"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Sijawahi kukupa like mkuu ila leo nimeitoa.kongole sana kwa bandiko hili la jumapili ya leo.

Nadhani Leo umeenda kifasihi zaidi ya uandishi.shida kubwa iliyopo kwa viongozi wetu ni kuendekeza tamaa na maslahi yao binafsi ndicho kilichotokea tangu mwanzo wa mchakato wa hiyo MoU,kuja IGA na inaenda HGA sasa.

Kwa akili za kawaida tu mtu mwenye akili timamu ukisoma hizo article za hiyo IGA unapata picha halisi ya viongozi tulionao kuwa ni sio vilaza tu Bali ni matutusa ya kupitiliza.

Serikali Haina watu wenye weledi ndio maana hawana hoja Wala utetezi wa kueleweka kuhusu hili la hao waarabu.
Mtu anaulizwa pungufu la mkataba yeye anataja faida zake utamuelewa huyo?
Serikali ina wanasheria vilaza tu na ndio maana wazee wakina mtikila waliyajua haya na wakawa wanashinda kesi dhidi ya serikali tu.

Wanasheria wajitokeze kesi zifunguliwe nyingi sisi raia hata kuchanga pesa tuko tayari hatutachoka ili hii serikali ya CCM tuipige chini wanashindwa kuheshimu wananchi wao hawa na wanajua hatuna Cha kuwafanya.

Mungu Yuko nasi na hili ndio jambo naona kaanza kutupa mwangaza wa kutokea.
 
Nchi inaongozwa na wale maadui nyerere aliowata, wajinga ,maskini na maradhi

UDSM nchio chuo pekeeee kuzalisha maprofesa wajinga kuwahi tokea tanzania hii,

Mtu anajijta profesa wa uchumi, critical thinking & reasoning kwake ni tatizo.
Mimi nadhani hawa maprofesa wana weledi mzuri tu. Njaa zao zinawafanya wajikombe kwa mtawala awweze kuteulwa.Wanategea mweye mamlaka ya uteuzi anataka nini, wanapitia humo humo
 
If possible, ungetoa tu huzo alama za kuuliza. Maana ni ukweli ulio wazi; tuna bunge kibogoyo na lililojaa vilaza, serikali yetu ni ya ajabu, tuna wanasheria vilaza, tunatawaliwa/ongzwa na watu wasio na sifa ya kuitwa watawala/viongozi, nk.
 
Kuhusu bunge letu kitu kinacho waathiri hata leo hii waonekane kama Vilaza niutamaduni waliojijengea, utamaduni wa ndiooo! Hata pale paspositahili kuunga hoja mkono

Matokeo yake wameunga hoja mkono yakupitisha dubwana bila kujuwa
Kuwa kunawakati dubwana hilo hata wao linaweza kuwatafuna tena bila huruma!
Nandio maana leo hii hata wale walio lipitisha hili dubwana wanashangaa
Nivipi walipigwa upofu wa akili hata wakashindwa kuitafsiri IGA! yaani hata tuliyo wategemea wauondeo huu mshangao naopia wanashangaaa🤔
 
Ila Paskali wewe Mungu amekubariki sana kwenye eneo la kuandika. Achilia mbali kuwa taaluma yako
 
Serikali kama inasikia wachukue huu ushauri serious; wapeleke watu kusoma business law haraka sana.

Kama agreement nyepesi kama hii isiyo na consideration wanasheria inawasumbua. Siku wakiwekewea full commercial agreement mtu kakopa sijui wapi mtaji wenyewe, kuna interest za mikopo, interest za inflation, FV ya hela yake, muda wa kurudisha, muda wa kuvuna, changes in external circumstances zinazo athari biashara, changes zinazoathiri interest rate ya mkopo, utakutana na weighted average costs of capital, sensitivity analysis and so on.

Huko kwenye ‘consideration’ kama una uelewa wa ‘advanced financial management’ mjomba utatandikwa utie akili na jamaa watavuna kwa miaka mingi sana huku unawaangalia; ukivunja mkataba mnakutana arbitration.

Kama wanasheria wanashindwa kuelewa njia moja wapo ya ku circumvent sheria zako ni ‘exclusion clause’ na zipo hapo kwenye IGA, kwanza hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza Tanzania na kukubali hiyo sheria ya 2017 it doesn’t protect their investment nadhani ndio sababu ya kuibadili.

Pelekani watu kusoma maswala ya mikataba ya kibiashara hao watu hakuna Tanzania na unapata picha kwanini nchi imekuwa ikishindwa kesi ata za kushinda.

Hiyo IGA aina shida yoyote.
 
huu ni mjadala mpana sana, wewe umechambua upande wa kisheria lakini Kuna pande nyingine ingawa zinagusa pande zote. Kuna sheria za manunuzi je zimefatwa kama kutangaza zabuni na kushindanisha makampuni tofauti?
Tuje kwenye katiba yetu, tuna mamlaka ya bandari ya muungano lakini tumeambiwa haigusi bandari za Zanzibar. Kama mamlaka ya bandari yanaishia bara kwanini wizara ipewe wazanzibar kuongoza? Kwanini mikataba isimamiwe na kusainiwa na wazanzibar bila kuhusisha bandari za upande mwingine wa Muungano kama kweli Zina faida kama wanavyosema.
Kingine tumeungana na watu wabinafsi ambao Chao Chao na Cha kwetu Cha wote.
Walikataa na kuondoa swala la gesi na mafuta kuwa la muungano baada ya kuhisi kuwa Wana hivyo kuwaza rais akitokea bara hataweza kulinda maslahi Yao ;lakini Samia alipoingia madarakani mkataba wa kwanza kusaini ulikuwa na serikali ya Kenya wa kujenga Bomba la gesi. kwanini na sisi tusiwe na mashaka na wao kusaini mikataba inayohusu rasilimali zetu.
 
