IGP kwenye suala la Lissu chutama, umatusononesha sana Watanzania kwa kumshambulia mhanga kwa maneno badala ya kutafuta wahalifu

Kwa maelezo ya IGP kuwa hakufika kuandikisha maelezo, nahisi pia gari ukipata ajali polisi hawahusiki hadi wahanga wafungue jalada kisha ndiyo ajali hiyo ishughulikiwe na polisi
 
Lisu alikwenda kwa mroto kudai gari lake wala hakutaka kutoa maelezo mengine kuhusu tukio lake.
Lisu na Dereva wake wanajua zaidi kwa nn hawataki kwenda kutoa maelezo yao polisi.
ukiwa na tukio unaweza kwenda polisi hata zaidi ya mara 100.
unacho takiwa kujiuliza je?.
tusiwe wajinga inawezekana Kuna jambo ambalo hatulijui ss washabiki zaidi ya Lisu na Dereva wake, wana siri nzito.
aende akatoe maelezo yake kwa IGP.
Lisu na Dereva wake ndio mashahidi, IGP hakuwepo ktk tukio aliye kuwepo kwenye tukio ni Lisu na Dereva wake.
 
ili kuondoa dhana potofu ktk sakata hili la Lisu ni kwa Lisu na Dereva wake kuamua kwenda kutoa maelezo yao polisi.
 
Kwa maelezo ya IGP kuwa hakufika kuandikisha maelezo, nahisi pia gari ukipata ajali polisi hawahusiki hadi wahanga wafungue jalada kisha ndiyo ajali hiyo ishughulikiwe na polisi

..hapo ni kwenye ajali za barabarani tena zile ndogo-ndogo.

..sio kwa matukio makubwa ya KIGAIDI kama shambulizi lililomtokea Lissu.

..kwa tukio lile Polisi wanatakiwa kulichunguza kwasababu wao ndio wenye wajibu wa kushitaki mahakamani.

..hata wewe au mimi tukishambuliwa na majambazi, polisi ndio watakaowajibika kuwakamata majambazi hao na kuwafungulia mashtaka / kesi.
 
Mficha wahalifu keshaeenda zake,wawaweke hadharani tuwashughulikie, wasiojulikana siku hizi wamevaa dela
 
..hapo ni kwenye ajali za barabarani tena zile ndogo-ndogo.

..sio kwa matukio makubwa ya KIGAIDI kama shambulizi lililomtokea Lissu.

..kwa tukio lile Polisi wanatakiwa kulichunguza kwasababu wao ndio wenye wajibu wa kushitaki mahakamani.

..hata wewe au mimi tukishambuliwa na majambazi, polisi ndio watakaowajibika kuwakamata majambazi hao na kuwafungulia mashtaka / kesi.
Uko sahihi kabisa
 
Lisu alikwenda kwa mroto kudai gari lake wala hakutaka kutoa maelezo mengine kuhusu tukio lake.
Lisu na Dereva wake wanajua zaidi kwa nn hawataki kwenda kutoa maelezo yao polisi.
ukiwa na tukio unaweza kwenda polisi hata zaidi ya mara 100.
unacho takiwa kujiuliza je?.
tusiwe wajinga inawezekana Kuna jambo ambalo hatulijui ss washabiki zaidi ya Lisu na Dereva wake, wana siri nzito.
aende akatoe maelezo yake kwa IGP.
Lisu na Dereva wake ndio mashahidi, IGP hakuwepo ktk tukio aliye kuwepo kwenye tukio ni Lisu na Dereva wake.

..mbona Igp ametoa maelezo tofauti?

..Igp hajasema kwamba Lissu alikataa kuhojiwa na Rpc Muroto.

..kama Lissu alikataa kuhojiwa, au alikaidi wito wa Igp, basi jeshi la polisi lilitakiwa kumkamata.
 
Ukisikiliza tu hoja za IGP, unajua kabisa nani alikuwa nyuma ya shambulizi lile baya dhidi ATL.
 
