IGP kupinga agizo la Rais, kumfokea na kumkejeli Rais -- hii ni sawa?

Kwenye hii video fupi sana hapa chini Rais Samia anaonekana kutoridhishwa na mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini na kutoa maagizo kadhaa kwa IGP.

Miongoni mwa maagizo aliyotoa Rais kwenda kwa IGP ni pamoja na IGP kuhakikisha kuwa anazuia vifo vya mahabusu,kuzuia matumizi ya nguvu kupindukia kwa raia na kadhalika.

Lakini kama video hii inavyoonekana, IGP aliibuka baadae kupinga maagizo yale,kuyabeza,kumfokea Rais na kumkejeli.

Haya yote yanaibua maswali muhimu sana kwa watanzania.Je,Taifa lina Rais mwenye mamlaka?Kuna watu nchini wameamua kuwa Marais?Rais tulienae ni Rais dhaifu sana?Kuna kundi Serikalini linampinga Rais?Kwa nini Rais hafukuzi hawa wateule wake wanaomdharau?Ni nini hatima ya Taifa hili kama mambo yataendelea kuwa hivi?

Lakini pia katika mazishi ya Polisi waliouawa na Bwana Hamza tulimsikia IGP akitoa kauli za ajabu,zenye utata mwingi,zisizo za kisheria,za kugandamiza na kadhalika.

IGP alisikika akilaumu ndugu wa marehemu kana kwamba ndugu hawa walishirikiana na Bwana Hamza katika kufanya uhalifu ule.Lakini pia IGP alisikika akiwaambia wananchi kuwa wakizubaa zubaa watakuwa wanachezea risasi za Polisi na kadhalika.

My take:
Haya yote yanathibitisha kuwa Taifa lipo chini ya mgogoro mkubwa wa viongozi wasio na uwezo wala hekima za kuongoza na muda wowote ule kuanzia sasa hivi Taifa litatumbukia katika migogoro ya kisiasa,kiuchumi na kijamii.

Kwa maoni yangu haya ni matokeo ya kuongozwa na chama kilichopora chaguzi na ambacho hakina kibali cha wananchi kwani kupora chaguzi husababisha watu wenye uwezo wa kuongoza kuwekwa kando katika kuliongoza Taifa.

View attachment 1914139
Anamuonya Boss wake asiwe na double standard😅😅😅

Haya ndio madhara ya kuingia madarakani kwa mgongo wa vyombo vya ulinzi na usalama badala ya heshima kutoka kwa wananchi.
 
Unaona kabisa kuwa lina kiburi linavyojibu! Loh, kweli linamdharau, Jiwe asingelimjibu hivi/au kutoa comment ya hivi (kama siyo kumjibu).

LINAJIAMINI AU KWA RIDHAA YAKE WAMEPANGA AJIBU HIVYO
Hawa ndio wamewaingiza madarakani kuanzia Diwani wa kata hadi Rais Acha wawe na kibri
 
Yaani mpaka muda huu ilipaswa Kiti cha IGP kiwe hakina mtu....inashangaza sana..ile ilikuwa ni insubordination ya kiwango cha juu sana
 
Nashauri kama Magufuli alivyofanya kwa Magereza kuweka mwanajeshi Mama aweke Mwanajeshi....

Kisha Ma RPC wote wafurushwe nafasi zao wapewe Makanali wa Kijeshi.....
 
IGP alikuwa anaongelea wanaharakati na sio kauli ya raisi, aliyecrop hiyo video ana ill intention
Rais kasema jeshi la polisi linatumia nguvu, IGP anasema "tumeambiwa tunatumia nguvu sana"
 
IGP kakamatwa mchana kweupe akipingana na bosi wake. Hali hii katika uongozi wa nchi haikubaliki na hasa kauli kama hii ikitoka kwa mmoja wa kiongozi wa juu ktk majeshi kuonekana kupingana mtazamo na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Lazima Amiri Jeshi Mkuu aonekana mbele ya macho ya wananchi kuwa ameshika Hatamu za kuongoza majeshi na ikitokea kiongozi mmoja akaonekana anapingana naye kimawazo hadharani, hali hii haikubaliki katika nidhamu na desturi ya vyombo hivi . Inakaribisha watu au wananchi kuanza kuwa na wasiwasi nani has anayeongoza nchi.

1630236997838.pngwww.nytimes.com
Stanley McChrystal, a Top General Fired Over Insults to Biden, Says ...
1 Oct 2020 — On Thursday, General McChrystal added a coda to the story: He endorsed Mr. Biden, now the Democratic presidential candidate, not ...
general Stanley McChrystal by president from www.nytimes.com
 
Mkuu uza duka, hizi siasa zimeshakushinda.

Mtu akiahakua IGP hata akiondolewa itakuwa ni hasara tu kwa walipa kodi maana anahudumiwa na kulindwa mpaka kifo huku wakihudumia IGP atakayekuwa kazini.

Hapa ndipo penye tatizo kati ya wanasiasa na wananchi.

Na ndio maana wanasiasa hata NEC wakisema uchaguzi urudiwe sasa hivi bila kujali gharama ndio furaha yenu ilimradi tu mpate madaraka.
Illogical reasoning
 
Wasaga sumu nyie, inaonekana ndio mliomtuma Hamza akawaue polisi. By the way, kama ningekuwepo Rais mwili wa Hamza ungechomwa moto na kutekezwa kabisaa.
Kwa akili yako unaona maiti ikisikia maumivu wakati wa kuchomwa moto,viongozi watumie hekima muda wote ndiyo maana tunaingia gharama kubwa kuwahudumia wapate utulivu wa akili.
 
