DOKEZO IGP ingilia kati kuhusu huyu Tapeli wa Dodoma Egron Rweyemamu aka Jenerali Mwamwega

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mleta mada, weka wazi, mhanga alikua anatuma hizo hela zote kwa ajili gani?

Cc: PCCB

Yani hao matapeli Wana mtandao mpana. Sasa walimdanganya kwamba Waziri Mkuu atamsadidi kutoa gari bandarini, na yeye kwa ujinga akatuma pesa kwenye namba ya hiyo ya Waziri Mkuu wa mchongo. Ndipo hapo walipobadilika na kuja kivingine Kama mapolisi na kudai ya kwamba ana kesi ya uhujumu Uchumi mpaka Leo wanakula pesa kiulaini.
 
Inasikitisha Sana, kwa Ikulu kukaa kimya muda wote.
 
Wanapeanaje hizo pesa?

Kwa njia ya utapeli. Nakutengezea kosa halafu nakuja Kama polisi kukukamata halafu baadae nakuja Kama Rais au Waziri Mkuu kukusaidia.
 
Sina hakika km wahanga waliripoti utapeli huu polisi..uliona RB? au ni vile tu mtu anasema tumesharipoti polisi..
Polisi hawawezi kukanusha jambo halijafikishwa kwao..! Hata ikulu lazima waulize polisi kabla ya kukanusha km wapo watu wameleta jambo hili kwao..lkn kupitia taarifa za miamala polisi wanaweza kuuliza kampuni za simu kujiridhisha km kweli miamala inayotajwa ipo na inasoma majina gani ya mtumaji na mpokeaji..ni mambo ya uvumi na ujinga ndio maana polisi hawana muda kuhangaika na wajinga..ni ajabu mmekazana kuleta jambo hili hapa wakati ujinga uko wazi kabisa.
 
Una uhakika? Namba za simu sasa hivi ni biometric.. anayechukua pesa akizituma kwani hawezi kumpata ili polisi wamuhoji? Utapewaje kesi wakati miamala ipo na mhusika mpokeaji yupo..utakuwa mpumbavu wa mwisho kuandikishwa kesi ya uhujumu uchumi ukakubali..na jela ndiko unastahili ili ujue gharama ya kuwa mjinga..ukitetea ujinga unakuwa mjinga zaidi ya mjinga unayemtetea.
 
Tumpige kurujuani ngoja niongee na Mzee Magoma.
 
Dah hii kitu imefika Tanzania ,hongera sana nafurahia kuwepo watu Kama nyie Niliowahi waza Ila nikafeli baadhi ya vitu .
Niko tayari kuwa mfanyakazi wako ninayo mengi hasa hapa kijijini njoo tufanye kazi .,Nimefurahi kiasi Cha kutamani nije PM Ila ndiyo vile Pm yangu uwa haukubali kutuma Wala kupokea ,hongera kaka
Kuhusu wateja Kuna jinsi ya kunipata. Hiyo naomba ibaki Siri mpaka mtuhumiwa akamatwe na kupelekwa polisi.
 
Ni aibu mtu kutumia Jina la JWTZ kutapeli watu na bado hakamatwi.
 
Na nyny hamuelimik tu kila siku munatapeliwa kitoto munasumbua serikali tu ina mambo meng ya kufanya.
Ila nchi yetu ina wajinga wengi sana sidhani kama serikali inaweza kuyafuatilia matukio yote ya kitapeli.
Wakati huu tunajadili hapa kuna watu wanampelekea hela kiboko ya wachawi na mwamposa baadae wataanza kuiita serikali iwasaidie wasitapeliwe😀😀😀😀😀
 
IGP saidia raia wako na huyu tapeli Egron Rweyemamu.
 
Waziri Mkuu saidia raia wako na Hawa matapeli wanaitumia jina la Ofisi yako.
 
Kwakweli serikali yetu inanuka Rushwa na uonevu. Mtu mmoja amewaweka polisi wetu kwenye mfuko. Inasikitisha.
 
Watanzania wase
Watanzania wapumbavu sana yaani mtu mmoja tu asiye na Dola anawahenyesha hivi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…