Ndugu IGP Sirro

Nimesikiliza mahojiano yako uliyofanya na mwanahabari mmoja hapa nchini ,katika mahojiano yako umeonyesha bila chembe ya shaka kuwa hauna interest ya kufuatilia, kuchunguza na hatimaye kuwafikisha katika mkono wa sheria wahalifu waliotenda tendo baya na la kinyama kabisa la kutaka kutoa roho ya Ndugu Tundu Antipass Lissu. Ndugu IGP umetusikitisha sana kwa sababu hizi zifuatazo:

1. Mosi, Unamshutumu Mhanga badala ya wewe kudeal na Wahalifu waliotekeleza jaribio la mauaji:
Ndugu Sirro, nimekusikia maneno yako uliyotoa kwenye kile chombo cha habari, umesema kuwa Lissu ni mkaidi, ukasema eti hakutoa ushirikiano wowote katika kipindi cha kampeni ulipomuita ili umhoji kuhusiana na tukio la shambulio lake. Ndugu Sirro nataka nikukumbushe tu kuwa hata wakaidi wanaowajibu wa kutii sheria bila shuruti. Sasa naomba uueleze umma huu wa Watanzania kwa kuwa Lissu alikataa kutoa ushirikiano katika kuhojiwa Je mlimchukulia sheria gani? Maana kosa alilotendewa Lissu ambalo ni jaribio la mauaji ni kosa dhidi ya Jamhuri na siyo kosa la madai kumhusu Lissu binafsi. Kwa kweli ndugu Sirro, sababu uliyoitoa ya Jeshi la polisi kutofanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa ndugu Lissu ni sababu nyepesi sana inayotufanya tuanze kuwa na mashaka na jeshi la Polisi, Je, Jeshi lako lina kitu gani cha kuficha katika shambulio lile?, Je wewe binafsi una kitu gani cha kuficha katika shambulio. Tueleze sisi wananchi tujue, maana nyie ndo mna dhamana ya ulinzi wa mali na raia. Majibu yako yanaacha wasiwasi mwingi sana

2. Hoja yako kuwa Lissu hajawahi kuripoti popote juu ya kushambuliwa kwake ina walakini:
Ndugu Sirro, usitake kutwambia kuwa kila Jinai ya wazi lazima aliyetendewa jinai ndo akaripoti. Ndugu Sirro, Lissu alikaa kwenye coma zaidi ya wiki moja na amekaa hospitali takriban mwaka mzima, na mpaka leo hii anaendelea bado na operesheni za kujitibia (imebaki moja), Ndugu Sirro je Jeshi la Polisi lilikuwa linangoja mhanga apone ndo muanze uchunguzi? Je, mhanga angekufa maana yake ni kwamba na uchunguzi wa tendo la jinai ndo ungeishia palepale?

Ndugu Sirro kwa nini Jeshi la polisi halijafungua jalada la upelelezi wa suala hilo, Je shahidi wa hilo tukio ni mmoja tu yaani yeye?, kwa nini hamjamuita dereva wake popte alipo kumhoji, na kama ni suspect kwa nini hamkutumia Interpol kumtafuta ili kumhoji?, Mbona hamjahoji majirani, hata wabunge waliokuwa na mheshimiwa Lissu siku hiyo mbona hamkuwaita kuchukua maelezo yao?, Sirro tueleze wewe na Jeshi la Polisi mnajua nini na mnaficha nini?

3. Sirro haukutimiza ahadi yako, uliwaahidi wanasiasa waliokimbia nchi warudi utawapa ulinzi sasa umebadilika:
Mara baada ya uchaguzi mkuu, ulitoka kwenye vyombo vya habari ukiwaambia wanasiasa waliokimbia nchi kufuatia sintofahamu za baada ya uchaguzi kuwa warejee nchini utawapa ulinzi maalum, lakini juzi wakati ukiongea na mwandishi wa habari ulibadili kauli, ukasema hakuna cha ulinzi maalum na kwamba hao wanasiasa ni kama watanzania wengine tu, ukasema kuwa hata watanzania wengine huwa wanashambuliwa na majambazi n.k. Ndugu Sirro, Je unafahamu mtu aliyesurvive risasi 16 atakuwa na hali gani katika kuhofia usalama wake hasa ukizingatia kuwa alitamka mara nyingi kuwa anafuatiliwa na watu kabla ya shambulio lake lakini Jeshi la polisi liliamua kukaa kimya tu?-

