IGP mtimue au mfute kazi RPC wa Dodoma ikikupendeza

IGP mtimue au mfute kazi RPC wa Dodoma ikikupendeza

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
7,762
Reaction score
7,100
Nimesoma taarifa ya RPC wa Dodoma juu ya sakata la unyanyasaji wa kingono aliofanyiwa Binti moja ambaye taarifa zake zilisambaa na kujadiliwa Sana mitandaoni na kwenye vyombo vingi vya habari.

Taarifa yake imekosa weledi wa kitaalamu na imekaa Kama ya kumlinda mhusika mkuu wa tukio lile. Afande RPC ni mwanamke kwa jinsi yake na ameshindwa kumtetea mwanamke mwenzake angalau kupata haki zake. Hii ni aibu na imepangwa na aliyepanga kaacha matundu mengi ya kulichafua Jeshi la polisi.

Kwa maana nyingine polisi Tena wenye madaraka na vyeo wanaharakisha kulichafua jeshi la polisi hivyo IGP chukua hatua na kwa kuanzia mtumbue huyu RPC wa DODOMA.
 
1000031903.jpg
 
😀 kulikua hakuna tena haja ili suala kuliongelea kwenye vyombo vya habar naona ata uko mitandaoni limeshaisha wamekuja kulifufua tena upya.
Ukishaamua kuwa upande wa uonevu haina haja ya kuleta ubabe kukaa kimya ni bora zaidi
serikali sjui inafeli wapi.
 
watz acheni ujinga hata namna ya kuelewa vitu kauli inasema alikuwa ni kahaba na haijasema ukimbaka kahaba sio kosa!,swala ni kwamba ametaja wasifu wa huyo mmbakwaji kama ambavyo walivyotajwa wale maasikari!.. nafikiri watu mnahitaji uyakinifu namna yakuchambua habari pia waandishi ktk maelezo huchukua maelezo yanayovutia zaidi nakuyaweka kama kichwa cha habari ili iwavute watu!.. mbona mnakuwa na fikra pungufu hivi...?
mnachotakiwa kuhoji ni ukahaba wa huyo dada na kama kweli ni kahaba basi nae anatakiwa kuchukuliwa hatua kama zipo sheria zinazokataa ukahaba kwenye jamii yetu!.
 
Back
Top Bottom