IGP kupinga agizo la Rais, kumfokea na kumkejeli Rais -- hii ni sawa?

Anamuonya Boss wake asiwe na double standard😅😅😅

Haya ndio madhara ya kuingia madarakani kwa mgongo wa vyombo vya ulinzi na usalama badala ya heshima kutoka kwa wananchi.
 
Unaona kabisa kuwa lina kiburi linavyojibu! Loh, kweli linamdharau, Jiwe asingelimjibu hivi/au kutoa comment ya hivi (kama siyo kumjibu).

LINAJIAMINI AU KWA RIDHAA YAKE WAMEPANGA AJIBU HIVYO
Hawa ndio wamewaingiza madarakani kuanzia Diwani wa kata hadi Rais Acha wawe na kibri
 
Yaani mpaka muda huu ilipaswa Kiti cha IGP kiwe hakina mtu....inashangaza sana..ile ilikuwa ni insubordination ya kiwango cha juu sana
 
Nashauri kama Magufuli alivyofanya kwa Magereza kuweka mwanajeshi Mama aweke Mwanajeshi....

Kisha Ma RPC wote wafurushwe nafasi zao wapewe Makanali wa Kijeshi.....
 
IGP alikuwa anaongelea wanaharakati na sio kauli ya raisi, aliyecrop hiyo video ana ill intention
Rais kasema jeshi la polisi linatumia nguvu, IGP anasema "tumeambiwa tunatumia nguvu sana"
 
IGP kakamatwa mchana kweupe akipingana na bosi wake. Hali hii katika uongozi wa nchi haikubaliki na hasa kauli kama hii ikitoka kwa mmoja wa kiongozi wa juu ktk majeshi kuonekana kupingana mtazamo na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

Lazima Amiri Jeshi Mkuu aonekana mbele ya macho ya wananchi kuwa ameshika Hatamu za kuongoza majeshi na ikitokea kiongozi mmoja akaonekana anapingana naye kimawazo hadharani, hali hii haikubaliki katika nidhamu na desturi ya vyombo hivi . Inakaribisha watu au wananchi kuanza kuwa na wasiwasi nani has anayeongoza nchi.

www.nytimes.com
Stanley McChrystal, a Top General Fired Over Insults to Biden, Says ...
1 Oct 2020 — On Thursday, General McChrystal added a coda to the story: He endorsed Mr. Biden, now the Democratic presidential candidate, not ...
 
Illogical reasoning
 
Wasaga sumu nyie, inaonekana ndio mliomtuma Hamza akawaue polisi. By the way, kama ningekuwepo Rais mwili wa Hamza ungechomwa moto na kutekezwa kabisaa.
Kwa akili yako unaona maiti ikisikia maumivu wakati wa kuchomwa moto,viongozi watumie hekima muda wote ndiyo maana tunaingia gharama kubwa kuwahudumia wapate utulivu wa akili.
 
IGP anakaidi amri ya rais na anaendelea kupeta tu tunakwenda wapi? Mama tumia akili yako kabla mambo hayajakushinda.
 
IGP anakaidi amri ya rais na anaendelea kupeta tu tunakwenda wapi? Mama tumia akili yako kabla mambo hayajakushinda.
Bado mnashindwa kuelewa kuwa hao wote ni kitu kimoja.
Ni Kama kipindi kile Cha mwendazake mlipokuwa mkisema amfukuze makonda
 
Tatizo haieleweki kwa nini wapinzani walijiaminisha kwamba samia ni mtu wao ndani ya ccm ie kama vile 5th column. Kwamba akishika urais basi wamechukua nchi. Niwakumbushe tu... Nchi inaongozwa na serikali ya ccm. Haiwezeka mama samia akaendesha nchi kama wapinzani wanavyotaka. Akijaribu kufanya hivyo bila shaka ataingia matatani. Kwa hivyo kufikiri kuna watu wanamkwamisha samia ni namna ileile ya wapinzani kuendesha mambo yao kwa kutegemea uongo na ulaghai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…