Je Ndugu Sirro unataka kutwambia kuwa haimo katika utendaji wa jeshi la polisi kufanyia kazi vitisho, na kauli zenye viashiria vya jinai kutendeka mpaka mtu aripoti polisi? Kama ni hivyo basi jeshi hilo chini yako litakuwa jeshi la ajabu sana!. Kwa hiyo leo kiongozi wa serikali akisema kuwa kuna kitisho dhidi yake hamtofanya lolote mpaka akaripoti polisi?-Sasa inakuwaje mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaita press conference kueleza kufuatiliwa na watu wasiojulikana na kuhofia maisha yake lakini jeshi la polisi lipolipo tu?- Tuambie Sirro, Jeshi lako linajua nini katika hili sakata?

4. Jinai haifi, wananchi tunataka tujue kwa nini Jeshi la polisi halifanyi uchunguzi juu ya tukio la jaribio la mauaji la ndugu Lissu:
Ndugu Sirro, maelezo uliyotoa kwenye vyombo vya habari juu ya hatua ya jeshi la polisi kutofanya lolote juu ya jaribio la mauaji ya ndugu Lissu ni maelezo mepesi sana, hayajasheheni sababu kuntu za kipolisi, za kiupelelezi na kwa kweli za kisheria. Sasa tunataka tujue ni lini jeshi la polisi litafungua jalada la upelelezi wa tukio la kumpiga risasi ndugu Lissu?, tunataka kuona wito wa kisheria wa kipolisi wa kuita mashahidi ili tuone kweli uchunguzi umefanyika, wahalifu wanafikishwa katika mkono wa sheria na haki inatendeka. Tunapotaka hivi hatumaanishi kuwa matukio yaliyowakumba wengine yasifanyiwe uchunguzi, la hasha, lakini uchunguzi wa tukio fulani hauzuii uchunguzi wa tukio jingine. Ndugu IGP tunaomba majibu

5. Mwisho kabisa ndugu IGP naomba ufahamu yafuatayo:
Sisi watanzania tuliumizwa sana na tukio la kinyama alilofanyiwa mtanzania mwenzetu ndugu Lissu, tulilia naye, tulimuombea Kwa Mwenyezi Mungu amponye. Ukatili ule uliofanywa juu yake wa kumpiga risasi zote zile utadhani watu walitaka kuua Chatu ni ukatili usio na mithili. Kila nikiufikiria ukatili roho yangu inagumia. Sisi Watanzania tuna haki ya kujua akina nani walihusika ili mkono wa sheria uwe juu yao. Ndugu Sirro unavyopiga chenga au kujivutavuta katika kufanya uchuhunguzi wa hili suala, na kadri unavyoongea kwa nguvu nyingi kulifunika ndivyo nasi tunakuwa tukufikiria vibaya sana. Tafadhali usistaafu huku damu ya Lissu iliyomwagika bila hatia pale Dodoma ikiwa inakulilia kudai haki yake. Wewe hapo ulipo unaweza kuamua uchunguzi wa hili suala ufanyike ili tujue umetimiza wajibu wako, na ukishindwa unawe mikono kama Pilato tujue. Ndugu Sirro, Watanzania tuna interest ya kujua juu ya jinai ile kwa sababu inahusu maslahi ya viongozi wetu tunaowachagua, kama mkiwaachia wahalifu kwenda free basi watarudia tena hayo matendo huko mbeleni, ndiyo maana sisi watanzania tunataka mfanye uchunguzi, wahalifu wajulikane na sheria ichukue mkondo wako!

IGP SIRRO KABLA HUJASTAAFU TANATAKA KUONA UKITENDA HAKI KATIKA DHULMA HII MBAYA KABISA ILIYOWAHI KULIKUMBA TAIFA LETU
Jinai haifi. Wanachelewesha tu lakini hata baada ya miaka 30 itakula kwao.
 