Kwenye hii video fupi sana hapa chini Rais Samia anaonekana kutoridhishwa na mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini na kutoa maagizo kadhaa kwa IGP.

Miongoni mwa maagizo aliyotoa Rais kwenda kwa IGP ni pamoja na IGP kuhakikisha kuwa anazuia vifo vya mahabusu,kuzuia matumizi ya nguvu kupindukia kwa raia na kadhalika.

Lakini kama video hii inavyoonekana, IGP aliibuka baadae kupinga maagizo yale,kuyabeza,kumfokea Rais na kumkejeli.

Haya yote yanaibua maswali muhimu sana kwa watanzania.Je,Taifa lina Rais mwenye mamlaka?Kuna watu nchini wameamua kuwa Marais?Rais tulienae ni Rais dhaifu sana?Kuna kundi Serikalini linampinga Rais?Kwa nini Rais hafukuzi hawa wateule wake wanaomdharau?Ni nini hatima ya Taifa hili kama mambo yataendelea kuwa hivi?

Lakini pia katika mazishi ya Polisi waliouawa na Bwana Hamza tulimsikia IGP akitoa kauli za ajabu,zenye utata mwingi,zisizo za kisheria,za kugandamiza na kadhalika.

IGP alisikika akilaumu ndugu wa marehemu kana kwamba ndugu hawa walishirikiana na Bwana Hamza katika kufanya uhalifu ule.Lakini pia IGP alisikika akiwaambia wananchi kuwa wakizubaa zubaa watakuwa wanachezea risasi za Polisi na kadhalika.

My take:
Haya yote yanathibitisha kuwa Taifa lipo chini ya mgogoro mkubwa wa viongozi wasio na uwezo wala hekima za kuongoza na muda wowote ule kuanzia sasa hivi Taifa litatumbukia katika migogoro ya kisiasa,kiuchumi na kijamii.

Kwa maoni yangu haya ni matokeo ya kuongozwa na chama kilichopora chaguzi na ambacho hakina kibali cha wananchi kwani kupora chaguzi husababisha watu wenye uwezo wa kuongoza kuwekwa kando katika kuliongoza Taifa.

View attachment 1914139
IGP anakaidi amri ya rais na anaendelea kupeta tu tunakwenda wapi? Mama tumia akili yako kabla mambo hayajakushinda.
 
Bado mnashindwa kuelewa kuwa hao wote ni kitu kimoja.
Ni Kama kipindi kile Cha mwendazake mlipokuwa mkisema amfukuze makonda
 
Kwenye hii video fupi sana hapa chini Rais Samia anaonekana kutoridhishwa na mwenendo wa Jeshi la Polisi nchini na kutoa maagizo kadhaa kwa IGP.

Miongoni mwa maagizo aliyotoa Rais kwenda kwa IGP ni pamoja na IGP kuhakikisha kuwa anazuia vifo vya mahabusu,kuzuia matumizi ya nguvu kupindukia kwa raia na kadhalika.

Lakini kama video hii inavyoonekana, IGP aliibuka baadae kupinga maagizo yale,kuyabeza,kumfokea Rais na kumkejeli.

Haya yote yanaibua maswali muhimu sana kwa watanzania.Je,Taifa lina Rais mwenye mamlaka?Kuna watu nchini wameamua kuwa Marais?Rais tulienae ni Rais dhaifu sana?Kuna kundi Serikalini linampinga Rais?Kwa nini Rais hafukuzi hawa wateule wake wanaomdharau?Ni nini hatima ya Taifa hili kama mambo yataendelea kuwa hivi?

Lakini pia katika mazishi ya Polisi waliouawa na Bwana Hamza tulimsikia IGP akitoa kauli za ajabu,zenye utata mwingi,zisizo za kisheria,za kugandamiza na kadhalika.

IGP alisikika akilaumu ndugu wa marehemu kana kwamba ndugu hawa walishirikiana na Bwana Hamza katika kufanya uhalifu ule.Lakini pia IGP alisikika akiwaambia wananchi kuwa wakizubaa zubaa watakuwa wanachezea risasi za Polisi na kadhalika.

My take:
Haya yote yanathibitisha kuwa Taifa lipo chini ya mgogoro mkubwa wa viongozi wasio na uwezo wala hekima za kuongoza na muda wowote ule kuanzia sasa hivi Taifa litatumbukia katika migogoro ya kisiasa,kiuchumi na kijamii.

Kwa maoni yangu haya ni matokeo ya kuongozwa na chama kilichopora chaguzi na ambacho hakina kibali cha wananchi kwani kupora chaguzi husababisha watu wenye uwezo wa kuongoza kuwekwa kando katika kuliongoza Taifa.

View attachment 1914139
Tatizo haieleweki kwa nini wapinzani walijiaminisha kwamba samia ni mtu wao ndani ya ccm ie kama vile 5th column. Kwamba akishika urais basi wamechukua nchi. Niwakumbushe tu... Nchi inaongozwa na serikali ya ccm. Haiwezeka mama samia akaendesha nchi kama wapinzani wanavyotaka. Akijaribu kufanya hivyo bila shaka ataingia matatani. Kwa hivyo kufikiri kuna watu wanamkwamisha samia ni namna ileile ya wapinzani kuendesha mambo yao kwa kutegemea uongo na ulaghai.
 
Back
Top Bottom