Mkuu sio vilasa ni rushwa, walichokifanya wanajua.
 
wenzetu timu ya , majadiliano inahusisha watu wa gani tofauti lakini sisi tunabeba wanasheria Tena wasio wabobevu? timu yetu ilitakiwa kuwa na wataamu wa fedha na uchumi, wanasheria wabobevu wa mambo ya ardhi, investment na wabobevu wa mambo ya Kodi.
 
Kiongozi wa bunge anasema watu wanaokosoa huo mkataba hawajawahi hata kupitisha fulana bandarini, ìnaonekana wewe ni miongoni mwao

Mwanasheria wa wizara anasema Proff. Shivji anaposema Tanzania tuna wajibu na DPW wana haki kwenye huu mkataba ni kwasababu ameshindwa kuelewa sijui wenyewe mnaita "birateral" na "hosting" anajua mwenyewe. Yaani kwa lugha rahisi anasema Shivji anaongea jambo asilolijua. Anataka kutwambia Prof. Shivji naye amekua muimba ngonjera tu kama kina Kibajaji hana anachoongea cha maana

Hamza Johari, mwenyekiti aliyesimamia mchakato mzima wa mkataba huo yeye anasema hiyo IGA mnayopigia kelele si lolote si chochote kama TPA na DPW watashindwana kwenye terms zao za kuanza biashara sijui upangishaji na hiyo IGA itakuwa imeishia hapo hapo na DPW hatutaiona tena na hatutadaiwa chochote!

Sasa hapa mjiulize, kama hivyo ndivyo ilivyo kulikuwa na sababu gani ya kujihusisha na hiyo IGA yao. Kwanini wasingewaacha TPA na DPW wamalizane kivyao serikali ifanye monitaring tu. Sasa wewe endelea kumtafuta kilaza ni nani

Wakati nyie mnasema Bandari zote zitakuwa chini ya DPW Bwana Johari yeye anasema ni bandari moja tu ya Dsm na hata hiyo ni kwa asilimia nane tu! Tena wataalamu wa bandari ya Mtwala wanalaumu kuachwa. Yaani kiongozi aliyeongoza mjadala anawashangaa nyie hiyo "exclussivity" ya bandari zote za bahari na maziwa mnayosema imewekwa wapi kwenye hilo andiko? Yeye hakumbuki kama kwenye mjadala aliouongoza hilo swala limo na anawashangaa kweli kweli nyie pamoja na Bwana Chongolo, "nahodha" wa CCM kwa kueneza uongo.

Rais anasema wàkati nyie mnabishana huku jirani zenu wamekimbilia huko huko ili wa-take advantage ya malumbano yenu na bendera yao imebandikwa kwenye jumba lile lile bendera yenu na sura yake vilipobandikwa. Yaani Rais hajui kuwa lile ni tukio la 2019 na letu ni la 2022 hivyo anawasihi muache malumbano badala yake muikimbilie fursa

Sasa wewe endelea kuhoji nani kilaza tu, mapendekezo ya tume ya haki jinai ndio kwanza yamewasilishwa jana hayajaanza kutekelezwa usije ukisumbua familia yako na watu wanaokutegemea
 
Nakuunga mkono [emoji817] taifa lina wanasheria either ni vilaza au wala rushwa? Hakuna mtu mmbaya kama mwanasheria mlarushwa! Yaani unakuta IGA imeandika waziwazi kuwa si uuzwaji wa bandari tu bali na SGR imeuzwa (transport corridor) itakuwa mali ya DP World??? Wanasheria vilaza! Sijui kama kidato cha nne walipata div 4 au 0!
 
HOJA NZITO HIVI ZINAJIBIWA NA CHAWA, SHOGA, CHOKO, KIBAJAJI!
 
wenzetu timu ya , majadiliano inahusisha watu wa gani tofauti lakini sisi tunabeba wanasheria Tena wasio wabobevu? timu yetu ilitakiwa kuwa na wataamu wa fedha na uchumi, wanasheria wabobevu wa mambo ya ardhi, investment na wabobevu wa mambo ya Kodi.
Huko bado, hayo yanafanyika kwenye project agreements. Ndio maana ata kwenye hiyo IGA wanakueleza mikataba hiyo itakuwa siri baada ya kukubaliana.

Ndio tuelewe hiyo IGA aina maajabu yoyote out of the ordinary as far as treaties go. Sasa kama yaliomo humo wanasheria wetu yanawasumbua huko kwenye mikataba ya uwekezaji watakutana na scenarios za ‘probability analysis’ ya mrejesho wa investment on different projection scenarios. Kama uyaelewi hayo mambo investment inayorudisha hela yake kwa miaka 10 unaweza kuwekewa mazingira ikageuka 20 years.

Kwa team ile aliyoenda nayo waziri juzi sijaona mtu pale wa kuingia mikataba ya concession agreements, walau Kakoko ulikuwa ukimsikiliza unaona anauelewa mpana wa maswala ya investment. Hope team iliyokuwa chini yake bado ipo bandarini au serikalini.

Iyo IGA sio lolote, sinema hipo kwenye mikataba inayofuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…