Mwache aende Kiabakari kijiji cha wanawake! tutamfuata huko huko! Lakini huyu anaweza kupofuka kwa laana alizochuma! Uwe uwavyo Siro lazima utujibu Nani aliyetuma wauaji kumuangamiza Lissu na walikuwa akina nani?
Kuna mwenzako Tibaigana alianza kuropoka ulevini akatekwa akafanywa bubu! sasa unangoja hadi ustaafu?
 
Lissu anakataa kutoa ushirikiano na IGP anakataa kufanya uchunguzi! Ngoma droo. Na nyinyi wapambe wa Lissu msifikiri watanzania wote tumeumizwa na matatizo ya Lissu! Hata wakina Amsterdam wamemkacha.
Na wewe Lissu, usiwe una andika humu JF kwa identity ya bandia ukitafuta huruma! Maana huyu alie andika haya ni wewe Lissu.
waandishi wa haya mavi kama huyu ni mandata aka viatu aka jino, polisi ambao hawakusoma wamefoji vyeti na wanaishi kusujudia mamlaka!
 
Kwahiyo we unatakaje?

Alafu tabia ya kipumbavu ya kusema sisi watanzania tuliumia sana unakosea ina manisha umenijumuisha na mimi.Ukwel ni kuwa sikuumia kabisa angekufa tu.Jiseme nafsi yako.

Siyo lazima uwemo wewe na basically haumo kwa sababu si miongoni mwa watanzania walioumia...

Lakini ametumia nafsi ya "watanzania tuliowengi....." kwa sababu tuliowengi ni mimi, yeye na wengine. Wewe haumo kabisa, na hufai kuwemo. Hivyo jiondoe kabisa, give us space....
 
Nadhani wengi wenye elimu na Akili waliumia na kukasirika sana kumsikia Sirro akijibu kama alivyojibu! Alijibu bila huruma kama vile anaongelea mnyama aliyekoswakoswa!! Nilidhani ni mtu wa hekima lakini kutokana na ulivyojibu sina respect for him tena!! Mungu akurudishie kiasi cha matamshi yako ya kukejeri raia mwema kama Lisu!! Mungu akulipe kwa stahili ya maneno yako!!
 
Yani jeshi la kipumbavu kuliko yote duniani ni hili jeshi la polisi Tanzania.

Ishu ya lissu itaishi igp siro hata mifupa yako itafukuliwa kaburini mwaka 2300 tujue ilikuwa mtu wa Aina gani wakati huo magufuli matamahuluku yake yatakuwa fosili fuel.
 
..kama dereva ni suspect basi jeshi la polisi linatakiwa kuwataarifu Interpol na polisi wa Ubelgiji ili dereva huyo akamatwe na kurejeshwa nchini.

..huo ndio utaratibu unaotumika kuwakamata watuhumiwa waliotoroka nchini kwao, au eneo walikotenda uhalifu.
Kwa nini dereva haji kwa hiari yake ili kusaidia upelelezi kwenye kuumizwa kwa bosi wake?
 
..hilo swali lingeweza kujibiwa na Polisi kama wangewaomba Interpol wamkamate dereva huyo na kumrejesha Tz ili atoe ushahidi.
 
Hiyo hatakuwa hiari tena! Nasema aje mwenyewe asaidie, kwa mapenzi yake siyo interpol kuhusika. Kwani yeye haoni kuwa ni muhimu katika upelelezi huu. Akija, na Lissu akatoa ushirikiano, basi tutabaki tunalaumu polisi kwamba hawafanyi kazi au Walihusika! Hawa watu wawili walikuwepo wanapaswa waisaidie polisi iwasaidie.
 
Kwahiyo we unatakaje?

Alafu tabia ya kipumbavu ya kusema sisi watanzania tuliumia sana unakosea ina manisha umenijumuisha na mimi.Ukwel ni kuwa sikuumia kabisa angekufa tu.Jiseme nafsi yako.

Anawasemea wale wote walioguswa na kuumizwa na kadhia hiyo ya kinyama.
 
Back
Top Bottom