masai mzaliwa anachokipata akikatiza eneo la mwarabu.Sasa Leo bandari zote Tanganyika apewe mtu mmoja tukitaka lolote tumwombe ruhusa mwekezaji.Je Uhuru Nyerere alioupigania si utakuwa umeporwa?
 
Tumewahi kujiuliza migogoro hii ya DP WORLD kwa wenzetu imetoka na nini? Jee huku kutumia nguvu kwa hawa viongozi na machawa wao wanaowatumia kutetea mkataba huu kunatokana na nini?
Jibu la haraka linalokuja ni RUSHWA ndio inayoleta upofu huu. Nasi kama nchi tukizembea tuu, rushwa itashinda na vizazi vitaumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…